30-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Ndoa Ambazo Ni Batili Kisharia:Ndoa Ya Siri (Ndoa Isiyosajiliwa Rasmi)

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

  الأَنْكِحَةُ الفَاسِدَةُ شَرْعًا

Ndoa Ambazo Ni Batili Kisharia

 

 

Alhidaaya.com

 

 

30:  Ndoa Ya Siri (Ndoa Isiyosajiliwa Rasmi):

 

Ndoa inayokusudiwa hapa ni ile tabia iliyoenea kati ya vijana ambapo kijana hutokea akafanya mahusiano na msichana ambaye anaweza kuwa ni mwanafunzi mwenzake chuoni.  Mahusiano kati yao yanakuwa ni ya siri bila yeyote kujua, au wanaweza kujua baadhi ya marafiki wao wa karibu sana.  Kisha wawili hao huanza kufanya mapenzi katika sehemu yoyote ya siri, halafu msichana anarudi nyumbani kwao kama kawaida bila wazazi wake kujua chochote kinachoendelea.  Mahusiano haya yanakuwa kwenye karatasi tu ambayo inakuwa haitambuliwi na vyombo husika vya dola, na mashahidi wao wanakuwa ni hao hao marafiki zao mafasiki.

 

Ndoa hii ni batili, bali kiuhalisia ni zinaa, kwa kuwa imekosa sharti miongoni mwa shuruti za ndoa ambayo inakuwa haifai bila kuwepo, nayo ni idhini ya walii wa mwanamke.   Qur-aan na Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimeshurutisha uwepo wa walii ili ndoa iwe sahihi.  Na huu ndio msimamo wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa.  Na kwa msingi huu, ndoa hii ni lazima ivunjwe.

 

 

                                  

 

Share