009 - At-Tawbah

 

 

التَّوْبَة

 

009-At-Tawbah

 

 

 009-At-Tawbah: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بَرَاءَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١﴾

1. (Hii ni) Kujitoa katika dhima (kunatangazwa) kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa wale mlioahidiana nao katika washirikina.[1]

 

 

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ اللَّـهَ مُخْزِي الْكَافِرِينَ﴿٢﴾

2. Basi vinjarini ardhini miezi minne, na jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Allaah (kumkwepa), na kwamba Allaah Ni Mwenye Kuwahizi makafiri.

 

 

 

 

وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّـهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُ ۚ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الَّذِينَ كَفَرُوا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣﴾

3. Na ni tangazo kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa watu siku ya Hajj kubwa, kwamba Allaah na Rasuli Wake hawana dhima yoyote kwa washirikina. Basi mkitubu, itakuwa kheri kwenu, na kama mtakengeuka, basi jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Allaah (kumkwepa). Na wabashirie wale waliokufuru watapata adhabu iumizayo. 

 

 

 

 

إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ثُمَّ لَمْ يَنقُصُوكُمْ شَيْئًا وَلَمْ يُظَاهِرُوا عَلَيْكُمْ أَحَدًا فَأَتِمُّوا إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٤﴾

4. Isipokuwa wale mlioahidiana nao katika washirikina, kisha hawakukupunguzieni chochote na wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi watimizieni ahadi yao mpaka muda wao (umalizike). Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.

 

 

 

فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٥﴾

5. Itapomalizika Miezi Mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni (mateka) na wahusuruni, na wakalieni katika kila kivuko cha njia zao. Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi waachieni huru njia zao. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ﴿٦﴾

6. Na ikiwa mmoja wa washirikina amekuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah (Qur-aan)[2] kisha mfikishe mahali pake pa amani. Hivyo kwa kuwa wao ni watu wasiojua.

 

 

 

كَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ اللَّـهِ وَعِندَ رَسُولِهِ إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ فَمَا اسْتَقَامُوا لَكُمْ فَاسْتَقِيمُوا لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٧﴾

7. Vipi iweko ahadi na washirikina mbele ya Allaah na mbele ya Rasuli Wake, isipokuwa wale mlioahidiana mbele ya Masjid Al-Haraam? Basi wakikunyookeeni (kwa uzuri), nanyi wanyookeeni. Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.

 

 

 

 

كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ لَا يَرْقُبُوا فِيكُمْ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ يُرْضُونَكُم بِأَفْوَاهِهِمْ وَتَأْبَىٰ قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨﴾

8. Vipi (mtashikamana na mkataba)? Hali wao wakikushindeni hawachungi kwenu udugu wa damu wala ahadi ya himaya? Wanakuridhisheni kwa midomo yao, na hali nyoyo zao zinakataa (makubaliano), na wengi wao ni mafasiki.

 

 

 

 

اشْتَرَوْا بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَصَدُّوا عَن سَبِيلِهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩﴾

9. Wamebadili Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo, na wakazuilia Njia Yake. Hakika ni maovu waliyokuwa wakitenda.

 

 

 

 

لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ﴿١٠﴾

10. Hawachungi kwa Muumini udugu wa damu wala ahadi ya himaya. Na hao ndio wenye kutaadi.

 

 

 

 

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ وَنُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿١١﴾

11. Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa Zakaah, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na Tunafasili waziwazi Aayaat (Ishara, Dalili, Hukmu) kwa watu wanaojua.

 

 

 

 

وَإِن نَّكَثُوا أَيْمَانَهُم مِّن بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُوا فِي دِينِكُمْ فَقَاتِلُوا أَئِمَّةَ الْكُفْرِ ۙ إِنَّهُمْ لَا أَيْمَانَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ﴿١٢﴾

12. Na wakivunja viapo vyao baada ya ahadi yao, na wakatukana Dini yenu, basi wapigeni vita viongozi wa ukafiri. Hakika viapo vyao havina maana. (Piganeni nao) ili wapate kukoma.

 

 

 

 

أَلَا تُقَاتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوا أَيْمَانَهُمْ وَهَمُّوا بِإِخْرَاجِ الرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ أَتَخْشَوْنَهُمْ ۚ فَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١٣﴾

13. Je, hamtopigana na watu waliovunja viapo vyao, na wakafanya hima kumtoa Rasuli, nao ndio waliokuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Allaah Anastahiki zaidi mumwogope ikiwa nyinyi ni Waumini (wa kweli).

