Dhokra

Dhokra 

Vipimo

Unga wa mahindi au wa mchele -  ¼ magi

Unga wa dengu - 2 magi

Mtindi (yogurt) - 1 kopo

Manjano - 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu (thomu/galic) - 2 vijiko vya supu

Pilipili ya chupa ya Sambal - 2 vijiko vya supu

Chumvi - 1 kijiko cha supu

Sukari - 6 vijiko vya supu

Pilipili mbichi - upendavyo

Kotmiri - kiasi

Baking powder - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 1

Rai - 2 kijiko cha supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya yogurt, unga wa mahindi na unga wa dengu vizuri
  2. Kata vitunguu, kotmiri, na pilipili mbichi vipande vidogo.
  3. Kisha uchanganye na vipimo vilivobaki isipokuwa baking powder
  4. Paka kisinia kidogo mafuta tia mchanganyiko kwenye bakuli kiasi
  5. Tia baking powder changanya kisha tia kwenye kisinia uliyoitayarisha.
  6. Chukuwa sufuria kubwa kidogo tia maji kikombe kimoja kisha weka bakuli jengine ndani ya sufuria ya maji.
  7. Tia kisinia cha mchanganyiko juu ya kibakuli funika vizuri upike kwa mvuke (steam) muda wa saa hivi.
  8. Weka mafuta Kijiko kimoja cha chai kwenye kisufuria kidogo ukaange rai  kotmiri na pilipili mbichi.
  9. Ikishaiva dhokra utanyunyiza kwa juu pamoja na masala ya unga
  10. Kidokezo
  11. Unaweza kuweka kwenye friji ukafanya kidogo kidogo   

 

Share