Umri Anaotakiwa Mtoto Mchanga Kunyolewa Nywele

SWALI:

asalam aleikhum,inshaala mwenyezi mungu awajaalie nyinyi pamoja na vizazi vyenu,kwa kutuelimisha.swali langu ni,ni umri gani inafaa kumkata mtoto mchanga nywele,shukrani


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa du'aa zenu nzuri mnazotuombea nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia ALHIDAAYA kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Atutakabalie hizo du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelimishana kwa kadiri Anavyotujaalia.

 

Kumnyoa nywele mtoto mchanga imekuja katika mafunzo ya Sunnah ni pale anapotimia umri wa siku saba. Hivyo ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa wajukuu zake na dalili ifuatayo imethibitisha kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 ((Kila mtoto amefungika na ‘Aqiyqah yake, itachinjwa kwa ajili yake siku ya saba na atapewa jina, na atanyolewa kichwa chake)) [Ahmad na An-Nasaaiy]

 

Kwa maelezo zaidi soma maelezo katika viungo vifuatavyo:

 

Utaratibu Wa 'Aqiyqah Katika Sunnah

Kufanya Aqiyqa Ni Lazima Au Sunnah?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share