Kutoa Mimba Isiyotimia Mwezi, Yaani Kabla Haijapuliziwa Roho, Atakabiliwa Na Hukumu Ya Kuua? Na Ataweza Kusamehewa?
SWALI:
Asalam aleykum ndugu zangu waislamu natanguliza samahni
Mimi ni dada wa kiislam nataka kujua je mtoa mimba anasamehewa sababu niliwahi kusikia kama kuna hukmu yakuuwa
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu kutoa mimba.
Hakika ni kuwa Allaah Aliyetukuka Amekataza kutoa mimba au kuua kiumbe kwa hofu ya rizki. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuhimiza tuoane ili tupate kuzaana na kuwa wengi kwani kwa
Ni hakika isiyopingika kuwa mtoto anapokuwa tumboni kwa mama yake kwa muda wa siku arubaini, akiwa katika hali ya mbegu, baadaye tone la damu kwa muda kama huo, tena huwa ni kipande cha nyama kwa muda kama huo, tena hupelekwa Malaika anayempulizia pumzi za uhai. Hivyo, roho inatiwa katika mwezi wa nne.
Hii haimanishi Uislamu umekubali kiumbe kitolewe kwenye tumbo la mama yake akiwa hajafika mwezi wa nne.
Hata kikiwa kiumbe kina siku moja tumboni, hairuhusiwi kabisa kukiua. Na mtu akifanya hivyo atapata madhambi makubwa ya kuua.
Kuna hali ambazo zimeruhusika kukitoa kiumbe tumboni kwa mama yake kikiwa amepuliziwa roho au bado kupuliziwa roho. Hali hiyo ni kikiwa kukua kwake kunakhatarisha maisha ya mama mzazi.
Ikiwa ulifanya kosa
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:
Kutoa Mimba - Hukmu Na Kafara Yake
Kutoa Mimba Ikiwa Ikiachwa, Mtoto Atakuwa Mgonjwa Au Kufariki Baadaye
Na Allaah Anajua zaidi