 

 

 

 

قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ﴿١٤﴾

14. Piganeni nao, Allaah Atawaadhibu kwa mikono yenu, na Atawahizi na Atakunusuruni dhidi yao, na Atapozesha vifua vya kundi la Waumini.  

 

 

 

 

وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ ۗ وَيَتُوبُ اللَّـهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٥﴾

15. Na Ataondosha ghaidhi za nyoyo zao (Waumini). Na Allaah Anapokea tawbah kwa Amtakaye, na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

 

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٦﴾

16. Je, mmedhani kuwa mtaachwa tu nailhali Allaah bado Hajawadhihirisha wale waliofanya Jihaad miongoni mwenu, na hawakufanya yeyote kuwa rafiki mwandani isipokuwa Allaah na Rasuli Wake na Waumini (wenzao)? Na Allaah Ndiye Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.

 

 

 

 

مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا مَسَاجِدَ اللَّـهِ شَاهِدِينَ عَلَىٰ أَنفُسِهِم بِالْكُفْرِ ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ وَفِي النَّارِ هُمْ خَالِدُونَ﴿١٧﴾

17. Haiwi kwa washirikina kuamirisha Misikiti ya Allaah hali wanajishuhudia nafsi zao kwa ukafiri. Hao zimeporomoka amali zao, na katika moto wao watadumu.

 

 

 

إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّـهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَـٰئِكَ أَن يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ﴿١٨﴾

18. Hakika wanaoamirisha Misikiti ya Allaah ni wale wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah na hawamkhofu (yeyote) isipokuwa Allaah. Basi asaa hao wakawa miongoni mwa waliohidika.

 

 

 

 

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ لَا يَسْتَوُونَ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٩﴾

19. Je, mmefanya kunywesha maji Hujaji na kuamirisha Masjid Al-Haraam kama sawasawa na (amali za) anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akafanya Jihaad katika Njia ya Allaah? (Hapana!) Hawawi sawa mbele ya Allaah. Na Allaah Hawahidi watu madhalimu.[3]

 

 

 

 

الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾

20. Wale walioamini na wakahajiri na wakafanya Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao, wana daraja kubwa zaidi kwa Allaah. Na hao ndio waliofuzu.

 

 

 

يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ﴿٢١﴾

21. Rabb wao Anawabashiria Rahmah kutoka Kwake na Radhi na Jannaat (Pepo), watapata humo neema zenye kudumu.

 

 

 

 

خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٢٢﴾

22. Wadumu humo abadi. Hakika kwa Allaah kuna ujira mkubwa mno.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾

23. Enyi walioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu marafiki wandani ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya imaan. Na atakayewafanya marafiki wandani miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu.

 

 

 

 

قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٢٤﴾

24. Sema: Ikiwa baba zenu, na watoto wenu, na ndugu zenu, na wake (au waume) zenu, na jamaa zenu, na mali mliyoichuma, na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Rasuli Wake na kufanya Jihaad katika Njia Yake, basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu). Na Allaah Hawahidi watu mafasiki.

 

 

 

 

لَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ ۙ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ﴿٢٥﴾

25. Kwa yakini Allaah Amekunusuruni katika maeneo mengi (ya vita) na Siku ya (Vita vya) Hunayn[4] (pia) ulipokughururini wingi wenu (kwa kujigamba), lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki juu yenu juu ya upana wake, kisha mkageuka na kurudi nyuma kukimbia.

 

 

 

 

ثُمَّ أَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ﴿٢٦﴾

26. Kisha Allaah Akateremsha utulivu Wake kwa Rasuli Wake na kwa Waumini, na Akateremsha majeshi (ya Malaika) msiyoyaona, na Akawaadhibu wale waliokufuru. Na hivyo ndio jazaa ya makafiri.

 

 

 

ثُمَّ يَتُوبُ اللَّـهُ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٢٧﴾

27. Kisha Allaah Anapokea tawbah baada ya hapo kwa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٢٨﴾

28.                Enyi walioamini! Hakika washirikiana ni najisi (wachafu wa ‘aqiydah na vitendo), basi wasikaribie Masjid Al-Haraam baada ya mwaka wao huu. Na mkikhofu umasikini basi Allaah Atakutajirisheni kutokana na Fadhila Zake Akitaka. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

 

قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ ﴿٢٩﴾

29. Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, (piganeni nao) mpaka watoe jizyah (kodi) kwa khiyari, wakiwa wanyonge wadhalilifu.

