Zipi Ishara Za Kurogwa Au Kufanyiwa Uchawi?

SWALI:

 

 

Nashukuru sana kwa majibu mazuri mnayoupa kuhusu masuala yetu mbalimbali. Vipi nitaweza kujua kwamba nimerogwa au nimepatwa na uchawi, naomba mnieleze ishara mbali mbali za kumjua mtu aliyeathirika na uchawi.

 

Ombi, kama itakuwa vigumu kurushwa kwenye mtandao kwa sasa naomba nijibuni kupiti kwenye e-mail yangu.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ishara za kurogwa.

Hakika zipo ishara nyingi na kila mmoja anapata ishara zake mwenyewe. Ishara moja ni Kufikiria kuwa unafanya kitu ilhali hufanyi na mengineyo. Na njia rahisi ni kusomewa Surah na Aayah za Ruqyah, ikiwa mtu huyo kafanyiwa uchawi basi atatoa ishara ambazo mwenye kumsomea atazifahamu na hivyo kumtibu. Mara nyingi inakuwa huyo aliyerogwa anazungumza kwa sauti isiyo ya kawaida na kuelekeza vitu vilivyotumika na mahali vilipowekwa.

 

Lililo muhimu zaidi ni kila Muislamu awe atasoma sehemu za Qur-aan na nyiradi ambazo zitamuhifadhi yeye na uchawi na kulogwa. Nazo utapata katika maelezo yaliyomo katika viungo vifuatavyo:

 

 

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Naingiliwa Na Majini

 

Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi

 

Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa

 

 

Pia ingia katika kiungo hiki, upate Du’aa na Adhkaar mbalimbali za kinga na kulogwa:

 

 

Hiswnul Muslim

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share