Hajj: Hatua Kwa Hatua

 

Hajj: Hatua Kwa Hatua

 

www.alhidaaya.com 
 

 

 

1 – 7 Dhul-Hijjah – Makkah au Madiynah

 

Kuzuru Msikiti wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuweko Makkah kufanya 'Umrah (kwa wanaofanya Hajjut-Tamattu'u) na kuendelea kuswali hapo Masjidul-Haraam.

 

 

 

Madiynah

 

Kuswali Masjidun-Nabawiy na wanaume kuzuru kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

  

 

Makkah

 

Kufanya Twawwaaf:  Kuzunguka Ka'bah mara 7
Kuswali Raka'ah mbili Maqaam Ibraahiym

 

 

 

Sa'yi  -  Swafaa  Na Marwah
Kuanza kilima cha Swafaa kwenda kilima cha Marwah mara saba.

 

Wakimaliza 'Umrah watabakia Makkah na kuswali katika Masjidul-Haraam kupata fadhila zake.

 

 

8 Dhul-Hijjah – Minaa

 

Asubuhi wanaondoka Makkah kuelekea Minaa.

 

 

9 Dhul-Hijjah – Siku ya 'Arafah

 

Wanaondoka kutoka Minaa asubuhi kuelekea 'Arafah na kubaki hadi jua litakapozama. 

 

Ni siku ya kutekeleza fardhi kubwa miongoni mwa taratibu za Hajj. Siku ya kuomba Du'aa sana. Na ndiyo siku iliyokamilika Dini yetu tukufu aliposimama Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika mlima wa 'Arafah na kutoa khutbah yake ya mwisho. Na ni siku ambayo wengi wetu wataachiwa huru na moto.

 

Hapa wataswali Swalaah ya Adhuhuri na Alasiri 'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Raka’ah mbili mbili). Watasikiliza khutbah (watakaojaaliwa kuweko karibu na Masjidun-Namirah).  Wasiokuwepo huko siku hiyo watafunga Swawm ya 'Arafah ambayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema inafuta madhambi ya mwaka uliopita na ujao.

 

Jua likizama, wataelekea Muzdalifah.

 

10 Dhul-Hijjah – Muzdalifah – Minaa - Makkah

 

Watafika Muzdalifah usiku na wataswali Magharibi na 'Ishaa  'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Raka’ah tatu Magharibi kawaida na kufupisha Raka’ah mbili 'Ishaa).

 

Watabakia Muzdalifah usiku mzima kwa kumkumbuka Allaah ('Azza wa Jalla) sana.  

 

Asubuhi – Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja) kwa Mahujaji, na kwa wasiokuwepo huko ni siku ya 'Iyd. Wataelekea kutekeleza vitendo vifuatavyo vya fardhi za Hajj:

 

1) Kurusha vijiwe katika Jamaraat

2) Kutufu Twaaful-Ifaadhwah

3) Kunyoa nywele  

4) Kuchinja

(vyovyote watakavyotanguliza katika vitendo hivi inajuzu)
 

Kurusha vijiwe katika Jamaraat. 

  

 

11 – 12 Dhul-Hijjah – Ayyaamut-Tashriyq

(Siku ya kwanza na ya pili ya Tashriyq)

 

Watarudi Minaa na kwa ajili ya kurusha vijiwe katika Jamaraat.

 

Ni siku za kula na kunywa na kumdhukuru mno Allaah ('Azza wa Jalla).

 

 

13 Dhul-Hijjah (Siku ya mwisho ya Tashriyq):

 

Wanaopenda kubakia Minaa watabakia kisha watarudi Makkah na ikiwa safari imewadia watafanya Twawwaaful-Wida'a (Twawaaf ya kuaga).

 

 

Alhidaaya inawaombea ndugu zetu Waislamu wote ulimwenguni wanaokwenda kutekeleza nguzo hii ya tano ya Uislamu, Hajjun-Mabruwr, (Hajj ya kukubaliwa) Na Dhambun-Maghfuwr (dhambi za kughufuriwa) na warudi salama kwa watu wao.

 

Na inawaombea wasiojaaliwa kutekeleza nguzo hii, Allaah ('Azza wa Jalla) Awajaalie uzima na afya mwakani wawe miongoni mwa Hujaji. Aamiyn.

 

 

 

Share