Wanawake Lazima Waende Kuswali Ijumaa Msikitini?

 

Wanawake Lazima Waende Kuswali Ijumaa Msikitini?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI

 

Assalam Aalekum warahmatullahwabarakatu. Suali langu nataka kujuwa. Je mwanamke kuwenda msikitini kila swala ya ijumaa inafaa. Jazakallah khera.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Hakuna ulazima wa wanawake kwenda kwa ajili ya Swaalah ya Ijumaa lakini akienda hakatazwi na sheria. Bila shaka kuna faida nyingi kwa wanawake kwenda kwa Swaalah hiyo kwani wanapata mawaidha (khutbah) ambayo yatawasaidia katika maisha yao.

 

 

Tufahamu kuwa Swalah ya Ijumaa Msikitini ni lazima kwa wanaume wala sio wanawake.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share