Shaykh Fawzaan: Sha'baan: Hakujasihi Chochote Kuhusu Niswf Sha'baan
Hakujasihi Chochote Kuhusu Niswf Sha'baan
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Hadiyth zilizopokelewa kuhusu fadhila za usiku wa Niswf Sha´baan ni Swahiyh?
JIBU:
Hapana. Si Swahiyh.
Hakukusihi kitu juu ya usiku wa Niswf Sha´baan wala siku ya Niswf Sha´baan.
Mtu asisimame usiku wa Niswf Sha´baan, bi maana mtu asikhusishe kusimama usiku.
Ama kuhusu yule aliyekuwa akidumu kwa kusimama tokea mwanzo asimame (kuswali) usiku wa Niswf Sha´baan kama siku zingine.
Ama kusema aikhusishe kwa kusimama (kuswali Swalaah ya usiku), hii ni bid´ah. Au akafunga siku ya kumi na tano ya mwezi wa Sha´baan, hii ni bid´ah. Isipokuwa yule aliyekutwa akifunga Swawm zake kama kwa mfano Swawm ya masiku meupe, afunge katika Sha´baan na siku zingine.