Swalaah Za Sunnah Muakkadah (Zilizosisitizwa) Na Ghayr Muakkadah (Zisizosisitizwa)
Swalaah Za Sunnah Muakkadah (Zilizosisitizwa) Na Ghayr Muakkadah (Zisizosisitizwa)
Fadhila za Swalaah za Sunnah kwa ujumla ni nyingi, mojawapo ni Hadiyth:
عَنْ عبادةَ بنِ الصَّامِتِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ النَبيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْجُدُ للهِ سَجْدَةً إِلاَّ كَتَبَ اللهُ لَهُ بِهَا حَسَنَةً . وَمَحَا عَنْهُ بِهَا سَيِّئَةً ، وَرَفَعَ لَهُ بِهَا دَرَجَةً ، فَاسْتَكْثِرُوا مِنَ السُّجُودِ))
Imepokelewa kutoka ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) ((Mja yeyote atakayesujudu sijda moja ataandikiwa hasanah (jema) mmoja, na atafutiwa baya moja, na atapandishwa daraja yake, kwa hiyo zidisheni kusujudu)) [Ibn Maajah]
Fadhila za kuswali Swalaah za Sunnah Muakkadah (zilizosisitzwa) kabla ya Swalaah au baada ya Swalaah, jumla yake ni rakaa 12 kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
(( مَا مِنْ عبْدٍ مُسْلِم يُصَلِّي للَّهِ تَعَالى كُلَّ يَوْمٍ ثِنْتَيْ عشْرةَ رَكْعَةً تَطوعاً غَيْرَ الفرِيضَةِ ، إِلاَّ بَنَى اللَّه لهُ بَيْتاً في الجَنَّةِ ، أَوْ : إِلاَّ بُنِي لَهُ بيتٌ في الجنَّةِ )) رواه مسلم
((Hatoswali mja Rakaa 12 zisizo za fardhi kwa siku, ila atajengewa [na Allaah] nyumba Jannah)) [Muslim]
Alfajiri:
1-Muakkadah: Rakaa 2 kabla ya Swalaah
Suwrah za kusomwa: Suwratul-Kaafiruwn na Suwratul-ikhlaasw
Au Al-Baqarah 2:136 na Aal-‘Imraan 3:64 au Aal-‘Imraan 3:52.
Fadhila zake:
(( ركْعتا الفجْرِ خيْرٌ مِنَ الدُّنيا ومَا فِيها )) رواه مسلم
((Rakaa mbili (za Sunnah) kabla ya Alfajiri ni kheri kuliko duniya na yaliyomo ndani yake) [Muslim]
Bonyeza kiungo upate faida zaidi:
Swalah Ya Sunnah Ya Alfajiri Inaswaliwa Vipi Na Wakati Gani? Na Surah Zipi Zisomwe?
Adhuhuri:
2-Muakkadah: Rakaa 4 kabla ya Swalaah na rakaa 2 baada ya Swalaah
Ghayr Muakkadah: Rakaa 2 baada ya Swalaah
Alasiri:
Hakuna Swalaah za Sunnah.
Magharibi:
3-Muakkadah: Rakaa 2 baada ya Swalaah unasoma Suwratul-Kaafiruwn na Suwratul-Ikhlaasw.
Bonyeza kiungo upate faida zaidi:
Surah Gani Zisomwe Swalah Ya Alfajiri Na Magharibi? Inafaa Kusoma Surah Kubwa Na Ndogo?
Ghayr Muakkadah: Rakaa 2 baada ya Swalaah.
‘Ishaa:
4-Muakkadah: Rakaa 2 baada ya Swalaah
Ghayr Muakkadah: Rakaa 2 kabla ya Swalaah
Swalaah Nyenginezo Zilizosisitzwa:
5-Swalaah ya Tahajjud:
Ni Swalaah bora kabisa baada ya Swalaah za fardhi kwa dalili:
(( أَفْضَلُ الصَّلاةِ بَعْدَ الْفَرِيضَةِ صَلاةُ اللَّيْلِ)) رواه مسلم
((Swalah iliyo bora kabisa baada ya Fardh ni Swalah ya usiku)) [Muslim]
Bonyeza viungo upate faida zake:
Wakati Wa Swalah Ya Tahajjud Na Vipi Kuswali
Nini Fadhila Za Swalah Ya Tahajjud?
6-Swalaah Ya Dhwuhaa:
Ni Swalaah inayoanza kuswaliwa baada ya kuchomoza jua vizuri mpaka karibu na adhuhuri kabla ya kuingia kwake.
Idadi ya Rakaa zake kuanzia 2 hadi 8
Fadhila zake:
عـَن أبي ذَرٍّ رضي الله ُ عنه ، عن النـَبي ِّ صلـَّى الله عليه وسلم قال: ((يـُصـْبـِحُ عـَلى كـُلِّ سـُلامى مـِنْ أحـَدِكـُمْ صـَدَقةُ: فـَكُل تـَسْبـِيحـَةِ صـَدَقةٌ ،وَ كُل تـَحمِيدة صـَدَقةٌ ، وكُلُ تـَهْـليْلةٌ صـَدَقـَةٌ، وكُلُّ تـَكْبِيْرةِ صـَدقةٌ ، وأمرٌ بالمـَعرُوف صـَدقةٌ ، ونـَهىٌ عـَنِ المـُنْكرِ صـَدقةٌ ويـُجْزئ مـِنْ ذلكَ رَكـْعتـَانِ يـَركَعُهُما مـنَ الضـُّحى)) رواه مسلم
Kutoka kwa Abu Dharr (Radhiya Allahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Kila kiungo katika mwili wenu hupambaukiwa kikihitaji kutolewa sadaka, kwa hiyo kila tasbiyh (kusema ‘SubhaanaAllah’) ni sadaka na kila tahmiyd (kusema ‘AlhamduliLlaah’) ni sadaka na kila tahliyl (kusema ‘La Ilaaha Illa Allah’) ni sadaka na kila takbiyr (kusema ‘Allahu Akbar’) ni sadaka na kuamrisha mema ni sadaka na kukataza maovu ni sadaka na itamtosheleza (Mtu) kwa Rakaa mbili za Dhuhaa)) [Muslim]
Na pia bonyeza kiungo upate faida zaidi:
Swalah Ya Dhwuhaa - Rakaa Zake, Fadhila Zake na Wakati Wake
7- Swalah Ya Witr:
Ni Swalaah inayoswaliwa kuanza baada ya Swalaah ya ‘Ishaa mpaka kabla ya Swalaah ya Alfajiri.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ : أَوْصَانِي خَلِيلِي صلى الله عليه وسلم بِثَلاثٍ : صِيَامِ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ، وَرَكْعَتَيْ الضُّحَى، وَأَنْ أُوتِرَ قَبْلَ أَنْ أَنَامَ .
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba “Ameniusia rafiki yangu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mambo matatu; kufunga swawm siku tatu katika kila mwezi, rakaa mbili za dhwuhaa, na niswali Witr kabla ya kulala” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Bonyeza viungo kwa faida ziada:
Swalah Ya Witr Inaswaliwa Vipi Na Vipi Kutia Nia?
Surah Gani Kusoma Katika Swalah Ya Tahajjud Na Witr?