Sitta Shawwaal: Kufunga Ijumaa Na Jumamosi Katika Sita Ya Shawwaal Yafaa

 

Kufunga Ijumaa Na Jumamosi Katika Sita Ya Shawwaal Yafaa?

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalaam aleikum warahmatullahi wabarakaatuh, je kufunga siku ya ijumaa na jumamosi katika statu shawal ya faa?

 

 

JIBU: 

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakika funga hiyo ya Shawwaal katika masiku hayo ya Ijumaa na Jumamosi, 'Ulamaa wengi wakubwa wanaona inafaa na hakuna tatizo. Unaweza kuanza kufunga Ijumaa ukaunga na Jumamosi. Linalokatazwa ni kuifanya Ijumaa pekee kuwa ni siku ya kufunga Sunnah. Lakini kama utaunga siku nyuma yake (Alkhamiys) au siku mbele yake (Jumamosi) inafaa.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: 

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share