'Aqiyqah: Inafaa Kuwafanyia Watoto Wanapokuwa Wakubwa – Tofauti ‘Aqiyqah Ya Mtoto Wa Kiume Na Wa Kike

 

SWALI:

Assalaam `alaykum,mimi nina mtoto wa kike ana umri wa mwka mmoja na miezi tisa,sijawahi kumfanyia hakika,lakini ndio nataka kumfanyia sasa,je natakiw niandae nini na nifanye nini?Pia kuna tofauti ya hakika kati hakika ya mtoto wa kike na wa kiume?

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Kwa mwenye uwezo, ni vizuri kuwafanyia ‘Aqiyqah  watoto wanapofika umri mkubwa wowote, wakati wowote katika uhai wao ikiwa hawakufanyiwa walipokuwa wadogo.

Mtoto wa kiume ni mbuzi au kondoo wawili, na mtoto wa kike ni mbuzi au kondoo mmoja.

Tafadhali ingia katika viungo vifutavyo utapata jibu la swali lako.

Utaratibu Wa 'Aqiyqah Katika Sunnah

Kufanya Aqiyqa Ni Lazima Au Sunnah?

Na Allaah Anajua zaidi

Share