Maulidi: Wazazi Hawataki Kuacha Bid’ah Wananihukumu Siwatii

 

Mawlid: Wazazi Hawataki Kuacha Bid’ah Wananihukumu Siwatii 

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalam alaykum, mimi ni msichana naependa kufuata uislam kwa usahihi wake mfano kutofuata mifumo ya bidaa mfano kusherekea maulidi, lakini natokea katika familia inayohimiza mifumo ya bidaa wazazi wangu walipogundua kama mi sipo pamoja na wao wanasema nimepotea na nimevunja agizo la kuwatii kama anavyotuamrisha Allaah (subhanahu wa Ta'aalaa) pia baba anasema namuona yeye hajui na ninamdharau na kuwafata mashekh wangu, je nifanye nini ili kuwaelekeza wazazi wang, nimeshajarib kuwaeleza lkn wanasema wao wanafuata waliyoyakuta tangu enz hizo na ndivyo walivyofundishwa. Tafadhali naomba ushauri wenu. Napenda pia kuwaombea kila la kheri kwa kujitolea kwenu Allaah Awazidishie Aamiin.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Allaah Aliyetukuka na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wamehimiza sana kuwa wazazi ni lazima waheshimiwe na watiiwe kwa hali na mali. Hata hivyo, kuwatii wazazi haifai kuwa juu ya kumtii Allaah Aliyetukuka. Kwa hiyo, ikiwa kuwatii wazazi kutakwenda kinyume na shari’ah ya Kiislamu basi haifai kuwatii lakini inatakiwa ukae nao kwa kuwaheshimu.

 

Kuhusu hilo Allaah Aliyetukuka Anasema:

 

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿١٤﴾وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ

Na Tumemuusia insani kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa katika miaka mwili; ya kwamba, unishukuru Mimi, na wazazi wako; Kwangu ndio mahali pa kuishia. Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Na suhubiana nao kwa wema duniani, na fuata njia ya anayerudi kutubia Kwangu. [Luqmaan: 14 – 15].

 

 

Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba" [at-Tirmidhiy]

 

Nasaha ambazo tunaweza kukupa kwa yanayokukumba ni kama zifuatazo:

 

  1. Kuendelea kuwafanyia wema na kuwaheshimu mbali na mitihani uliyonayo kutoka kwao. Kwa kuwafanyia hayo zaidi kuliko ulivyokuwa ukiwafanyia huenda wakarudi nyuma na kukuachilia na yale unayo yafanya.
  1. Kuvumilia wanayokwambia bila kuudhika.
  1. Zungumza nao kwa njia nzuri kuhusu Uislamu kwa jumla na yale wanayotakiwa Waislamu kuyafanya ili wawe Waislamu wazuri.

     4. Ikiwa wanajua kusoma jaribu kuwapatia makala au vitabu kuhusu Uislamu kwa ujumla.           Unaweza pia kuwatafutia kanda au CDs au Video za mawaidha ili waweze kusikiliza.

 

Twataraji kuwa kwa kufanya hayo huenda wakaelewa na wakawa ni wenye kubadilika kwa yaliyo mema na mazuri kwenu nyote.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share