Sitta Shawwaal: Ufafanuzi Wa Thawabu Za Sita Shawwaal Kama Swiyaam Za Mwaka Mzima

 

 

Sitta Shawwaal:

Ufafanuzi Wa Thawabu Za Sita Shawwaal Kama Swiyaam Za Mwaka Mzima

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Asalam alaykum

 

Nataka kujua vipi imekusudiwa kuwa mtu akifunga sita atapata thawabu za mwaka mzima? Maana nimesikia kwamba ikiwa hukutimza Ramadhani basi hupati thawabu hizo je, ni kweli?

Nitashukuru kupata jibu kabla ya mwezi wa sita kwisha

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hayo ni kutokana na Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

(( من صام رمضان ثم أتبعه ستًّا من شوال كان كصيام الدهر)) أرجه مسلم في صحيحه

((Atakayefunga Ramadhwaan kisha akafuatiliza na siku sita za mwezi wa Shawwaal itakuwa kama ni Swiyaam ya mwaka)) [Muslim]

 

 

Inavyompasa Muislamu ni kwamba anatakiwa kwanza alipe deni lake la Ramadhwaan kisha ndio afunge 'sitatu Shawwaal' ili aweze kupata thawabu za kama kafunga mwaka mzima. Na 'Ulamaa wameona hivyo ni kutokana na dalili zifuatazo katika Qur-aan na Sunnah:

 

Katika Qur-aan:

 

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

 

((مَن جَاء بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا وَمَن جَاء بِالسَّيِّئَةِ فَلاَ يُجْزَى إِلاَّ مِثْلَهَا وَهُمْ لاَ يُظْلَمُون))

((Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu. Na wao hawatadhulumiwa)) [Al-An'aam:160]

 

Katika Sunnah:

 

Kuna Hadiyth mbali mbali zinazothibitisha kauli hiyo ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala), tutazitaja hapa mbili:

 

Ya kwanza ambayo kutokana na Imaam At-Tirmidhiy kuwa ni sababu ya kuteremshwa Aayah hiyo:

 

 ((من صام ثلاث أيام من كل شهر فقد صام الدهر كله))

((Atakayefunga siku tatu katika mwezi atakuwa amefunga mwaka mzima)) [Ahmad, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth ya pili:

 

عن أبي العبَّاسِ عبدِ اللهِ بنِ عباسِ بنِ عبد المطلب رضِيَ اللهُ عنهما، عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فيما يروي عن ربهِ تباركَ وتعالى قَالَ: ((إنَّ اللهَ كَتَبَ الحَسَنَاتِ والسَّيِّئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَها اللهُ تَبَارَكَ وتَعَالى عِنْدَهُ حَسَنَةً كامِلَةً، وَإنْ هَمَّ بهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ عَشْرَ حَسَناتٍ إِلى سَبْعمائةِ ضِعْفٍ إِلى ضعَافٍ كَثيرةٍ، وإنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلةً، وَإنْ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً)). مُتَّفَقٌ عليهِ.

‘Abul-‘Abbaas, ‘Abdillaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika aliyopokea kutoka kwa Rabb wake Tabaaraka wa Ta’aalaa: Amesema:  ((Kwa hakika Allaah Ameandika mema na mabaya, kisha akabainisha hayo: Atakayefanya hamu ya kutenda jema kisha asitende, Allaah Aliyetukuka Atamuandikia Kwake jema moja kamili. Na akilifanyia hamu na akalitenda, Allaah Atamuandikia mema kumi hadi nyongeza mia saba, hadi nyongeza nyingi zaidi (zaidi ya hizo). Na akifanya hamu ya kutenda jambo baya kisha asilitende, Allaah Atamuandikia Kwake jema kamili. Na akifanya hamu ya kulitenda na akalitenda, Allaah Atamuandikia baya moja)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Kutokana na dalili hizo, kwamba kila jema mtu anapata mara kumi, hivyo Swawm ya Ramadhaan itakuwa ni hivi:

 

       30 x 10  = 300

 

Na funga ya 'sitatu Shawwaal' itakuwa ni 6 x 10  = 60

 

300  + 60  = 360

 

Hivyo siku 360 ni sawa taqriban na mwaka mzima. 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share