Vibiskuti Vya Siagi Na Jam

 

Vibiskuti Vya Siagi Na Jam

 

 

VIPIMO
 
Unga  - 2 Vikombe
Sukari ya icing  - 1 Kikombe
Siagi   - 250 gm
Yai  -  1
Vanilla    -  2 Vijiko vya chai
Baking powder -1 Kijiko cha chai
Jam - ¼ kikombe
Lozi  -   ¼ kikombe
 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
  2. Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini  kama sufi.
  3. Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
  4. Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supufanya  duara kisha weka kwenye treya ya kupikia.
  5. Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa.
  6. Pika (bake) katika oven moto wa 375° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

 

Share