Maulidi: Kumfanyia Maulidi Mtoto Anapotahiriwa Jando Inajuzu?

 

Mawlid: Kumfanyia Maulidi Mtoto Anapotahiriwa Jando Inajuzu?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalaam Aeikum Ndugu zangu katika Uislam,

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa, kwa kunijaalia uzima na afya njema na uwezo wa kuweza kufahamu mtandao huu wa Alhidaaya. Katika siku ya leo napenda kuuliza maswali yafautayo ambayo yamekuwa yakinitatiza kichwani mwangu.

 

Je ni halali kufanya sherehe ya kama kusoma maulidi baada ya mtoto wa kiume kupatiwa sunna (kutahiriwa)? 

 

Natanguliza shukrani zangu kwa Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa na nyinyi pia ndugu zetu wa Alhidaaya. Wabillah Tawfiq

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Kufanya sherehe mtoto anapotahiriwa lililothibiti ni kufanya ‘Aqiyqah, na hakuna kusoma Mawlid wala sherehe nyinginze zaidi ya hiyo. Na kusoma Mawlid ni uzushi ambao unapachikwa kila eneo; imekuwa kwenye ndoa kunasomwa Mawlid, kwenye kuzaliwa mtoto kunasomwa Mawlid, kwenye mfungo sita kunasomwa Mawlid; imekuwa ni kama jambo la kishari’ah kwa wengi hivi sasa na wengine hata hawaamini au hawakubali kuwa mambo kama hayo si katika dini. Imekuwa leo hii yale ya Sunnah kama kufanya ‘Aqiyqah yanaachwa na yale ya bid’ah kama Mawlid ndio hufanywa.

 

Na maelezo kuhusu anayopaswa kufanyiwa mtoto anapozaliwa yamo ndani ya viungo hapa chini:

 

Utaratibu Wa 'Aqiyqah Katika Sunnah

 

'Aqiyqah

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share