Rudi Tena Ukaswali, Kwani Hukuswali

 

Rudi Tena Ukaswali, Kwani Hukuswali

 

Alhidaaya.com

  

 

BismiLLaahir-Rahmaanir-Rahiym

 

Sehemu Ya Kwanza

 

Katika usiku wa giza, Abu Lu’lu’ Al-Majuusi (kipenzi cha Mashia) alijificha katika vivuli akijiandaa kwa ajili ya Swalaah ya Alfajiri, wakati ambapo ataendesha mipango yake ya kishetani kumuua Amiyr wa waumini – ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu).

 

‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikuwa (na kawaida) ya kuongoza Swalah ya Alfajiri huku akisoma surah ndefu, akiwapa wafuasi wa jamii, muda wa kuhudhuria mkusanyiko (wa Swalaah). Katika siku hii, wakati (‘Umar) akisoma (Qur-aan), Abuu Lu’Lu’ akachukua hatua kutoka kwenye nguzo inayofifia, hali ya kuwa ana kisu cha sumu katika mkono wa vazi lake. Akaruka mbele ya ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na akamkata tumbo wazi kwa (kile) kisu. Baada ya hapo, akajaribu kuukimbia mkusanyiko. Akiwa ana chana chana mbele na nyuma, akiwauwa watu wengi zaidi ambao walikuwepo katika njia yake. Swahaba mmoja akamtupia nguo juu yake na alipo tahayari kwamba keshakamatwa Abu Lu’lu’ akajiua. 

 

‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akaikamilisha Swalaah ya Alfajiri ambayo aliianza ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu). ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikamilisha Swalaah yake hali ya kuwa ni miongoni mwa watu (maamuma) katika Jama’ah na akafariki dunia baadaye katika kitanda chake, (Radhwiya Allaahu ‘anhu).

 

Umuhimu wa Swalaah katika Uislam hauwezi kudharauliwa. Ni nguzo ya kwanza ya Uislamu iliyotajwa na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya tamko la Imani (shahada), ambayo kutokana nayo mtu huwa Muislamu.

 

Swalaah imefaradhishwa kwa Manabii na watu wote. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Alitangaza hadhi yake ya kuwa ni faradhi katia tukio Tukufu. Kwa mfano, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Alipozungumza na Muwsaa (‘Alayhis- salaam), Amesema:

 

وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ ﴿١٣﴾ إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي 

 

Nami nimekuchagua; basi sikiliza kwa makini yanayofunuliwa Wahy (kwako).  Hakika mimi ni Allaah hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi; basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa ajili ya kunidhukuru. [Twaahaa: 13-14]

 

Hivyo hivyo, Swalaah imefaradhishwa kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipopelekwa mbinguni. Zaidi, wakati Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anawasifu waumini kama katika Suwrah Al-Muuminuwn, moja katika sifa ambazo Anazitaja kuhusiana nao ni kule kushikana kwao na Swalaah:

 

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١﴾ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿٢﴾

 

Kwa yakini wamefaulu Waumini. Ambao katika Swalaah zao huwa wananyenyekea. [Al-Muuminuwn: 1-2]

 

Umuhimu wa Swalaah unaendelea kuonyeshwa katika kauli nyingi za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa mfano, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:

 

“Jambo la kwanza ambalo mja atahukumiwa katika Siku ya Hisabu ni Swalaah. Kama ikiwa ni nzuri basi amali zake zilizobakia zitakuwa nzuri. Na ikiwa ni mbaya, basi amali zake zilizobakia zitakuwa mbaya.” [At-Twabaraaniy].

 

Kwa kweli, ikiwa Swalaah imeswaliwa vizuri ikiambatana na ukumbusho wa kweli wa kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), na kumgeukia Yeye kutaka msamaha, itakuwa na athari kubwa juu ya mtu kwa kipindi kirefu. Mtu anapokamilisha Swalaah yake, moyo wake utajaa ukumbusho wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Atakuwa ana hofu na pia vilevile matarajio juu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Baada ya tukio hilo, hatotaka tena kuondoka kutoka katika sehemu hiyo ya fakhari kuelekea kwa ile ambayo ndani yake atamuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) anaitaja hali hii ya Swalaah katika Qur-aan:  

  ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ

 

Hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. [Al-‘Ankabwut: 45].

