Tawbah Ya Shirk Inakubaliwa? Na Vipi Kuomba?

 

Tawbah Ya Shirk Inakubaliwa? Na Vipi Kuomba?

 

 

 

SWALI LA KWANZA

 

Amesema Allaah s.w atakayejua kwamba mimi nina uwezao wa kusemehe dhambi basi nitamsamehe wala sitojali maadau hakunishirikisha na chochote.

Suali mtu anajua kwa Allaah anao ouezo kusamehe madhambi, na yeye kafanya madhambi na katika hizo dhmabi zimo nyengine za shirki. Vipi toba ya hizi dhambi pia kwasababu pia m/mungu anasema katika suratun-nissaa aya 48 na aya

116 yeye hasamehe dhambi ya kushirikisha isipokua anasemehe dhambi nyingine kwa amfakaye

Na pia tunaona pia katika suratul-furqan aya 68-70 Na suratul-zumar aya 53 naomba tuwekewe waza kwasababu tunasoma qur-ani-lakini saa nyingine aye zinatuchanga akili. Na tumesoma katika al-hidaya. Natak kutubia... Lakini!!!

 

SWALI LA PILI

 

 Je toba ya shirki hukubaliwa? na inakuwaje?

 

 

 

JIBU:

 

 

 AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Tawbah ya aina yoyote inakubaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hata shirki maadam mtu yuko hai, kwa dalili ya kauli Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu Manaswara waliomshirikisha Naye na Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam):  

 

لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.”

 

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Na hali hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.  [Al-Maaidah: 72-73]

 

Lakini baada ya Aayah hizo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaahidi kwa Rahma Zake kuwaghufuria pindi watakapotubu na kuacha kumshirikisha. Anasema   (Subhaanahu wa Ta'aalaa):   

 

أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧٤﴾

Je, hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfirah? Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.   [Al-Maaidah:  74]

 

 

Na maswahaba walipomuuliza  Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kuhusu madhambi yao ya nyuma ya kumshiriki Allaah kwa kuabudu masanamu, kuua, kulewa n.k Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)    Akateremesha kauli Yake:

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾

Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: “Msikate tamaa na rahmah ya Allaah; hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote; hakika Yeye Ndiye Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.” [Az-Zumar: 53]

 

 

Hakika Aayah nyingi zimekuja kutuonyesha Rahma za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) jinsi zilivyo pana ya kutughufuria madhambi yetu, na hii ni neema kwetu sisi Waislamu kuweko katika dini hii tukufu. Lakini neema hii haitumii kila mtu ila wale ambao wanaojirudi kutubia kwa Rabb wao kabla ya mauti kuwafika.

 

Na pia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth nyingi kupokelewa tawbah zetu, mfano mmojawapo ni Hadiyth ifuatayo inatuonyesha jinsi gani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anavyofurahi mja Wake Anapotubia Kwake:

 

عن أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الَلَّهُ أَشَدُّ فَرَحًا بِتَوْبَةِ عَبْدِهِ حِينَ يَتُوبُ إِلَيْهِ مِنْ أَحَدِكُمْ كَانَ عَلَى رَاحِلَتِهِ بِأَرْضِ فَلاَةٍ فَانْفَلَتَتْ مِنْهُ وَعَلَيْهَا طَعَامُهُ وَشَرَابُهُ فَأَيِسَ مِنْهَا فَأَتَى شَجَرَةً فَاضْطَجَعَ فِي ظِلِّهَا قَدْ أَيِسَ مِنْ رَاحِلَتِهِ فَبَيْنَا هُوَ كَذَلِكَ إِذَا هُوَ بِهَا قَائِمَةً عِنْدَهُ فَأَخَذَ بِخِطَامِهَا ثُمَّ قَالَ مِنْ شِدَّةِ الْفَرَحِ: "اللَّهُمَّ أَنْتَ عَبْدِي وَأَنَا رَبُّكَ" ‏ أَخْطَأَ مِنْ شِدَّةِ الْفَرَحِ)) مسلم

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Allaah Hufurahikiwa mno na tawbah ya mja Wake wakati anapotubia Kwake kuliko furaha ya mmoja wenu aliyekuwa amempanda mnyama wake kwenye jangwa (la joto kali hakuna mtu), kisha mnyama huyo aliyebeba chakula chake na maji yake akampotea, na akakata tamaa kabisa ya kumpata tena. Akaenda kwenye mti, akalala chali ya kivuli chake huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpata tena mnyama wake. Akiwa katika hali hiyo (ya kutojua nini la kufanya), mara anashtuka kumwona huyo amesimama mbele yake, akaikamata hatamu yake, na kwa ile furaha akasema:  "Ee Allaah, Wewe ni mja wangu na mimi ni Rabb wako.” Alikosea (kumshukuru Rabb wake) kwa wingi wa furaha aliyokuwa nayo.” [Muslim]

 

 

Fadhila na fadhila za kuomba tawbah na maelezo mengi yanayohusu tawbah yote utayapata katika viungo vifuatavyo:  

 

 

Na masharti ya tawbah ni yafuatayo:

 

1.Ayaache maovu aliyokuwa anayafanya.

 

2. Ayajutie makosa aliyoyafanya.

 

3. Aazimie kutourejea tena uovu huo katika maisha yake.

 

Na endapo kosa hilo litahusiana na haki ya mtu hapo litaongezeka sharti la nne nalo:

 

4. Ni kumuomba msamaha uliyemkosea kwa ulichomkosea ikiwa ni kuhusu haki za binaadamu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

  

 

 

Share