Umuhimu Wa Kukimbilia Kutekeleza Nguzo Ya Hajj

Umuhimu Wa Kukimbilia Kutekeleza Nguzo Ya Hajj

 

www.alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

   

إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾ 

96. Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu.

 

فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾ 

97. Ndani yake kuna Aayaat (ishara, dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu. [Aal-‘Imraan 96-97]

 

Na kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ((بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ: شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ )) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdullaah bin 'Umar bin  Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema:  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  akisema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake,  kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Tunatambua kutokana na kauli hizo kuwa kutekeleza Hajj ni fardhi kwa kila mwenye uwezo. Hivyo asiyeharakisha kutekeleza fardh hii atakuwa amemuasi Rabb wake na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na itakuwa ni dhambi kubwa kwake ikiwa kuacha huko ni kwa makusudi na hali alikuwa ana uwezo wa mali, siha n.k., sababu atakuwa amekanusha amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

Na haiwi kwa Muumini mwanamme na wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana hiari katika jambo lao.  Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana.  [Al-Ahzaab: 36].

 

 

Sababu Za Umuhimu Wa Muislam Kuharakisha Kutekeleza Hajj

 

1-Asiyetekeleza Hajj Huenda Akafikwa Na Masaibu Yamzuie Kutekeleza Nguzo Hii Ya Kiislamu

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuhimiza na kutuonya hayo:  

((مَنْ أَرَادَ الْحَجَّ فَلْيَتَعَجَّلْ)). رواه الإمام أحمد وأبو داود وابن ماجه. وفي رواية أحمد وابن ماجه: (( فَإِنَّهُ قَدْ يَمْرَضُ الْمَرِيضُ ، وَتَعْرِضُ الْحَاجَةُ)) حسنه الألباني في صحيح ابن ماجه  

((Mwenye kutaka kufanya Hijjah basi aharakize)). [Imaam Ahmad, Abuu Daawuwd na Ibn Maajah – Swahiyh Abiy Daawuwd (1732), Swahiyh Ibn Maajah (2349), Swahiyh Al-Jaami’ (6003)]

 

Na katika riwaayah ya Ahmad na Ibn Maajah

 

((Kwani huenda akapata maradhi au akafikwa na haja)). [Kaipa daraja ya hasan Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh-Ibn Maajah (2349) na Swahiyh Al-Jaami’ (6004)]

 

Vile vile amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((تعجَّلوا إلى الحجِّ - يعني الفريضةَ - فإنَّ أحدَكم لا يدري ما يعرِضُ له)) أخرجه الإمام أحمد رحمه الله وحسَّنه الألباني في إرواء الغليل.

((Harakizeni Hajj, [yaani kutekeleza fardhi ya Hajj] ((kwani hajui mmoja wenu nini kitamsibu)). [Imaam Ahmad na kaipa daraja ya hasan Shaykh Al-Albaaniy katika Irwaaul-Ghaliyl (990), Swahiyh Al-Jaami’ (2957)]

 

 

2-Asiyetekeleza Hajj Azingatia Kwamba Ana Dhamana Ya Umri Mrefu

 

Waislamu wengi hawaifanyii hima ‘ibaada hii na aghalabu ya sababu ni:

 

a-Wengine huona kuwa ni bado vijana hivyo wanangojea wafikie umri mkubwa ndio watimize. Basi wajiulize: Je, Wana uhakika gani kuwa wataruzukiwa umri mrefu? Bali wana dhamana gani kama wataishi hata mwaka mmoja zaidi? Au mwezi mmoja zaidi? Au wiki moja zaidi? Au hata siku moja zaidi? Hawasomi kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqmaan: 34].

 

b-Wengine wameshughulika na anasa za dunia na kughafilika kuwa huenda wakaaga dunia na kukosa kutekeleza nguzo hii ya Uislamu. Tambua ndugu unayechelea kutekeleza Hajj kwamba nafsi inayojidhulumu hujuta wakati wa kutolewa roho na mtu hutamani arudi atende yale aliyoyakosa kutenda lakini haiwezekani tena kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

   

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾

Mpaka itakapomfikia mmoja wao mauti, atasema: “Rabb wangu! Nirejeshe (duniani).”

 

لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٠٠﴾

“Ili nikatende mema katika yale niliyoyaacha.” (Ataambiwa) “Laa hasha!” Hakika hilo ni neno alisemaye yeye tu.  Na nyuma yao kuna barzakh mpaka Siku watakayofufuliwa. [Al-Muuminuwn: 99-100].

 

 

3-Hajj Ni Katika ‘Amali Bora Kabisa

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهم عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ أَيُّ الْعَمَلِ أَفْضَلُ فَقَالَ: ((إِيمَانٌ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ)) قِيلَ ثُمَّ مَاذَا قَالَ: ((الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ)) قِيلَ ثُمَّ مَاذَا قَالَ: ((حَجٌّ مَبْرُورٌ))   متفق عليه

Aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ipi 'amali njema kabisa? Akasema: ((Kumuamini Allaah na Rasuli Wake)) Akaulizwa: "Kisha nini"? Akasema: ((Jihaad katika Njia ya Allaah)) Akaulizwa: "Kisha nini"? Aakasema: ((Hajj yenye kukubaliwa)). [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

4-Mwenye Kutekeleza Hajj Hufutiwa Madhambi Yote

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ:  سَمِعْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَنْ حَجَّ لِلَّهِ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ)) متفق عليه

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo vichafu atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

5-Jazaa Ya Kutekeleza Hajj Ni Kuingizwa Jannah

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ: ((العُمْرَةُ إِلَى العُمْرَةِ كَفَّارَةٌ لِمَا بَيْنَهُمَا، وَالحَجُّ المَبْرُورُ لَيْسَ لَهُ جَزَاءٌ إِلَّا الجَنَّةَ)) متفق عليه  

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (('Umrah hadi 'Umrah ni kafara (kufutiwa dhambi) baina yao, na Hajjul-Mabruwr [yenye kukubaliwa] haina jazaa isipokuwa ni Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate faida tele nyinginezo:

 

Fadhila Za ‘Umrah Na Hajj - Kutoka Kitabu: Alhidaaya Katika Manaasik Za Hajj Na 'Umrah

 

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Awajaalie Waislamu ambao bado hawakujaaliwa kuitekeleza fardhi hii, uwezo wa kutekeleza Hajj na Awaghufurie madhambi yao na Awathibitishe katika Manhaj ya Salaf mpaka mwisho wa uhai wao. Aamiyn.

 

 

Share