 

Lakini katika wale ambao wanaoswali, utakuta kuna vitendo vya kivivu ambavyo vinahitaji kumulikwa. Kwa mfano:

 

·         Wengine hawazingatii kile ambacho wanakisema.

·         Wengine wanafanya haraka katika Swalah zao

·         Wengine wanaachilia nadhari yao ya macho izurure wakati wa Swalah

·         Wengine mara kwa mara husahau nambari ya rakaa zilizotimizwa.

·         Dunia inakumbatia mioyo ya baadhi ya watu wakati wa Swalah na inafunika akili zao.

·         Na watu wengine katika Jamaa’ah wanaanza kusujudu kabla hata ya Imaam kusema “Allaahu Akbar”

 

Linganisha hii (hali yetu katika Swalaah) na Swalaah za watu ambao walikuja kabla yetu. Watu walikuwa wanafikiria ya kwamba Ar-Rabiy’ bin Khaytham alikuwa ni kipofu kwa sababu ya kuinamisha macho yake mara kwa mara. Alikuwa akiishi nyumbani kwa Abdullaah bin Mas’uud (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwa miaka ishirini na mtumwa wake wa kike akimuona alikuwa akisema: “Rafiki yako kipofu anakuja” na Abdullaah alikuwa akimcheka kwa kauli yake.

 

Ndani ya Al-Bukhaariy na Muslim, Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anatueleza ya kwamba, kuna mtu aliingia msikitini, ambao Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amekaa. Akaswali rakaa mbili na kisha akaja kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akatoa salamu. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaijibu salamu yake na halafu akasema, “Rudi tena ukaswali kwani hukuswali.” Hivyo, yule mtu akarudi, akaswali (rakaa mbili) kama alivyofanya mara ya kwanza, akaja tena na kurudia kutoa salamu. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaijibu salamu na akasema “Rudi tena ukaswali kwani hukuswali.” Hivyo, yule mtu akarudi, akaswali (rakaa mbili) kama alivyofanya mara ya kwanza akaja tena na kurudia kutoa salamu. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alijibu salamu kwa mara nyingine tena na kwa mara nyingine tena akasema: “Rudi tena ukaswali kwani hukuswali”. Hadi kufikia mara hii ya tatu, mtu huyo alisema: “Naapa kwa Yule ambaye alikutuma wewe na ukweli, Ee Rasuli wa Allaah, sijui vyovyote isipokuwa hivi, Nifundishe.” Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

 

“Ikiwa unasimama kwa ajili ya Swalaah sema “Allaahu Akbar”. Halafu soma ambacho kitakujia kwa wepesi katika Qur-aan. Kisha rukuu mpaka utakapohisi kwamba umetulia katika rukuu yako. Kisha, simama mpaka uwe umesimama wima kisawa sawa. Kisha, sujudu mpaka uwe umetulia katika sujudu yako. Kisha keti mpaka uwe umetulia katika juluus yako. Kisha sujudu mpaka uwe umetulia katika sujudu yako. Na uwe unafanya hivi ndani ya Swalaah yako yote”.

  

(Kwahiyo turudi tukarudie Swalah zetu)

 

Kwanini tunakuja msikitini; nini sababu yetu ya kutekeleza Swalah? Tunafanya hivyo kwa kufuata amri ya Rabb wetu (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Kwanini hasa tupoteze baraka na thawabu kwa sababu ya moyo usiotulia na mkono unaowasha. Khushuu ni kiini cha Swalaah zetu. Khushuu ni matunda ya imani yetu. Lakini, hata baada ya kujua haya, watu hawafanyi juhudi kukamilisha Swalah zao na kwa hiyo huandikiwa sehemu ndogo tu. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema;

 

“Kwa hakika, mtu ataondoka (katika Swalaah yake) na ataandikiwa (thawabu) kumi za Swalaah yake; tisa, nane, saba, sita, tano, nne, tatu, nusu.” [Abu Daawuud na at-Tirmidhiy]

  

‘Uthmaan bin Abii Dahshah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Sijawahi kuswali Swalah ambayo baada yake nilikosa kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anisamehe kwa upungufu wangu katika Swalah ile.”

