106-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kurudisha Zawadi ya Manukato Bila Udhuru

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب كراهة رد الريحان لغير عذر

106-Mlango Wa Ukaraha wa Kurudisha Zawadi ya Manukato Bila Udhuru

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ عُرِضَ عَلَيْهِ رَيْحَانٌ ، فَلاَ يَرُدَّهُ ، فَإنَّهُ خَفيفُ المَحْمِلِ ، طَيِّبُ الرِّيحِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kupatiwa zawadi ya manukato asirudishe, kwani ni nyepesi kubebwa na yenye harufu nzuri." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أنس بن مالكٍ رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ لاَ يَرُدُّ الطِّيبَ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa ni mwenye kurudisha zawadi ya manukato. [Al-Bukhaariy]

 

Share