107-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kumsifu Mtu Mbele Yake kwa Anayehofiwa Ufisadi Kama Vile Kiburi na Mfano Wake na Kufaa kwa Yule Anayeaminiwa katika Haki Yake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهة المدح في الوجه لمن خيف عليه مفسدة

من إعجاب ونحوه ، وجوازه لمن أمِنَ ذلك في حقه

107-Mlango Wa Ukaraha wa Kumsifu Mtu Mbele Yake kwa Anayehofiwa Ufisadi Kama Vile Kiburi na Mfano Wake na Kufaa kwa Yule Anayeaminiwa katika Haki Yake

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه قال : سَمِعَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم رَجُلاً يُثْنِي عَلَى رَجُلٍ وَيُطْرِيهِ في المِدْحَة ، فقالَ : (( أهْلَكْتُمْ – أوْ قَطَعْتُمْ – ظَهْرَ الرَّجُلِ )) . متفق عليه .

Amesema Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu mmoja akimsifu mwenziwe na kutupa mipaka katika kumsifu, akasema: "Amemuangamiza (amemuua) au ameuvunja mgongo wa huyo mtu." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

Hadiyth – 2

وعن أبي بكرة رضي الله عنه : أنَّ رجلاً ذُكِرَ عند النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَأَثْنَى عَلَيْهِ رَجُلٌ خَيْراً ، فقال النبيّ صلى الله عليه وسلم : (( وَيْحَكَ ! قَطَعْتَ عُنُقَ صَاحِبِكَ )) يَقُولُهُ مِرَاراً : (( إنْ كَانَ أحَدُكُمْ مَادِحاً لاَ مَحَالَةَ فَلْيَقُلْ : أحْسِبُ كَذَا وَكَذَا إنْ كَانَ يَرَى أنَّهُ كَذَلِكَ وَحَسِيبُهُ اللهُ ، وَلاَ يُزَكّى عَلَى اللهِ أحَدٌ )) . متفق عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mara moja mtu mmoja alitajwa mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na mtu mwengine akamsifu kwa kheri. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ole wako! Umekata shingo ya sahibu yako." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikariri jambo hilo: "Ikiwa mtu hana budi mpaka amsifu (mtu yeyote), aseme: 'Ninamuhesabu (ninamchukulia) yeye ni kadha na kadha, ikiwa kweli anaona kuwa yeye yuko hivyo na Allaah Atamhesabu kwa hilo, wala hakuna anayeweza kujisifu kwa usafi mbele ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن همام بن الحارث ، عن المِقْدَادِ رضي الله عنه : أنَّ رَجُلاً جَعَلَ يَمْدَحُ عُثْمانَ رضي الله عنه ، فَعَمِدَ المِقْدَادُ ، فَجَثَا عَلَى رُكْبَتَيْهِ ، فَجَعَلَ يَحثو في وَجْهِهِ الحَصْبَاءَ . فقالَ لَهُ عُثْمَانُ : مَا شَأنُكَ ؟ فقال : إنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إذَا رَأَيْتُمُ المَدَّاحِينَ ، فَاحْثُوا فِي وُجُوهِهِمُ التُّرَابَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoks kwa Hammaam bin Al-Haarith kutoka kwa Al-Miqdaad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtu mmoja alikuwa akimsifu 'Uthmaan (Radhwiya Allaahu 'anhu). Miqdaad alipiga magoti na kuanza kumrushia changarawe mdomoni mwa mzungumzaji. Akamwambia yeye 'Uthmaan (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Una nini wewe (mbona unafanya hivyo)?" Akasema (Miqdaad): "Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 'Mukimuona mtu anamsifu mwenziwe mbele yake, basi mtieni usoni mwake mchanga'." [Muslim]

 

 

فهذهِ الأحاديث في النَهي ، وجاء في الإباحة أحاديث كثيرة صحيحة .

قال العلماءُ : وطريق الجَمْعِ بين الأحاديث أنْ يُقَالَ : إنْ كان المَمْدُوحُ عِنْدَهُ كَمَالُ إيمانٍ وَيَقينٍ ، وَرِيَاضَةُ نَفْسٍ ، وَمَعْرِفَةٌ تَامَّةٌ بِحَيْثُ لاَ يَفْتَتِنُ ، وَلاَ يَغْتَرُّ بِذَلِكَ ، وَلاَ تَلْعَبُ بِهِ نَفْسُهُ ، فَليْسَ بِحَرَامٍ وَلاَ مَكْرُوهٍ ، وإنْ خِيفَ عَلَيْهِ شَيءٌ مِنْ هذِهِ الأمورِ ، كُرِهَ مَدْحُهُ في وَجْهِهِ كَرَاهَةً شَديدَةً ، وَعَلَى هَذا التَفصِيلِ تُنَزَّلُ الأحاديثُ المُخْتَلِفَةُ فِي ذَلكَ .

 

وَمِمَّا جَاءَ فِي الإبَاحَةِ قَولُهُ صلى الله عليه وسلم لأبي بكْرٍ رضي الله عنه : (( أرْجُو أنْ تَكُونَ مِنْهُمْ )) أيْ مِنَ الَّذِينَ يُدْعَونَ مِنْ جَمِيعِ أبْوابِ الجَنَّةِ لِدُخُولِهَا . متفق عليه .

وَفِي الحَدِيثِ الآخر : (( لَسْتَ مِنْهُمْ )) : أيْ لَسْتَ مِنَ الَّذِينَ يُسْبِلُونَ أُزُرَهُمْ خُيَلاَءَ . رواه البخاري .

وَقالَ صلى الله عليه وسلم لعُمَرَ رضي الله عنه : (( مَا رَآكَ الشَّيْطَانُ سَالِكاً فَجّاً إلاَّ سَلَكَ فَجّاً غَيْرَ فَجِّكَ )) . متفق عليه .

 

والأحاديثُ في الإباحة كثيرةٌ ، وقد ذكرتُ جملةً مِنْ أطْرَافِهَا في كتاب " الأذكار"

 

Wamesema wanazuoni: Na njia ya kuoanisha baina ya Hadiyth ni kauli: Ikiwa kusifiwa mbele yake yule mwenye ukamilifu wa Imani na yakini na mtu anaye inyima nafasi yake na mwenye maarifa barabara ya maadili ya Dini, hivyo kutofitinika wala kuhadaika wala nafsi yake haitamchezea kwa hilo. Katika mas-ala haya ya kusifiwa hakutakuwa haramu wala makruhu. Na ikiwa anahofiwa kwa mambo haya yaliotajwa, inakuwa  ni makruhu kumsifu mbele yake, na ukaraha ni mkali na mzito zaidi. Na kwa mujibu wa tafsili hizi tunapata Hadiyth tofauti katika hilo. Na katika Hadiyth zinazoelezea kuruhusiwa kumsifu mtu mbele yake ni:

 

Kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Ninatarajia kuwa utakuwa miongoni mwao." [Al-Bukhaariy na Muslim], yaani miongoni mwa wale watakaoitwa kuingia Peponi kwa kupitia milango yote.

 

Na Hadiyth nyengine: "Wewe si miongoni mwao." [Al-Bukhaariy], yaani wewe ni katika wale wanaoburuza vikoi vyao kwa kiburi.

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Shetani hakuoni ukitembea njiani isipokuwa huacha njia hiyo na kuchukua nyengine." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na Hadiyth katika mlango huu ambazo zinaruhusu kumsifu mtu mbele yake ni nyingi, baadhi yake nimezitaja katika kitabu changu cha al-Adhkaar.

 

 

Share