31-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Sifa Ambazo Mke Na Mume Wanatakiwa Kuwa Nazo: Mke

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

 

 

الصِّفَاتُ المطْلُوْبَةُ في الزَّوْجَينِ

 

Sifa Ambazo Mke Na Mume Wanatakiwa Kuwa Nazo:

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

31. Sifa Ambazo Inapendeza Mke Kuwa Nazo: Mke

 

1-  Awe ameshika dini: 

 

Ni kwa Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ"

 

“Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni”.  [Al-Baqarah: 221] 

 

Na kwa kauli ya Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam):

 

"فَاظْفَرْ بِذَات الدِّيْنِ تَرِبَتْ يَدَاكَ"

 

“Basi mpanie mwenye dini, (la sivyo) utaharibikiwa”.  [Hadiyth Swahiyh]

 

2-  Akiwa ni mwenye dini, jamala, nasaba njema na mali, itakuwa ni bora zaidi:

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"تُنْكَحُ الْمَرْأَةُ لِأَرْبَعٍ: لِمَالِهَا وَلِحَسَبِهَا وَلِجَمَالِهَا وَلِدِينِهَا، فَاظْفَرْ بِذَاتِ الدِّيْنِ تَرِبَتْ يَدَاكَ"

 

“Mwanamke huolewa kwa moja ya mambo manne:  Kwa mali yake, kwa hadhi yake, kwa uzuri wake, na kwa dini yake.  Basi mpanie mwenye dini, (la sivyo) utaharibikiwa”.  [Al-Bukhaariy (5090) na Muslim (1466)]

 

3-  Awe mpole mwenye huruma:

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"خَيْرُ نسَاء رَكِبْنَ الْإِبِلَ صَالحَ نِسَاء قُرَيْش أَحْنَاهُ عَلَى وَلَدٍ فِي صِغَرِهِ وَأَرْعَاهُ عَلَى زَوْجٍ فِي ذَاتِ يَدِهِ"

 

“Wanawake bora zaidi waliopanda ngamia, ni wanawake wema wa Kiquraysh.  Wana huruma mno kwa watoto wadogo, na wanasimamia vyema mali za waume zao”.  [Al-Bukhaariy (5082) na Muslim (2527)]

 

4-  Inapendeza zaidi akiwa bikra:

 

Ni pale Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomuuliza Jaabir bin ‘Abdillaah alipooa:  Je, ni bikra au mkubwa (aliyewahi kuolewa)?  Akamwambia:  Ni mkubwa.  Akamwambia: 

 

فَهَلاَّ بِكْرًا تُلاَعِبُهَا وَتُلَاعِبَكَ"

 

“Kwa nini usioe bikra ukamchezea naye akakuchezea?”  [Al-Bukhaariy (5079) na Muslim (715)]   

 

Ni vyema mno kuoa bikra isipokuwa kama kuna sababu ya nguvu ya kuoa mwanamke aliyewahi kuolewa, kama kupata ukwe wa watu wema, au kumliwaza aliyefiwa na mume wake, au kulea mayatima na mfano wa hayo.

 

5-  Awe mzuri, mtiifu na mwaminifu:

 

Ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa kuhusu mwanamke aliye bora zaidi, akajibu:

 

"الَّتِي تَسُرُّهُ إِذَا نَظَرَ، وَتُطِيعُهُ إِذَا أَمَرَ، وَلَا تُخَالِفُهُ فِيمَا يَكْرَهُ فِيْ نَفْسِهَا وَلَا فِيْ مَالِهِ"

 

“Ni yule ambaye mumewe anafurahi anapomwangalia, anamtii anapomwamrisha, na haendi kinyume naye katika yale asiyopenda yeye kuwa nayo wala katika mali yake”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na An-Nasaaiy (6/68) na Ahmad (7373)]

 

6-  Awe mwenye penzi na mwenye kizazi:

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza hili kama zilivyogusia Hadiyth zilizotangulia nyuma.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share