'Aqiyqah Ni Lazima Wapatikane Mbuzi Weupe Tu?

SWALI:

 

assalam alykum warahmatu llahi wabrakatuh.

 

suala langu ni hili jee katika kufanya aqykah ni lazima wapatikane mbuzi weupe tuu? wabillah tawfiq

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu suala la ‘Aqiyqah.

 

Kwa hakika, ‘Aqiyqah inafanywa kwa kuchinjwa mnyama yeyote aliyekubaliwa na shari’ah kama kondoo au mbuzi.

 

Ama kuhusiana na rangi wanyama hao wanaweza kuwa wa rangi yoyote ile akiwa ni mweusi, mwekundu, mweupe, amechanganya rangi na kadhalika.

Kinachotakiwa kwa mnyama ni kuwa asiwe na ila ya aina yoyote ile kama kuwa kilema, kipofu, na kadhalika.

 

Zaidi utapata faida katika makala zifuatazo:

 

Utaratibu Wa 'Aqiyqah Katika Sunnah

 

'Aqiyqah

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share