 

 

 

 

وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٣٠﴾

30. Na Mayahudi wanasema: ‘Uzayr[5] ni mwana wa Allaah. Na Manaswara wanasema: Al-Masiyh (‘Iysaa) ni mwana wa Allaah. Hiyo ni kauli yao kwa midomo yao. Wanaiga kauli ya wale waliokufuru kabla. Allaah Awaangamize! Basi namna gani wanaghilibiwa wasione haki?

 

 

 

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣١﴾

31. Wamewafanya Ahbaar[6] (Mafuqahaa weledi) wao na Ruhbaan (Monaki)[7] wao kuwa ni miola badala ya Allaah, na (pia) Al-Masiyh mwana wa Maryam na hali hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Ilaah Mmoja Pekee.[8] Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye tu. Utakasifu ni Wake kutokana na yale yote wanayomshirikisha nayo.

 

 

 

 

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿٣٢﴾

32. Wanataka kuzima Nuru ya Allaah kwa vinywa vyao lakini Allaah Anakataa isipokuwa Atimize Nuru Yake, japo watakirihika makafiri.

 

 

 

 

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾

33. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.[9]

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾

34. Enyi walioamini! Hakika wengi katika Ahbaar (Mafuqahaa weledi wa Kiyahudi) na Ruhbaan (Monaki wa Kinaswara) wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia Njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika Njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo.[10]

 

 

 

يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ﴿٣٥﴾

35. Siku zitakapopashwa katika moto wa Jahannam, na kwazo vikachomwa moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao (wakiambiwa): Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika.

 

 

 

 

إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾

36. Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah ni kumi na mbili katika hukmu ya makadirio ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo iko Minne Mitukufu.[11] Hiyo ndiyo Dini iliyo nyoofu. Basi msijidhulumu humo nafsi zenu. Na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.

 

 

 

إِنَّمَا النَّسِيءُ زِيَادَةٌ فِي الْكُفْرِ ۖ يُضَلُّ بِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُحِلُّونَهُ عَامًا وَيُحَرِّمُونَهُ عَامًا لِّيُوَاطِئُوا عِدَّةَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ فَيُحِلُّوا مَا حَرَّمَ اللَّـهُ ۚ زُيِّنَ لَهُمْ سُوءُ أَعْمَالِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿٣٧﴾

37. Hakika kuakhirisha (au kuizuia Miezi Mitukufu) ni kuzidi katika kufuru. Hupotezwa kwayo wale waliokufuru, wanauhalalisha mwaka na wanauharamisha mwaka (mwingine) ili kuusawazisha na idadi ya (miezi) Aliyoitukuza Allaah. Basi huhalalisha Alivyoviharamisha Allaah. Wamepambiwa uovu wa amali zao. Na Allaah Hawahidi watu makafiri.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ ۚ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ ۚ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٣٨﴾

38. Enyi walioamini! Mna nini mnapoambiwa tokeni (mwende Jihaad)[12] katika Njia ya Allaah, mnajitia uzito katika ardhi. Je, mmeridhika na uhai wa dunia badala ya Aakhirah? Basi starehe za uhai wa dunia kulinganisha na Aakhirah ni chache.

 

 

 

 

إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٩﴾

39. Msipotoka kwenda Atakuadhibuni adhabu iumizayo, na Atabadilisha watu wasiokuwa nyinyi, na wala hamtomdhuru chochote. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

 

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ الَّذِينَ كَفَرُوا السُّفْلَىٰ ۗ وَكَلِمَةُ اللَّـهِ هِيَ الْعُلْيَا ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٤٠﴾

40. Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa mmoja katika wawili, walipokuwa katika pango, alipomwambia swahibu[13] yake: Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi. Basi Allaah Akamteremshia Utulivu Wake, na Akamsaidia kwa majeshi ambayo hamkuyaona, na Akajaalia neno la waliokufuru kuwa chini. Na Neno la Allaah ndilo lililo juu. Na Allaah Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٤١﴾

41. Tokeni mwende (ni sawa) mkiwa na hali ya wepesi na mkiwa na hali ya uzito na fanyeni Jihaad kwa mali zenu na nafsi zenu katika Njia ya Allaah. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.

