097-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kumuombea Mtu katika Adhabu (Hadd)

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب تحريم الشفاعة في الحدود 

097-Mlango Wa Uharamu wa Kumuombea Mtu katika Adhabu (Hadd)

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ  ﴿٢﴾

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme mpigeni kila mmoja katika wawili hao mijeledi mia. Na wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika Hukmu ya Allaah mkiwa nyinyi mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. [An-Nuwr: 2]

 

 

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ قُرَيْشاً أهَمَّهُمْ شَأْنُ المَرْأَةِ المَخْزُومِيَّةِ الَّتي سَرَقَتْ ، فقَالُوا : مَنْ يُكَلِّمُ فِيهَا رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ؟ فقالوا : وَمَنْ يَجْتَرِئُ عَلَيْهِ إِلاَّ أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ ، حِبُّ رَسُولِ اللهِِ صلى الله عليه وسلم . فَكَلَّمَهُ أُسَامَةُ ، فَقَالَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( أتَشْفَعُ في حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللهِ تَعَالَى ؟! )) ثُمَّ قَامَ فاخْتَطَبَ ، ثُمَّ قَالَ : (( إنَّمَا أهْلَكَ الَّذِينَ قَبْلَكُمْ أنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيِهمُ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ ، وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الضَّعِيفُ ، أَقَامُوا عَلَيْهِ الحَدَّ ، وَايْمُ اللهِ لَوْ أنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا )) . متفق عَلَيْهِ .

وفي روايةٍ : فَتَلوَّنَ وَجْهُ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( أتَشْفَعُ في حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللهِ !؟ )) فَقَالَ أُسَامَةُ : اسْتَغْفِرْ لِي يَا رَسُولَ اللهِ . قَالَ : ثُمَّ أَمَرَ بِتِلْكَ المَرْأَةِ فَقُطِعَتْ يَدُهَا .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Maquraysh walikuwa na hamu sana kwa kesi ya mwanamke kutoka katika Makhzuum ambaye kwamba aliiba, wakasema: "Nani atazungumza na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya jambo hilo?" Wakasema: "Nani anaweza kuzungumza naye ila Usamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye ni kipenzi cha Rasuli wa Allaah?" Usamah alikwenda na kuzungumzu naye, hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Unamuombea msamaha kwa Hadd (adhabu) miongoni mwa adhabu alizotoa Allaah Ta'aalaa?" Kisha alisimama na kuhutubia watu kwa kusema: "Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu alipoiba mtukufu miongoni mwao alikuwa akiachiliwa na anapoiba dhaifu miongoni mwao basi walikuwa wakimuadhibu. Naapa kwa Allaah! Lau Faatimah bint Muhammad angeiba basi ningemkata mkono wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah nyengine: "Uso wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ulibadilika rangi (kwa ghadhabu)." Akasema: "Unamuombea msamaha kwa Hadd miongoni mwa adhabu alizotoa Allaah?" Akasema Usamah (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Ee Rasuli wa Allaah! Niombee msamaha." Akasema: "Kisha akaletwa yule mwanamke, hivyo kukatwa mkono wake." 

 

 

Share