Kuolewa na Mume Aliyeahidi Kuacha Maasiya Lakini Hakuacha Sasa Hana Maelewano Naye Aombe Talaka?

ASALAM ALAIKUM WARAHMATULLAHI WABARAKAT

 

NASHUKURU SAANA ALLAH KUNIEZESHA KUPATA WEB SITE YENU IMENIFUZA MENGI NABADO NAEDELEYA KUFATIZA. NINA SWALI LANGU NAOBA JAWABU YENU

 

MIMI NAFANYA KAZI OFFICIN SECRETARY NAPOKEYA SALARY ALHAMDULILLAH YAKUTOSHA. LAKINI NILIHAGAIKA FASI PA KUISHI KISHA NIKAPATA JAMA PIYA KUTOKA **** WAKANIKARIBISHA KWAO NIKAISHI LAKINI SINA RAHA. ALHAMDULILLAH NIWATU WAZURI SAANA ALLAH AWAZIDISHIYE EMAAN. NIKAWA NATAKA ATA NIOLEWE ILE BASI. NIKAPATA MWANAUME MWENYE MIAKA 45 PIYA KUTOKA ****  AKANIOBA KUOLEWA NAYE NIKAMUOBA MUDA NIPATE KUFIKIRIYA. NIKAULIZIYA KWA WATU. NIKABIWA ANALA MAIRUGI, MLEVI, BAGI, WALA HASALI.

 

LAKINI NIKAABIWA NIMUTU MWENYE ROHO ZUURI PEGINE AKIKUWOWA ATAWACHA.  NIKAAMWABIYA AKASEMA ATAWACHA IZO VITU ZOTE AKISHA KUWOWA. NIKASALI SALAT ISTAHAR NIKAOBA IKIWA ANAKHER NAMIMI ANISAHLISHIYE. MARA NYINGI NA SALA NIKIOBA. MABO YAKAWA NYEPESI TUKAWOWANA SASA MIEZI 7 POMBE AMEACHA LAKINI ZEGINE HAJAWACHA. NAKILAMARA NAMWABILIYA INAKUWA NIUGOVI NA KWA MAMBO YA DOA ANAJIRIDHISHA YEYE BASI KILA SIKU NIKIMWABIYA HAIFAYI KWA DINI ANANIGOBANISHA NAKUNITOKANA MANENO MABAYA SANA.  PAKA NIMEFIKA KUMUCHUKIYA ATA SINA HAJA NAYE SIMUSHUGHULIKIYA TENA KWA MAMBO MEGI ABAYO INAFA KWA DINI. LAKINI NASUBIRIYA KWA AJILI AMALIZE DENI ZENYE TUNAZO KISHA NIMUOBE TALAKA YANGU. NAOBA MUNIFAHAMISHE KAMA INAFA KUMOUBA TALAKA YANGU KISHA NIBAKI KWANYUBA NIJILIPIYA MAHITAJI ZOTE NAOBA USHAURI YENU DUNGU ZANGU. INSHAALLAH ALLAH AZIDI KUWAPA AFYA, UZIMA NA KILA LA KHRI HAPA DINIAAN

 

ASLAMA ALAIKUM

MIMI DADA YENU


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mwanamme aliyekuahidi kuwa ataacha maasiya yake akikuoa.

Hakika dada zetu mara nyingi huwa wanadanganyika kwa maneno matamu ambayo wanaambiwa na wanaume ambao haja zao ni kutimiza uchu wao tu. Dada zetu inatakiwa tuwe waangalifu sana wala tusijiangamize kwa ahadi za uongo mara nyingi kutoka kwa wanaume.

 

Ni afadhali sana wewe umeolewa lakini wapo wasichana wengi hupotezwa na kuingizwa katika uzinifu kwa ahadi ya kuolewa baadaye. Na mara zote ahadi hizo huwa hazitekelezwi kabisa. Ikiwa hali ni hiyo kutoka kwako tuliyoisikia, jaribu tena kumnasihi, kwani ameweza kuacha moja anaweza kuacha na mengine. Ikiwa amefuata nasiha vyema na lau hakufuata wewe utapata thawabu za kutoa nasaha.

 

Ikiwa hatokuwa ni mwenye kubadilika katika hilo basi tafuta marafiki zake au watu wanaoweza kusikiliza ili wazungumze naye kuhusiana na hayo maasiya. Ikiwa pia hakubadilika, itabidi mkutane wewe, yeye na wazazi wenu ili kujadili suala hilo na ikiwa wazazi hawapo karibu basi nenda mara moja kwa Qaadhi au Shaykh mwadilifu ili awasulishe katika tatizo lenu hilo.

 

Fuata utaratibu huo wa kutaka kuleta mabadiliko na kuiokoa ndoa hiyo yenu.

 

Tunamuomba Allaah Aiyetukuka Akufanyie kila la kheri katika mambo yako.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share