Mama Ameacha Watoto Watano Mmoja Wa Kike Wanne Wanaume

SWALI:

 

Assalam Alaykum.

 

Baada ya kufiliwa na Mama wetu Mungu amrehemu na waislamu waliotangulia wote....aliwacha pesa au nyumba kwa nduguye wa kike ambaye atakuwa Khaalat wetu...amabye anasema kuwa ana pesa tu na pesa zenyewe ni elfu kumi na moja za kiamerika. Na sisi ndugu tuko watano. Mmoja tu ni wa kike na umri wake ni 27 na wengine sote ni 41,34,33 na 26. Sote waume tuko na wake zetu na watoto illa mdogo wetu ambaye ni miaka 26 ambaye hajaowa napia yule wa kike pia hajaolewa. Suala ni kuwa tutagawanya hiyo $11000 vipi?

Jazakumulu Allah khairan.


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu ugawaji wa mirathi baada ya kuaga dunia mama yenu.

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Amuweke pema pamoja na wema na Amsamehe madhambi yake.

Kulingana na swali lako inaonyesha mama yenu wakati wa kuaga dunia hakuwa na wazazi wala mume. Kwa hivyo, tutalijibu swali lenu kulingana na hilo. Ikiwa atakuwa ameacha wazazi na mume, au wazazi peke yao au mume peke yake pamoja na nyinyi basi ugawaji huo utabadilika. 

Kawaida katika mirathi mtoto wa kiume hupata mara mbili ya atakachopata mwanamke. Hakuna tofauti kama mtoto ameoa au hajaoa au ameolewa au hajaolewa, kila mmoja ana kiwango chake maalumu.

Kwa hiyo, kila mtoto wa kiume atapata $ 2,444.44 na msichana atapata $ 1,222.22

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share