Urithi Wa Mke Na Mtoto

 

SWALI:

ASALAAM ALEIKUM,   

 (1)  MIMI NAITWA ****,MUME WANGU AMEFARIKI NA KUNIACHA NA MTOTO MMOJA WA KIUME UMRI WA MTOTO HUYO NI MIAKA 6.  MUME WANGU PIA AMEACHA MAMA MZAZI WAKE NA KAKA ZAKE 3 NA DADA ZAKE 3, BABA WA MUME ALIFARIKI KABLA YA MUME WANGU, SWALI LANGU NI: NATAKA KUJUA NANI NA NANI ANARITHI MALI YA MUME WANGU, NA PIA MGAWANYIKO WA MIRATHI BAINA YA WANAORITHI.

 (2)  SWALI LA NYONGEZA:MALI YA YULE MWANANGU YATIMA NANI ANAYO HAKI YA KUKAA NAYO BAINA YA MIMI MAMA YAKE AMA KAKA WA MUME WANGU

 (3)   TUNAOMBA HILI SWALI MUTUJIBU KWA HARAKA MAANA MUME WANGU KAFA WIKI YA JANA NA KAKA ZAKE WAMEKUJA JUU WANATAKA MALI ZA MUME WANGU.

 WABILLAHI TAWFIK

 


 

JIBU:  

Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tunakupa pole zetu kwako kwa kufiwa na mumeo. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akupe subira ambayo unaiihitaji wakati huu, Akusahilishie maisha yako mapya, na Amghufurie aliyefariki na Amrehemu. Aamiyn. .

Pili tunakushukuru kwa kuweka maudhui iliyowazi jambo ambalo linatufanyia wepesi katika kazi hizi za kujibu maswali

Shukran kwa swali lako ambalo umesema ni la haraka lakini tumeshindwa kufanya haraka unayoihitajia kwa sababu ya shughuli nyingi za mwezi huu mtukufu wa Ramadhaan.

Hesabu za kugawa urithi ni kama ifuatavyo ikiwa kima kilichoachwa ni shilingi 100: 

Warithi

Uhusiano na aliyekufa

Hela

Hukumu

1

Mama

16.667

Kwa sababu ya kuwepo kwa mtoto wa aliyefariki anapatiwa sudus (1/6).

2

Mtoto 1

70.833

Mtoto anachukua baki ya urithi.

3

Mke 1

12.5

Kwa sababu ya kuwepo kwa mtoto sehemu yake ya wirathi itakuwa ni thumun (1/8)

4

Kaka 1

0

Kaka na dada wanazuiliwa kurithi kwa sababu ya kuwepo kwa mtoto.

5

Kaka 2

0

 

6

Kaka 3

0

 

7

Dada 1

0

 

8

Dada 2

0

 

9

Dada 3

0

 

 

Jumla

100

 

Hii ndiyo jadwal ya ugawaji urithi wa mume aliyeaga dunia.

 
Kuhusu swali  la pili :

Hili ni kuwa yule mwenye kumlea mtoto ndiye mwenye haki ya kukaa na mali ya mtoto huyo. Mlezi anatakiwa ajali maslahi ya mtoto mpaka atakapo baleghe na kuwa na akili timamu (Qur-aan kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)

((   وَابْتَلُواْ الْيَتَامَى حَتَّىَ إِذَا بَلَغُواْ النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُواْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ وَلاَ تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُواْ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُواْ عَلَيْهِمْ وَكَفَى بِاللّهِ حَسِيبًا ((

(( Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliyekuwa tajiri naajizuilie, na aliye fakiri basi naale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Allaah Anatosha kuwa Mhasibu)) [An-Nisaa:6]

Kwa kuwa kaka wa aliyefariki wanaonekana ni mapapa na wanataka mali ya ndugu yao hata kabla ya kumaliza eda ya shemeji yao. Hivyo, yule ambaye anaweza kuwa na maslahi ya mtoto huyo ni mama mzazi ambaye hatakula mali hiyo. Twamuombea kila la kheri dada yetu na aweze kupata haki yake.

Na Allah Anajua zaidi

 

 


Share