098-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kwenda Haja Njiani, Mapito ya Watu, Sehemu ya Vivuli, katika Maji na Mfano wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب النهي عن التغوط في طريق الناس

وظلِّهم وموارد الماء ونحوها

098-Mlango Wa Kukatazwa Kwenda Haja Njiani, Mapito ya Watu, Sehemu ya Vivuli, katika Maji na Mfano wake

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]

 

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( اتَّقُوا اللاَّعِنَيْنِ )) قالوا : وَمَا اللاَّعِنَانِ ؟ قَالَ : (( الَّذِي يَتَخَلَّى في طَرِيقِ النَّاسِ أَوْ في ظِلِّهِمْ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ogopeni laana mbili." Akaulizwa: "Na ni zipi hizo laana mbili?" Akasema: "Ni yule ambaye anakidhi haja yake katika ya njia inayotumiwa na watu au katika kivuli chao (sehemu ambayo watu hupumzika)." [Muslim]

 

Share