 

Mtu ambaye anaharakisha Swalah yake ni mwizi.  Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema katika Hadiyth sahihi, “Mwizi muovu kuliko wote ni yule ambaye anaiba katika Swalaah yake”. Swahaaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wakauliza: “Ee Rasuli wa Allaah, anaibaje katika Swalah yake?” Naye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Hakamilishi rukuu na sujudu zake”

  

Kwa sababu ya kasi ya jinsi ya watu wanavyoswali, wanaonekana kama ndege, wanaodonoa juu na chini. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza mtu kudonoa (katika Swalah) kama kunguru.

  

‘Umar (Radhwiya Allahu ‘anhu) wakati mmoja alisimama katika Minbari akiuhutubia umati wa watu kwa sauti ya nguvu akisema, “Mtu anaweza akakulia mpaka utu uzima katika Uislamu na asiweze kamwe kukamilisha kwa ajili ya Allaah hata Swalah moja!” (Watu) wakasema, “Vipi hali hii?” (‘Umar) (Radhwiya Allahu ‘anhu) akasema: “Hakamilishi khushuu yake, hata unyenyekevu wake, hata nadhari yake juu ya Allaah ‘Azza wa Jalla.”

 

Wakati mmoja, Ma’aruuf Al-Karkhiy (Rahimahu Allaahu) aliposimama miongoni mwa wanafunzi wake, mmoja wao akamwambia mwenziwe, “Tafadhali swalisha Swalaah ya ‘Ishaa”. Mwanafunzi wa kwanza akakubali lakini akasema “Nitaswalisha Swalaah ya ‘Ishaa kwa sharti ya kwamba wewe utaswalisha Swalaah ya Alfajiri sio mie” Ma’aruuf Al-Karkhiy alishtushwa na kauli aliyoisema na akasema, “Naapa kwa Allaah, ikiwa unafikiria ya kwamba utakuwa hai wakati wa Alfajiri, basi naapa kwa Allaah, hujakamilisha Swalah yako”.

 

Sehemu Ya Pili

 

Jinsi ya kuwa na Khushuu ndani ya Swalah

Al-Qaasim bin Muhammad (Rahimahu Allaahu) alisema: “Nilikwenda nje siku moja, na kila nilipotoka ni lazima nipite kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allahu ‘anhaa) na kumsalimia. Siku hiyo nilitoka na nilipomkuta mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allahu ‘anha) akiswali Swalah ya Dhwuhaa, akisoma tena na tena Aayah ya Allaah:

 

قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ 

 

Watasema: Hakika sisi tulikuwa kabla kwenye ahli zetu wenye kuogopa. Basi Allaah Akatufadhilisha, na Akatuokoa na adhabu ya moto unaobabua. [Atw-Twuur: 26-27]

 

Alikuwa analia na akimwomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na huku akirudia Aayah hiyo. Nilisimama pale mpaka nikachoka, hali ya kuwa yeye amebaki kama nilivyomkuta. Nilipoona haya nilijiambia, “Hebu niende sokoni, nifanye ninachotakiwa kufanya, halafu nije tena”. Kwa hiyo, baada ya kumaliza kufanya nilichotaka kufanya sokoni, nilirudi kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allahu ‘anhaa). Alikuwa kama nilivyomuacha, akirudia Ayaah, akimuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na akilia”.

 

Vipi tuwe na khushuu katika Swalaah?

 

Katika Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tunafundishwa yafuatayo:

 

1.     Njoo mapema kwa ajili ya Swalaah na jitayarishe kuwa na khushuu.

Fuatiliza adhana pamoja na Mu’adhin na baada ya adhana, sema dua iliyoamriwa. Omba dua baina ya Adhaana na Iqaamah. Tia wudhuu vizuri, hali ukisukutuwa mdomo wako, na vaa nguo zako nzuri kabisa.

 

2.     Nuia kupata dhawabu zote za Swalaah yako.

Abu Bakr bin ‘Iyaash alisema, “Nilimuona Habiyb bin Thaabit katika sujudu. Ukimuona utadhania kwamba kashakufa (kwa urefu wa sujudu zake).”

