Kamba Wa Toast

Kamba Wa Toast 

 

Vipimo

Kamba wa maganda bila vichwa - 500 grams

Unga ngano - 1 kikombe cha chai

Yai - 1

Pilipili ya unga kijiko - ½ cha chai

Bizari ya manjano kijiko - ½ cha chai

Chumvi - kiasi

Mafuta Ya Kukaangia - kiasi

Namna ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Changanya yai, pilipili, bizari na chumvi kwenye bakuli.   
  2. Osha kamba usiwatowe maganda, watoe vichwa.
  3. Ukishawaosha vizuri mimina kamba kwenye huo mchanganyiko, halafu mimina na unga.
  4. Bandika mafuta kwenye karai yakishakupata moto, kaanga kamba mpaka wawe rangi ya hudhurungi (golden brown). Moto uwe wa kiasi.
  5. Tayari kwa kuliwa na mkate au chips, au saladi.

 

 

 

Share