 

 

 

 

لَوْ كَانَ عَرَضًا قَرِيبًا وَسَفَرًا قَاصِدًا لَّاتَّبَعُوكَ وَلَـٰكِن بَعُدَتْ عَلَيْهِمُ الشُّقَّةُ ۚ وَسَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَوِ اسْتَطَعْنَا لَخَرَجْنَا مَعَكُمْ يُهْلِكُونَ أَنفُسَهُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٤٢﴾

42. Kama ingelikuwa pato la karibu na safari nyepesi ya karibu, basi (wanafiki) wangelikufuata, lakini imekuwa ni ya masafa ya mbali kwao na ina mashaka. Na watakuapia kwa Jina la Allaah: Lau tungeliweza, bila shaka tungelitoka pamoja nanyi. Wanaangamiza nafsi zao na Allaah Anajua kwamba wao bila shaka ni waongo.

 

 

 

عَفَا اللَّـهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَتَعْلَمَ الْكَاذِبِينَ﴿٤٣﴾

43. Allaah Akusamehe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwa nini umewapa ruhusa? (Usingelifanya hivyo) mpaka wakubainikie wale waliosadikisha na uwajue waliokadhibisha.

 

 

 

 

لَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ﴿٤٤﴾

44. Hawakuombi ruhusa wale waliomwamini Allaah na Siku ya Mwisho wasifanye Jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na Allaah Anawajua vyema wenye taqwa.

 

 

 

 

إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ﴿٤٥﴾

45. Hakika wanaokuomba ruhusa ni wale ambao hawamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zina shaka, basi wao katika shaka zao wanasitasita.

 

 

 

 

وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ﴿٤٦﴾

46. Na ingelikuwa wametaka kutoka, wangeliandaa maandalizi yake, lakini Allaah Amekirihika kutoka kwao, basi Akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa.

 

 

 

 

لَوْ خَرَجُوا فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا خِلَالَكُمْ يَبْغُونَكُمُ الْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّاعُونَ لَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ﴿٤٧﴾

47. Lau wangelitoka nanyi, wasingelikuzidishieni isipokuwa machafuko (vurugu, rabsha) na wangeliharakia huku na huku baina yenu kukutieni fitnah, na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza kwa makini. Na Allaah Anawajua vyema madhalimu.

 

 

 

 

لَقَدِ ابْتَغَوُا الْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُوا لَكَ الْأُمُورَ حَتَّىٰ جَاءَ الْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ اللَّـهِ وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٤٨﴾

48. Walikwishataka kabla kukuleteeni fitnah, na wakakupindulia mambo mpaka ikaja haki na ikadhihirika Amri ya Allaah, nao wamekirihika.

 

 

 

 

وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ ائْذَن لِّي وَلَا تَفْتِنِّي ۚ أَلَا فِي الْفِتْنَةِ سَقَطُوا ۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌ بِالْكَافِرِينَ﴿٤٩﴾

49. Na miongoni mwao yuko anayesema: Niruhusu (nibaki) na wala usiniingize kwenye fitnah. Tanabahi! Wamekwishaanguka katika fitnah. Na hakika Jahannam imewazingira makafiri.

 

 

 

 

إِن تُصِبْكَ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ ۖ وَإِن تُصِبْكَ مُصِيبَةٌ يَقُولُوا قَدْ أَخَذْنَا أَمْرَنَا مِن قَبْلُ وَيَتَوَلَّوا وَّهُمْ فَرِحُونَ﴿٥٠﴾

50. Linapokusibu zuri lolote lile linawachukiza. Na unapokusibu msiba wowote ule, wanasema: Tumechukua tahadhari jambo letu tokea mwanzo, na wanageuka kwenda zao na huku wanafurahia.

 

 

 

 

قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿٥١﴾

51. Sema: Halitusibu (lolote) isipokuwa lile Alilotukidhia Allaah. Yeye ni Mawlaa[14] wetu. Basi kwa Allaah watawakali Waumini.  

 

 

 

 

قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ ۖ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَن يُصِيبَكُمُ اللَّـهُ بِعَذَابٍ مِّنْ عِندِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا ۖ فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ﴿٥٢﴾

52.  Sema: Je, mnalo la kungojea kututazamia isipokuwa mojawapo ya mazuri mawili? Na sisi tunangojea kukutazamieni kwamba Allaah Atakusibuni kwa adhabu kutoka Kwake au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeeni, nasi tuko pamoja nanyi tunangojea.

