Utumiaji Kondom Kwa Mke Anaedai Kuwa Ni Mgonjwa

SWALI:

Asalam Alaikum Warahmatullah Wabarakatu

Ndugu zangu limenikuta tatizo kwa mke wangu kuwa kila tunapokutana kimwili mke wangu ananilazimisha kutumia kondom kwa madai yeye amekatazwa na daktari asije akashika mimba kwa vile yeye ni mgonjwa nimemshauri nioe mke mwengine na nilijaribu kuoa lakini yeye alitaka kunya sumu nikamwacha huyo mke sio kwa sababu hiyo sasa hivi ninapangiwa kila mwezi mara moja na mimi si faidiki na hivyo je huyu mke nimfanye nini kwa vile nimekwisha zaa nae watoto 4.


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu utumiaji wa kondom kwa mkeo.

Mke anapokuwa mgonjwa mume anatakiwa akae naye kwa wema kabisa kwani mlikuwa katika hali ya furaha mlipokuwa nyote ni wazima.

Pia ni vyema kama mume ujue hali ya mkeo na ugonjwa yaani ni lazima ujishughulishe kuhakikisha kwa uwezo ulio nao wa kumpeleka kwa madaktari tofauti waliobobea katika fani hiyo ili waweze kumtibu.

Ikiwa kondomu hiyo ndio itamsaidia kutopata mimba kwa sababu ya ugonjwa kutakuwa hakuna tatizo kishari’ah kwa mume kuivaa. Hata hivyo, inatakiwa hilo liyakinishwe na daktari mzoefu katika fani hiyo ya utabibu wa kizazi.

Ikiwa umejaribu kwa uwezo ulio nao lakini hakuwa ni mwenye kupona basi kaa naye kwa wema na uoe mke mwengine ili uweze kutimiza mahitaji yako ya kimwili usiwe ni mwenye kwenda nje katika zinaa. Na mas-ala ya kuoa mke wa pili katika shari’ah si lazima kutaka ruhusa mke wako wa kwanza. Ikiwa anafanya hivyo alivyofanya mpaka ukamuacha mke wako wa halali yeye mke atakuwa na dhambi nawe pia utakuwa na makosa ya kumuacha mke bila ya sababu yoyote. Inabidi uzungumze naye au utume watu wa kuzungumza naye juu ya suala hilo la shari’ah. Shari’ah hiyo ndiyo inamfanya yeye asitirike kwa hali ambayo ni njema.

Tafadhali bonyeza viungo upate maelezo zaidi:

Utumiaji Wa Mpira (Condom)

Kuzuia Mimba Na Madhara Yake

Uzazi Wa Kupanga Unafaa?

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share