Ndugu Amefariki Ameacha Mama, Watoto 3 wa Kike Na 1 Wa Kiume Na Kuna Hisa Ya Mali Yake
SWALI:
Asalam aleikum
Niko na swali ambalo laleta vita katika familia na ni habari ya urathi nina ndugu ambaye amefariki na amwecha watoto wane - watatu wa kike na moja wa kiume, na mimi katika hio mali nina share pia na amwecha mama, ndugu wa kiume tatu na dada moja sasa hii mali itagawanywa vipi. Naomba msaada katika haya maswala.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu urithi wa ndugu aliyeaga dunia.
Awali ya yote ni kuwa kabla ya mgao kufanywa inatakiwa ijulikane hisa ya marehemu. Wewe kama ndugu ambaye mlikuwa mnashirikiana naye katika
Baada ya kujulikana hisa yake, sasa ndio mnaweza kuigawa. Maadamu marehemu ana watoto, ndugu zake wa kiume na wa kike hawatorithi chochote. Kulingana na swali pia inaonyesha marehemu kaka yako hakuacha mke wala baba kabisa. Ima alikuwa na mke akamuacha au ameaga dunia kabla yake ilhali baba yake mzazi inaonyesha naye ameaga. Ikiwa wapo hai itabidi mtueleze mnapopata jibu kwa swali lako hili. Ikiwa ni hivyo mgao wao utakuwa
1. Mama atapata sudusi ya
2. Mtoto wa kiume atapata thuluthi (1/3 au 33.3%).
3. Ilhali watoto watatu wa kike watagawa nusu ya hiyo
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
