Kufanya Tasbiyhi Kutumia Mkono Wa Kushoto

SWALI:

 

Salaam alaykum.

Naomba nipatiwe ufafanuzi kuhusu kusoma nyiradi (Subhanallah, Alhamdulillah,,,Allahu Akbar) baada ya sala kwa kutumia vidole, iwapo utatumia mikono yote wa kulia na wakushoto haifai? kuna mtu ameniambia kuna hadithi inakataza kutumia mkono wa kushoto,,unatakiwa utumie wa kulia pekee.,,,Naomba uafanunuzi ndugu zangu.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kufanya tasbiyb baada ya Swalaah.

Katika Sunan ya Abu Daawuud kumeelezwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitumia mkono wa kuume pekee katika kuleta tasbiyh. Hivyo inatakiwa nasi tutumie mkono huo huo kwa kufanya hilo.

 

Pia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitukataza kutumia mkono wa kushoto ila kwa mambo machafu kama kujisafisha baada ya kwenda haja na akatuhimiza kutumia mkono wa kuume kwa mambo mazuri kama kula na kadhalika.

Hivyo tasbiyh zinatakiwa zitumie mkono wa kuume kuhesabiwa na sio mkono wa kushoto.

 

Kadhalika unaweza kusoma majibu mengine katika viungo vifuatavyo:

 

Kutumia Tasbihi Katika Kumdhukuru Allaah Inafaa?

 

Inafaa Kutumia Tasbiyh Kwa Khofu Ya Kupotewa Hesabu?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share