Mama Amefariki Ameacha Watoto Wanne – Ana Shamba – Kabla Ya Kufariki Aliolewa Na Mume Mwingine Ambaye Hakuzaa Naye

Mama Amefariki Ameacha Watoto Wanne,  Ana Shamba Kabla Ya Kufariki Aliolewa

Na Mume Mwingine Ambaye Hakuzaa Naye

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Asalam alaikum

 

Sifa zote ni za Allah Subhanna wa Taalaa. Kwa kutuwezesha kuvuta pumzi mpaka dakika ya sasa.

 

Swali langu haswa ni hili: Kuna mama kafariki ameacha nyumba moja shamba eka tatu. Amezaa watoto 4. Watoto 2 wakike na wawili wakiume. Kabla ya kufariki alikuwa ameolewa na mume ambaye hakuzaa nae. Pia mume huyu hakumpa mahari yake huyu aiyefariki.

Tatu mwanamume huyu hakujushuhulisha kumtizama mkewe alipokuwa anaugua. Watoto wamemuuguza mama yao, wakamlipia madeni. Mume hakufanya chochote zaidi alileta pesa za sanda baada ya mke kuzikwa. Je mume huyu afaa kurithi? Pia watoto wamesaidiana na aliyefariki mama yao kujenga nyumba je huyu mume anahaki ya kurithi? Shukran

 

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwa hali yoyote ile mume anamrithi mkewe ila anaporitadi ndio Kiislamu mume hatoweza kurithi. Mume kuwa ameacha majukumu yake ya kimsingi kwa kumtizama mkewe ni makosa yake mume naye atapata madhambi kwa kupuuza huko na makosa hayo aliyoyafanya. Hata hivyo, makosa yake hayo hayamfanyi yeye kukosa wirathi wake kwa mkewe.

 

Ikiwa mke hakupatiwa mahari na mume, inategemea sasa mke mwenyewe, je alimsamehe mumewe asilipe kabla ya kuaga kwake au hakumsamehe na alikwua anatazamia kupata kutoka kwake. Ikiwa alimsamehe litakuwa si deni tena na lau hakusamehewa basi katika ile sehemu yake ya mirathi itabidi akatiwe pesa hizo ambazo wka sasa ni haki ya warithi yeye akiwa ndani. Mfano ikiwa mahari ya mke yalikuwa ni shilingi 10,000, pesa hiyo itaongezwa katika ile thamani ya vitakavyorithiwa kisha igawanywe kila mmoja apate haki yake.

 

Kama tulivyotangulia kusema kuwa ikiwa mume hakushughulika hayo yatakuwa ni madhambi yake kwa kukosa kutekeleza wajibu wake. Ama watoto kusaidiana na mama yao kujenga inategemea:

 

  • Je, watoto hao walikuwa wanamsaidia kama mama yao mzazi tu. Ikiwa wamefanya hivyo watapata ujira mkubwa kwa Allaah ('Azza wa Jalla)  kwa kufanya ihsani hiyo lakini hawatakuwa na haki ya kile walichokitoa kwani wamemfanyia mama yao.

 

 

 

  • Ikiwa walitoa waingie katika shirika na mama yao, hapo watakuwa na haki na itabidi pesa waliyoitiwa iwe itatolea katika kutia thjamani mali ya aliyefariki mama.

 

 

 

Kwa minajili hiyo, mirathi ya kila mmoja itakuwa kama ifuatavyo:

 

 

1-Mume ambaye atapata robo ya mali ya aliyefariki kwa kuwa aliyefariki alikuwa na watoto. Hii ni kwa mujibu wa maneno yafuatayo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)   

 

وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ

Nanyi mtastahiki nusu katika walichoacha wake zenu ikiwa hawakuwa na mtoto. Na ikiwa wana mtoto, basi mtastahiki robo katika walichoacha, baada ya kutoa wasia waliyousia au kulipa deni.   [An-Nisaa: 12]

  

 

 

2-Watoto watagawa kilichobaki yaani robo tatu (3/4), wakiume watapata sehemu mbili kwa ya kike moja. Hii ni kwa mujibu wa kauli ifuatayo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)   

 

يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۚ   

Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili.  [An-Nisaa: 11]

  

 

Kwa hiyo, kila mtoto wa kiume atapata robo na wakike kila mmoja atapata thumuni (1/8).

 

 

Mirathi igawanywa baada ya kutoa madeni anayodaiwa aliyefariki na wasiya alioacha.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share