 

3.     Zingatia Aayah na adhkaar ambayo inasomwa ndani ya Swalaah.

Fikiria kuhusu maana za Aayah ambazo unazisoma. Je haivunji moyo ya kwamba mtu anaweza kuswali miaka kumi baada ya kumi, siku baada ya siku na pia bado hajui anasema nini? Qur-aan iliteremshwa ili itafakariwe! Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Kateremsha (katika Qur-aan Ayaah inayosema):

 

 كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ

 

Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chenye Baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayaat zake, na ili wapate kukumbuka wenye akili. [Swaad: 29].

  

4.     Swali Jama’ah. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anaamrisha:

 

 وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ

 

Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika utiifu). [Al-Baqarah: 43].

 

5.     Usikose kamwe kuswali Swalah zako za nawaafil (Sunnah zilizotiliwa mkazo), hasa zile ambazo Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali siku zote, kama vile Witri na Sunnah ya Alfajiri.

 

6.     Usiharakishe Swalah yako.

Chukua muda wako na usikubali kuifanya Swalah yako kuwa kitendo kilichokuwa hakina thamani katika siku yako. Ibn Wahb (Rahimahu Allaahu) alisema: “Nilimuona Ath-Thawriy (Rahimahu Allaahu) kwenye Kaa’bah.  Baada ya Swaalah ya Magharibi, alinyanyuka kuswali na kisha akasujudu. Hakunyanyuka katika ile sujudu mpaka adhana ya ‘Ishaa ilipoadhiniwa.”

  

7.   Jua ya kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anajibu Swalah yako. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:

 

“Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Aliyetukuka alisema: “Nimeigawa Swalah kati Yangu na mja Wangu  katika nusu mbili, na mja Wangu atapata alichokiomba” [Kutoka katika Suwrah Al- Faatihah ] Wakati mja anaposema, “AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)) Rabb wa walimwengu, (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema, “Mja Wangu Amenihimidi” . Wakati mja anaposema “Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu” Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema, “Mja wangu Amenisifu.” Wakati mja anaposema, “Mfalme wa siku ya malipo”, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema mja Wangu Amenitukuza”.  Wakati mja anaposema, “Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) anasema, Hii ni kati Yangu Mimi na mja Wangu, na mja Wangu atapata alichokiomba”. Wakati mja anaposema “Tuongoze njia iliyonyooka, njia ya uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa, wala walioptea,” Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema, “Hivi vyote ni kwa ajili ya mja Wangu, na mja Wangu atapata alichokiomba” [Muslim]

  

8.     Swali pamoja na kizuizi (weka sutrah) mbele yako na swali karibu yake.

 

Kitu chengine ambacho kitakusaidia kuwa na khushuu’ [utulivu] ni kushughulika (au kuwa makini) katika suala la kuwa na kizuizi (sutrah) na kuswali karibu yake. Kuwa na sutrah kutazuia uoni wako, kutakulinda juu ya Shaytwaan, na kutazuia watu kupita mbele yako, kitu ambacho husababisha wasiwasi na hupunguza thawabu za Swalah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: 

 

“Ikiwa mmoja wenu ataswali basi na aswali akielekea kwenye sutrah, na awe karibu nayo” [Abuu Daawuud].

  

9.     Tafuta [ulinzi] kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kutokana na Shaytwaan.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitufundisha vipi tupambane na wasi wasi wa Shaytwaan. Abul- ‘Aas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kasimulia ya kwamba alisema, “Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Shaytwaan ananisumbua wakati ninaswali, na hupata wasiwasi katika kisomo changu.” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Huyo ni Shaytwaan ambaye jina lake ni Khanzab. Ikiwa utahisi kwamba yupo, jilinde kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kutokana naye, na tema mate (makavu) katika upande wako wa kushoto mara tatu”. Abu’l –‘Aas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema: “nilifanya hivyo na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akaniondoshea.” [Muslim].

 

10.   Swali kama kwamba umeambiwa kuwa baada kumaliza Swalah utarudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Abu Bakr Al-Muzaniy (Rahimahu Allaah) alisema, “Kama unataka Swalah yako ikufae, basi sema: “Nitakufa baada tu ya Swalah hii!”  

 

Share