Kwa Nini Mashekhe Wengine Wanakubali Arubaini Na Wanashiriki Katika Kula Chakula Chake?
SW
Asalaam alaykum
Kwanza kabisa natanguliza shukran zangu za dhati nimejua mengi
Nimesoma katika hii site yenu maswali na majibu na kuwa hakuna kitu kama arobaini katika uislam sasa mbona tunapofiwa baaada ya siku arobaini tunajumuika pamoja na mashekhe wakubwa kabisa tunakula mpunga na kusoma Qur-an na wao hawakemei swala
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Arubaini na kula ndani yake. Pia tunakushukuru kufahamu kuwa umejifunza mengi kutoka ALHIDAAYA, InshaAllaah Allaah Akuzidishie wewe elimu na sisi Atutaqabalie amali hii.
Kadhalika tunakujulisha wewe na wengine kuwa tunawajibu wengi maswali
Tukirejea kwenye swali lako, tunataka kuweka wazi kuwa Uislamu hauendi kwa matamanio ya watu, wawe ni wakubwa au wadogo, Mashaykh au maamuma. Uislamu unakwenda kwa misingi yake ambayo ni thabiti kabisa.
Mtu akitoka katika misingi hii hata akiwa nani atakuwa amefanya makosa. Hili jambo la chakula liliwekwa kwa maslahi ya watu fulani ambao ni Mashaykh hao unaozungumzia. Kwa ukosefu wa mshahara au ajira watu wamekuwa wakitafuta njia tofauti za kuweza kujikimu kimaisha. Ama Sunnah hasa inavyotakiwa ni yale maneno aliyotuambia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwataka majirani na wanaokwenda kwa wafiwa siku tatu za msiba ni kufanya kama alivyosema wakati wa kifo cha Swahaba Ja’afar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kutokana na maimulizi ya ‘Abdullaah bin Ja’afar: Ulipofika msiba wa Ja’afar wakati alipouawa vitani,
“Wafanyieni chakula watu wa Ja’afar kwani wamepata lenye kuwashughulisha”. (Wamepokea Maimaam watano isipokuwa An-Nasaaiy pekee)
Hivyo, inatakiwa Waislamu wawe ni wenye kuwafanyia wafiwa chakula na kuwapelekea kuliko wafiwa kuwatengenezea wengine wawe ni wenye kuja kula hapo na kuzidi kuwatia dhiki.
Zaidi soma ndani hapa upate faida nyingi:
Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti
Kawaida mwenye kukemea ni yule ambaye atajua kuwa
Kwa hiyo jambo hilo la kisomo cha Arubaini na kufanyiwa chakula halimo katika sheria na halipasi kutendwa kwani ni bid’ah iliyokemewa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akatuhidhirishia madhara yake kuwa ni upotovu na adhabu zake ni kujitayarishia makazi motoni.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha

Assalam alaikum
Assalam alaikum warahmatullah, nataka kudokeza kuhusu malalamishi ya watu ambao wasema hawapokei majibu ya maswali yao. Ningependa kuwajulisha ya kwamba wajaribu kuangalia "spam folder" ina uwezekano kuwa jawabu limo humo. shukran wa jazakumullahu khair.