Fatwaair bil-Jibnah -Vitobosho Vya Jibini

Fatwaair bil-Jibnah -Vitobosho Vya Jibini

 

Vipimo

Manda za sambusa za tayari - *idadi unayotaka

Jibini (cheese) ya vipande - (kama ya KIRI)

(Ikiwa ni kiri kata kipande kimoja cha jibini katika vipande 5)

Lozi na pistachio zilizosagwa - 1 Kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kata kata jibini vipande vidogo
  2. Tia kipande kimoja cha jibini katika manda na  uifunike kwa kuizungusha manda hadi mwisho iwe katika umbo la mstatili (kama katika picha)
  3. Funga mwishoni kwa gundi ya unga kama unavyofunga sambusa.
  4. Kaanga katika mafuta kama unavyokaanga sambusa.
  5. Epua kwenye mafuta na tia katika shira kisha zitoe na zipange katika sahani.
  6. Saga lozi (na pistachio kama unazo) kama unga kisha nyunyizia juu yake.

Shira

Sukari - 1 Kikombe

Maji - 3/4 Kikombe

Zaafarani rowanisha - 1 kijiko cha chai

Ipikie shira pamoja na zaafarani hadi iwe tayari, isiwe nzito  

*KIDOKEZO:

Wingi wa Fatwaair unategemea manda za sambusa na kiasi unachotaka mwenyewe, hivyo kila manda moja ya sambusa utie kipande kimoja cha jibini.

 

 

Share