 

 

 

 

 قُلْ أَنفِقُوا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمْ ۖ إِنَّكُمْ كُنتُمْ قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٣﴾

53. Sema: Toeni (mali) kwa khiari au kutokupenda haitokubaliwa kwenu. Hakika nyinyi mmekuwa ni watu mafasiki.

 

 

 

 

وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَبِرَسُولِهِ وَلَا يَأْتُونَ الصَّلَاةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٥٤﴾

54. Na haikuwazuilia ikubaliwe michango yao isipokuwa kwa kuwa wao walimkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafiki katika Swalaah isipokuwa wao huwa katika hali ya uvivu, na wala hawatoi isipokuwa wakiwa wamekirihika.

 

 

 

 

فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٥٥﴾

55. Basi zisikubabaishe mali zao wala watoto wao. Hakika Allaah Anataka kuwaadhibu kwayo katika uhai wa dunia, na zitokelee mbali nafsi zao na huku wao wakiwa makafiri.

 

 

 

وَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنَّهُمْ لَمِنكُمْ وَمَا هُم مِّنكُمْ وَلَـٰكِنَّهُمْ قَوْمٌ يَفْرَقُونَ﴿٥٦﴾

56. Na wanaapa kwa Jina la Allaah kwamba wao ni miongoni mwenu. Na wala wao si katika nyinyi, lakini wao (wanafiki) ni watu wanaoogopa mno.

 

 

 

لَوْ يَجِدُونَ مَلْجَأً أَوْ مَغَارَاتٍ أَوْ مُدَّخَلًا لَّوَلَّوْا إِلَيْهِ وَهُمْ يَجْمَحُونَ﴿٥٧﴾

57. Lau wangelipata mahali pa kukimbilia, au mapango, au mahali finyu pa kuingia (na kujificha), basi wangelielekea huko wakikimbia mbio kali.

 

 

 

 

وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْهَا رَضُوا وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا مِنْهَا إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ﴿٥٨﴾

58. Na miongoni mwao wako wanaokukosoa katika (ugawaji wa) swadaqa. Wakipewa fungu wanaridhika, na wasipopewa fungu tahamaki wao wanaghadhibika.[15]

 

 

 

 

وَلَوْ أَنَّهُمْ رَضُوا مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ سَيُؤْتِينَا اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَرَسُولُهُ إِنَّا إِلَى اللَّـهِ رَاغِبُونَ﴿٥٩﴾

59. Na lau wangeliridhiya yale Aliyowapa Allaah na Rasuli Wake, na wakasema: Anatutosheleza Allaah, karibuni Allaah Atatupa katika Fadhila Zake na Rasuli Wake (pia), hakika sisi kwa Allaah tuna raghba.

 

 

 

إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٦٠﴾

60. Hakika Zakaah ni kwa ajili ya mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (katika Uislamu) na kuwakomboa mateka, na wenye deni, na katika Njia ya Allaah, na msafiri (aliyeharibikiwa). Ni faradhi itokayo kwa Allaah. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.[16]

 

 

 

وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ ۚ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ ۚ وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦١﴾

61. Na miongoni mwao wako wale wanaomuudhi Nabiy, na wanasema: Yeye ni mtegaji sikio tu.[17] Sema: Sikio la kheri kwenu. Anamwamini Allaah na anawasadiki Waumini, na ni Rahmah kwa wale walioamini miongoni mwenu. Na wale wanaomuudhi Rasuli wa Allaah watapata adhabu iumizayo.  

 

 

 

يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ لِيُرْضُوكُمْ وَاللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَحَقُّ أَن يُرْضُوهُ إِن كَانُوا مُؤْمِنِينَ﴿٦٢﴾

62. Wanakuapieni kwa Jina la Allaah ili wakuridhisheni, hali ya kuwa Allaah na Rasuli Wake ndio wanaostahiki zaidi kuridhishwa lau kama wao ni Waumini.

 

 

 

 

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّهُ مَن يُحَادِدِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَأَنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدًا فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ الْخِزْيُ الْعَظِيمُ﴿٦٣﴾

63. Je, hawajui kwamba yeyote mwenye kumpinga Allaah na Rasuli Wake basi hakika atapata Jahannam adumu humo. Hiyo ni hizaaya kubwa mno.

