Mali Ya Urithi Iliyokuzwa Na Ndugu Mmoja Inakuwa Haki
SWALI:
Assalam alykm warahmatu LLah wabarakatuh, ama baada salam ningependa kuwapongeza ndugu zetu kwa bidii yenu na ishaAllah Allah awaeeke mahala pema, amin. Tafadhali naomba kujua taratibu za miradhi hulingana na
1. baba amefariki ameacha urathi walakin kabla kufariki alimuachia mkubwa wetu aendeleze biashara ya duka, ndugu yetu akafanya bidii na kuliendeleza kwa kiasi kikubwa na kuzaa biashara zingine. Jee nani anahaki ya kumiliki yote haya, yeye ama sisi sote?
2. baba ameacha nyumba ikiwa ina thamani duni baadaye huyu ndugu yetu akaiboresha na ikawa inatoa kodi kubwa, jee hizi kodi pamoja na nyumba ni haki yake ama yetu sote na kama ni sote fungu lake na ndugu zake wengine wa kiume litakuwa sawa na vipi mirathi yatatekelezwa baada ya kujibu nawaomba kunijulisha kama kuna electronic book nikasoma zaidi. shukran jazila wallahu yajzykum
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi ya baba baada ya kufa. Hakika hili ni suala nyeti katika masuala ya kijamii mbali na kuwa ni suala lenye mfumo mzuri uliowekwa na Allaah Aliyetukuka. Inatakiwa matatizo yote ambayo yanajitokeza katika mas-ala ya mirathi yaelekezwe katika Qur-aan na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na utata wote utaondoka.
Awali ya yote ni kuwa baba anapokufa huwa anaacha watoto akiwa amebariwa nao
Allaah Aliyetukuka Anatuambia yafuatayo kuhusiana na
Tunapata kuwa Maimaam al-Bukhaariy na Muslim wamenukuu Hadiyth kutoka kwa ‘Abdillaahi bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) aliwasimulia kisa kuhusu watu watatu waliofungiwa na jiwe katika mlango wa pango. Walimuomba Allaah Aliyetukuka kwa amali zao njema. Na mmoja wao alikuwa na mfanyikazi ambaye hakuchukua ujira wake wa siku. Huyu mwajiri akatumia ujira huo kwa kuufanyia biashara mpaka ikazaa ngamia, ng’ombe, mbuzi na watumwa. Na mwajiriwa aliporudi kutaka ujira wake, mwajiri akamwambia kuwa kila unachoona ni chake, naye akachukua kila kitu bila kumbakishia chochote. Jiwe likaondoka kwenye mlango na wakawa ni wenye kutoka huku wanatembea. Huu ni uadilifu wa hali ya juu kabisa mpaka mwajiri huo akapata radhi za Allaah Aliyetukuka seuze ndugu ambaye anatakiwa awe ni mwenye kuwajali zaidi ndugu zake ambao kwa sasa wa wamekuwa.
Tukirudi kwa maswali yako mawili ni kuwa tunasema hivi: Ikiwa
Nasaha ambayo tunaweza kukupeni ni kuwa msiwe na pupa kwa hilo bali inatakiwa mzungumze hayo katika kikao kwa busara, utaratibu mwema ili kila mmoja apate haki yake katika mali na faida. Tunamuomba Allaah Aliyetukuka ikiwa kuna mzozo wowote usiwe ni wenye kulipuka bali msuluhishe kwa njia iliyo muafaka pamoja na kuwashirikisha wazee wenu waliobakia.
Na Allaah Anajua zaidi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
