Tafsiyr Ya Imaam As-Sa'dy: Kufaridhiswa Swawm

Tafsiyr Ya Imaam As-Sa'dy:  

Kufaridhishwa Swawm

www.alhidaaya.com

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾

Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 183]

 

Allaah Anajulisha katika Aliyoyafadhilisha kwa waja Wake kwamba Amewajibisha Swawm kama Alivyowajibisha ummah zilizopita kwa sababu ni shariy’ah (hukmu) na amri zinazomnufaisha bin Aadam katika kila zama.

 

Nayo ni changamoto ya kumhuisha mtu nafsi yake kwani inapasa kushindana na wengine katika mambo ya khayr ili mkamilishe 'amali zenu na mkimbilie (kuchuma) sifa njema na hakika hayo si katika mambo mazito mliyohusishwa nayo.

 

Kisha Allaah Anataja hikma Yake kuhusu Shariy’ah ya Swawm, Anasema:

لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

mpate kuwa na taqwa

 

kwamba Swawm ni sababu kuu ya taqwa (kumcha Allaah) kwa kuwa ni kutekeleza amri za Allaah na kujiepusha na yaliyokatazwa.

 

Kwa hiyo katika Swawm yanapatikana yafuatayo:

 

  1. Taqwa ya asw-swaaim (anayefunga swawm) huacha yote Aliyoyakataza Allaah; kula, kunywa, kujimai na kama hayo, na yote yanayoelemea nafsi yake kuyatamani; hapo basi hujikurubisha kwa Allaah kwayo akitaraji thawabu kwa kujiepusha nayo. Haya yote ni kutokana na taqwa. 

 

  1. Na Swawm pia inamfunza mtu kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) basi hujiepusha na hawaa ya nafsi yake, kwa (kutegemea) Uwezo Wake (Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kuwa anatambua kwamba Allaah Anamuona (ayatendayo yote).

 

  1. Swawm pia inamzuia mtu na shaytwaan kwani hakika shaytwaan anatembea katika mwili wa binaadam kamba damu inavyotembea katika mishipa. Kwa hiyo Swawm inamvunja nguvu shaytwaan (na uchochezi wake), hivyo madhambi hupunguka.

 

  1. Swawm pia aghalbu humfanya mtu azidishe utiifu na utiifu ni katika sifa za taqwa.

 

  1. Swawm pia inamfanya tajiri anaposhikwa na njaa inayombidi imshike (kwa kuwa ni fardhi kwake, huwafikiria na) huwahurumia  masikini na mafuqara na hii ni miongoni mwa sifa za taqwa.  

 

Share