Keki Za Icing Mbali Mbali Za Vikombe

Keki Za Icing Mbali Mbali Za Vikombe

 

Vipimo:

Unga wa keki wa tayari - 1 boksi (510 g)

Maji - 1 ¼ kikombe cha chai

Mafuta - 1/3 kikombe cha chai

Mayai - 3

Malai (whipped cream) - 2 vikombe viwili

Marembo yake ya rangi na kiasi

chengachenga za pipi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Washa jiko (oven) moto wa 350F° ama 180°C na utayarishe tray ya keki za vikombe kwa kupaka mafuta.
  2. Changanya kwenye mashine (cake mixer) unga wa keki, maji, mafuta na mayai upige kwa mwendo mdogo kwa muda wa sekunde 30, halafu ongeza mwendo wa mpigo wa mashine kwa muda wa dakika mbili.
  3. Mimina kwenye tray usijaze sana katika vikombe vya tray kisha tia ndani ya oven kwa muda wa dakika 17 mpaka 22
  4. Toa ndani ya oven na uziacha zipoe
  5. Paka  malai (whipped cream) na unyunyize marembo

 

 

Share