 

 

 

 

يَحْذَرُ الْمُنَافِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ سُورَةٌ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلِ اسْتَهْزِئُوا إِنَّ اللَّـهَ مُخْرِجٌ مَّا تَحْذَرُونَ﴿٦٤﴾

64. Wanafiki wanatahadhari isije kuteremshwa Suwrah itakayowajulisha yaliyomo nyoyoni mwao. Sema: Fanyeni istihzai, hakika Allaah Atayatoa yale mnayotahadhari nayo.  

 

 

 

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾

65. Na ukiwauliza, bila shaka watasema: Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza. Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?

 

 

 

لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚ إِن نَّعْفُ عَن طَائِفَةٍ مِّنكُمْ نُعَذِّبْ طَائِفَةً بِأَنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٦٦﴾

66. Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.[18] Tukilisamehe kundi miongoni mwenu, Tutaliadhibu kundi (jingine), kwa kuwa wao walikuwa wahalifu.

 

 

 

الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ بَعْضُهُم مِّن بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ ۚ نَسُوا اللَّـهَ فَنَسِيَهُمْ ۗ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿٦٧﴾

67. Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake wote ni washirika wamoja, wanaamrisha munkari na wanakataza mema na hufumba mikono yao. Wamemsahau Allaah, basi Naye Amewasahau. Hakika wanafiki wao ndio mafasiki.

 

 

 

وَعَدَ اللَّـهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ هِيَ حَسْبُهُمْ ۚ وَلَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٦٨﴾

68. Allaah Amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri moto wa Jahannam, wadumu humo, inawatosheleza hiyo (adhabu)! Na Allaah Amewalaani, na watapata adhabu ya kudumu.

 

 

 

كَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا فَاسْتَمْتَعُوا بِخَلَاقِهِمْ فَاسْتَمْتَعْتُم بِخَلَاقِكُمْ كَمَا اسْتَمْتَعَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَاقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَالَّذِي خَاضُوا ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٦٩﴾

69. Ni kama wale wa kabla yenu, walikuwa wana nguvu zaidi kuliko nyinyi, na wana mali na watoto wengi zaidi. Basi walistarehe kwa fungu lao nanyi mnastarehe kwa fungu lenu, kama walivyostarehe kwa fungu lao wale wa kabla yenu, na mkatumbukia katika ubatilifu na ukanushaji kama walivyotumbukia. Hao zimeporomoka amali zao duniani na Aakhirah. Na hao ndio waliokhasirika.

 

 

 

أَلَمْ يَأْتِهِمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَقَوْمِ إِبْرَاهِيمَ وَأَصْحَابِ مَدْيَنَ وَالْمُؤْتَفِكَاتِ ۚ أَتَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٧٠﴾

70. Je, haikuwafikia khabari ya wale wa kabla yao; kaumu ya Nuwh, na ‘Aad na Thamuwd, na kaumu ya Ibraahiym, na watu ya Madyan, na miji iliyopinduliwa juu chini? Rusuli wao waliwafikia kwa hoja bayana. Na Allaah Hakuwa Mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.

 

 

 

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٧١﴾

71. Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki wandani.[19] Wanaamrisha mema na wanakataza munkari[20] na wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah na wanamtii Allaah na Rasuli Wake. Hao Allaah Atawarehemu. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

وَعَدَ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٧٢﴾

72. Allaah Amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo, na makazi mazuri katika Jannaat za kudumu milele. Na Radhi kutoka kwa Allaah ndio kubwa zaidi. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.

 

 

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٧٣﴾

73.  Ee Nabiy! Fanya Jihaad dhidi ya makafiri na wanafiki na kuwa mkali kwao. Na makazi yao ni Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kuishia!  

