Zakaatul-Fitwr: Anapata Misaada Ya Kulea Yatima, je Atoe Zakaatul-Fitwr?

Anapata Misaada Ya Kulea Yatima, je Atoe Zakaatul-Fitwr?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

swali langu ni mimi nina watoto yatima watatu katika mwezi huu tukufu wa Ramadhani watu wananilete sadaka mbali mbali kama vile mchele, na wakati mwingine wananipa pesa, sasa nauliza katika hivi vitu wanavo nipa ninaweza nikatoa na mimi zakatil fitri?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Ikiwa pesa unazopata zinakutosheleza kuwatimiza haja zao yatima unaolea pamoja na wewe mwenyewe na unaweza bado kumiliki chakula cha siku ya 'Iyd, basi inakupasa utoe Zakaatul-Fitwr kujilipa wewe mwenyewe pamoja na pia kuwalipa Mayatima unaowalea wote kwa kiwango cha saa' moja kila mtu. Hii ni kwa sababu Zakaatul-Fitwr imefaridhishwa kwa kima Muislamu, kama ilivyothibitika katika dalili ifuatayo:

 

عَن ْابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَاقَالَ: " فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِصَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ صَاعًا مِنْتَمْرٍ أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ عَلَى الْعَبْدِ وَالْحُرِّوَالذَّكَرِ وَالأنْثَى وَالصَّغِيرِ وَالْكَبِيرِ مِنْالْمُسْلِمِينَ". البخاري

 

Kutoka kwa bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma): "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya Zakaatul-Fitwr ni fardhi kwa mtumwa na aliye huru, mwanamume na mwanamke, mdogo na mkubwa miongoni mwa Waislamu kwa kutoa swaa' moja ya tende kavu au swaa' moja ya shayiri" [Al-Bukhaariy] 

 

*swaa' (pishi) moja = kilo mbili na nusu hadi tatu au (mteko) viganja viwili vya mkono vya mtu wa wastani vilivyojaa mara nne.

 

Tafadhali soma Fataawa katika viungo vifuatavyo:

 

Fataawaa: Za Zakaatul-Fitwr

Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Za Zakaatul-Fitwr

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share