Vipi Atahakikisha Kama Msichana Anayetaka Kufunga Naye Ndoa Ni Bikra; Na Kama Si Bikra Atajua Vipi?

SWALI:

 

S/Alaykum napenda niulize nakama itakua kuna makosa naomba unisidie. natarajia kufanya ndoa karibuni, vipi nitahakikisha kama huyu mtarajiwa mwenzangu ni bikra siku ya mwanzo nitakapo fanya nae tendo la ndoa? Nilazima nitaona damu ya bikra? Na vipi nitajua kama si bikra? AHSANTE KWA MAJIBU. WABILLAH TAWFIQ


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu vipi kuhakikisha ubikra wa msichana.

Mwanzo ni kutafiti kuhusu msichana huyo na familia yake pamoja na mahusiano yao na Uislamu Kidini na Akhlaaq. Ikiwa msichana mwenyewe ni yule aliyeshika Dini sawasawa basi atakuwa amejihifadhi kwa njia iliyo nzuri.

 

Tufahamu kuwa mvulana anataka msichana ambaye hajatembea nje na vilevile msichana anahitajia mvulana aliyejihifadhi kutokana na uasherati. Ni rahisi kwa msichana kufahamika kama ni bikra lakini hakuna vipimo kwa wavulana. Wewe unataka bikra je, wewe ndugu yetu ni bikra?

 

Ama msichana ambaye ni bikra, usiku wa mwanzo wa kulala na kujamiiana na mwanamme anakuwa na hayaa ya kupita kiasi. Na mvulana anapomuingilia basi hutoka damu kwa kupasua kile kizinda.

Hata hivyo, wapo wasichana wachache ambao wanakuwa kinyume na maumbile hayo ya kutoka damu lakini kwa yule aliye bikra inakuwa ngumu kujimai usiku huo wa mwanzo, na msichana hupata maumivu makubwa.

 

Ishara hizo zote zinaashiria ubikra wa msichana.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kumsubiri Bibi Harusi Nje Ya Mlango Kujua Kama Ni Bikra (Kijibu Harusi)

 

Kuna Hukmu Msichana Ameolewa Na Hakukutwa Na Bikra?

 

Anatangaza Kuwa Mke Wake Ni Bikra

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share