 

 

 

 

يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ مَا قَالُوا وَلَقَدْ قَالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَكَفَرُوا بَعْدَ إِسْلَامِهِمْ وَهَمُّوا بِمَا لَمْ يَنَالُوا ۚ وَمَا نَقَمُوا إِلَّا أَنْ أَغْنَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ مِن فَضْلِهِ ۚ فَإِن يَتُوبُوا يَكُ خَيْرًا لَّهُمْ ۖ وَإِن يَتَوَلَّوْا يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ عَذَابًا أَلِيمًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَمَا لَهُمْ فِي الْأَرْضِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٧٤﴾

74. Wanaapa kwa Jina la Allaah kuwa hawakusema ilhali wamekwishasema neno la kufuru, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao. Na wakaazimia yale ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia isipokuwa kwa kuwa Allaah na Rasuli Wake Amewatajirisha kwa Fadhila Zake. Basi wakitubia, itakuwa ni kheri kwao. Na wakikengeuka, Allaah Atawaadhibu adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na hawatopata katika ardhi rafiki mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.

 

 

 

وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿٧٥﴾

75.  Na miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah (kuwa): Akitupa katika Fadhila Zake, bila shaka tutatoa swadaqa, na bila shaka tutakuwa miongoni mwa wema.[21]

 

 

 

فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٧٦﴾

76. Alipowapa katika Fadhila Zake, walizifanyia ubakhili, na wakakengeuka huku wakipuuza.

 

 

 

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ﴿٧٧﴾

77. Basi Akawapatilizia unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakayokutana Naye kwa sababu ya kumkhalifu kwao Allaah yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kukadhibisha kwao. 

 

 

 

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ﴿٧٨﴾

78. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua siri zao na minong’ono yao, na kwamba Allaah ni Mjuzi wa Ghaibu?

 

 

 

الَّذِينَ يَلْمِزُونَ الْمُطَّوِّعِينَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ فِي الصَّدَقَاتِ وَالَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهْدَهُمْ فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْ ۙ سَخِرَ اللَّـهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٩﴾

79. Wale (wanafiki) wanaowafanyia tashtiti Waumini wenye kujitolea kwa khiari katika kutoa swadaqa na wale wasiopata (cha kutoa) isipokuwa kadri ya juhudi zao, basi wanawafanyia dhihaka, Allaah Analipiza dhihaka zao na watapata adhabu iumizayo.[22]

 

 

 

اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٨٠﴾

80. Waombee maghfirah (ee, Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), au usiwaombee maghfirah, hata ukiwaombea maghfirah mara sabini, Allaah Hatowaghufuria. Hivyo kwa kuwa wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake. Na Allaah Hawahidi watu mafasiki.

 

 

 

فَرِحَ الْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَافَ رَسُولِ اللَّـهِ وَكَرِهُوا أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَالُوا لَا تَنفِرُوا فِي الْحَرِّ ۗ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا ۚ لَّوْ كَانُوا يَفْقَهُونَ﴿٨١﴾

81. Waliobaki nyuma walifurahi kwa kule kukaa kwao (wasiende vitani) baada ya Rasuli wa Allaah (kutoka), na walikirihika kufanya Jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika Njia ya Allaah na wakasema: Msitoke kwenda katika joto. Sema: Moto wa Jahannam ni mkali zaidi lau wangelifahamu.

 

 

 

فَلْيَضْحَكُوا قَلِيلًا وَلْيَبْكُوا كَثِيرًا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٢﴾

82. Basi na wacheke kidogo (duniani), na watalia sana (Aakhirah) ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

 

 

 

فَإِن رَّجَعَكَ اللَّـهُ إِلَىٰ طَائِفَةٍ مِّنْهُمْ فَاسْتَأْذَنُو كَ لِلْخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخْرُجُوا مَعِيَ أَبَدًا وَلَن تُقَاتِلُوا مَعِيَ عَدُوًّا ۖ إِنَّكُمْ رَضِيتُم بِالْقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَاقْعُدُوا مَعَ الْخَالِفِينَ﴿٨٣﴾

83. Basi Allaah Akikurejesha kwenye kundi moja miongoni mwao na wakakutaka idhini ya kutoka, sema: Hamtotoka pamoja nami abadani, na wala hamtopigana na maadui pamoja nami. Nyinyi mliridhika kubakia nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao wanaobakia nyuma.

 

 

 

وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِ ۖ إِنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَمَاتُوا وَهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨٤﴾

84. Na wala usimswalie yeyote abadani miongoni mwao akifa, na wala usisimame kaburini kwake. Hakika wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wakafa hali wao ni mafasiki.[23]

 

 

 

 

وَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَأَوْلَادُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٨٥﴾

85. Na wala zisikubabaishe mali zao na watoto wao. Hakika Allaah Anataka Awaadhibu kwayo duniani, na zitokelee mbali nafsi zao na huku wao wakiwa ni makafiri.

