Jimai Wakati Mwanamke Ana Mimba

 

SWALI:

 

Aslam aleikum,

 

Kwa ufupi swali langu ni kama ilivo katika subject, je inafaa jimai wakati mwanamke anamimba, na wakati gani inafaa akiwa ana mimba. washukran.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kujimai na mkeo wakati akiwa na mimba.

Hakuna tatizo kabisa kishari’ah kwa mume kumuingilia mkewe wakati ana mimba hata ikiwa atazaa kesho. Itakatazwa tu ikiwa labda mke ana matatizo na kujimai wakati huo ima kwa kuumia au kudhurika.

 

Ama kuhusiana na wakati wa jimai, Uislamu haukuweka wakati maalumu ila hayo yanategemea masikizano yenu nyinyi wanandoa. Mnaweza kufanya baada ya Alfajiri au kabla yake, baada ya Dhuhr au baada ya ‘Ishaa au wakati mwengine wowote. Kinachokatazwa ni kufanya jimai wakati wa Swalah hivyo kuikosa au wakati ambao mmefunga Funga ya faradhi. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameagizia kuwa mke asikatae kumstarehesha mumewe hata akiwa kwenye tanuri. Hii ina maana kuwa ikiwa mume amerudi nyumbani na mke yuko jikoni, mume anapomtaka inabidi atoke huko kwenye kazi yake ili kumkidhia haja mumewe.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share