Babu Amefariki Ameacha Watoto 7 Wa Kike...

Babu Amefariki Ameacha Watoto 7 Wa Kike...

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalam aleykum wa rahmatullah wabarakatu,

 

Naomba kuuliza kuwa Babu yangu amefariki ameacha mke na watoto 7 wakike na waume zao, mmoja alikuwa mume wake ameisha fariki na walikuwa na bin ami yao mmoja, sasa hapa kwanza nataka kujua mirathi yao itakua vip? Pili palipita muda hapa kurithiwa kuwa wasia alisema mali aliyo acha Babu yana deni ni mpaka lipite deni, ilipo malizika deni wasii akasema kua hizi mali nime usiwa kila mtu chake na akafanya hivo, lakini tuliona kua wasiya huo kua ume wapa wengine zaid kuliko wengine kwa mfano nyumba 7 kila mtu kapata yake lakini kuna shamba wame chukua dada wawili na waume zao kwa sababu ni wana wa mjomba kwa shangazi na waume zao ni ndugu kuna nyumba pia wamechukua. Sasa kuna matatizo wajukuu wadai haki ya mama yao na watoto wengine mama zao wamishafariki pia wadai. Na hapa ndio naomba msaada wa marifa juu ya urithishaji wa mali hizi? Namna ya urathi huu. Wa shukran Jazaka Allaah kheir

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tufahamu kuwa Mirathi hugawanyiwa warithi pindi madeni yote ya aiyefariki yanapolipwa kwa wanaomdai. Ikiwa aliyefariki pia ameandika wasiya kwa watu wengine wasiorithi wapewe au kutoa wakfu kwa Msikiti au Madrasah, hizo pia zitolewe kabla ya watu kurithishwa. Hata hivyo, wasiya huo haufai kuzidi thuluthi ya mali yake.

 

Pia tunafaa tuelewe kuwa waume wa binti za aliyefariki hawarithi chochote kutoka kwa baba mkwe wao. Na tena ikiwa watoto wa aliyefariki wameaga kabla ya baba yao mzazi pia nao hawatakuwa ni wenye kurithi. Tufahamu kuwa hakuna wasiya kwa wanaorithi na kukiwa na wasiya unaokwenda kinyume na mgao wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)   na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Madada wawili kurithi zaidi ya wengine ni makosa Kidini na haifai kuwa hivyo kabisa. Na waume wa hao madada wawili hawana urithi kutoka kwa baba mkwe wao, hivyo kurithishwa ni makosa ambayo yamefanywa. Kwa hiyo, wanatakiwa warudishe hizo walizorithi kwani si haki yao, yaani madada hao wawili na waume zao.

 

Pia binamu na wajukuu hawarithi. Wajukuu watarithi tu kwa mama zao walioaga dunia. Na ikiwa wapo mabinti wa aliyefariki walioaga kabla ya baba yao basi pia wao hawatakuwa na sehemu yoyote ya mgao wa kutoka kwa baba yao.

 

Ikiwa mabinti wote waliaga dunia baada ya aliyefariki baba yao, basi mgao utakuwa kama ufuatao:

 

1.     Mke atapata thumuni (1/8 au 12.5%).

2.     Kila binti atapata pia thumuni (1/8 au 12.5%).

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share