 

 

 

وَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ أَنْ آمِنُوا بِاللَّـهِ وَجَاهِدُوا مَعَ رَسُولِهِ اسْتَأْذَنَكَ أُولُو الطَّوْلِ مِنْهُمْ وَقَالُوا ذَرْنَا نَكُن مَّعَ الْقَاعِدِينَ﴿٨٦﴾

86. Na inapoteremshwa Suwrah kwamba muaminini Allaah, na fanyeni Jihaad pamoja na Rasuli Wake, wanakuomba idhini wale (wanafiki) wenye utajiri miongoni mwao, na husema: Tuache tubakie pamoja na wanaokaa nyuma.

 

 

 

رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ﴿٨٧﴾

87. Wameridhika kuwa pamoja na waliobakia nyuma, na zikapigwa chapa nyoyo zao, basi wao hawafahamu.

 

 

 

لَـٰكِنِ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ جَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْخَيْرَاتُ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٨٨﴾

88. Lakini Rasuli na walioamini pamoja naye, wamefanya Jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na hao watapata kheri nyingi. Na hao ndio wenye kufaulu.

 

 

 

أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٨٩﴾

89. Allaah Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.

 

 

 

 

وَجَاءَ الْمُعَذِّرُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ الَّذِينَ كَذَبُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ سَيُصِيبُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٩٠﴾

90. Na wakaja wenye kutoa udhuru katika Mabedui ili waruhusiwe (wasiende vitani), na wakabakia (majumbani) wale waliomwambia uwongo Allaah na Rasuli Wake. Itawasibu waliokufuru katika wao adhabu iumizayo.

 

 

 

لَّيْسَ عَلَى الضُّعَفَاءِ وَلَا عَلَى الْمَرْضَىٰ وَلَا عَلَى الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُوا لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ مَا عَلَى الْمُحْسِنِينَ مِن سَبِيلٍ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩١﴾

91. Hapana lawama juu ya wale walio dhaifu na wala juu ya walio wagonjwa, na wala juu ya wale wasiopata cha kuchangia (katika Jihaad), madamu wanamsafia niya Allaah na Rasuli Wake. Hapana njia ya kuwalaumu wafanyao ihsaan. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَلَا عَلَى الَّذِينَ إِذَا مَا أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَا أَجِدُ مَا أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوا وَّأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا مَا يُنفِقُونَ﴿٩٢﴾

92. Na wala (hakuna lawama) juu ya wale ambao wanapokujia ili uwapatie kipando, ukasema: Sijapata cha kukupandisheni, wanaondoka na huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa cha kuchangia.

 

 

 

إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَسْتَأْذِنُونَكَ وَهُمْ أَغْنِيَاءُ ۚ رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٩٣﴾

93. Hakika (ipo) sababu ya kulaumu kwa wale wanaokuomba idhini na hali wao ni matajiri. Wameridhia kuwa pamoja na waliobakia nyuma, na Allaah Akapiga chapa juu ya nyoyo zao, basi wao hawajui. 

 

 

 

يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ ۚ قُل لَّا تَعْتَذِرُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا اللَّـهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ ۚ وَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٤﴾

94. Watakutoleeni udhuru mtakaporejea kwao. Sema: Msitoe udhuru, hatutokuaminini! Allaah Amekwishatujulisha khabari zenu. Na hivi karibuni Allaah na Rasuli Wake wataona amali zenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

 

سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾

95. Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika wao ni najsi (wachafu wa aqiydah na niya), na makazi yao ni Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.[24]

 

 

 

يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾

96. Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki.

 

 

 

الْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٩٧﴾

97. Mabedui wamezidi zaidi kufuru na unafiki, na wameelekea zaidi kwamba wasijue mipaka ya (sharia) Alizoteremsha Allaah juu ya Rasuli Wake. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٩٨﴾

98. Na katika Mabedui, wako wanaochukulia yale wanayoyatoa kuwa ni gharama tupu, na wanakungojeleeni migeuko ya misiba. Misiba mibaya itawafika wao! Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَاتٍ عِندَ اللَّـهِ وَصَلَوَاتِ الرَّسُولِ ۚ أَلَا إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ ۚ سَيُدْخِلُهُمُ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩٩﴾

99. Na katika Mabedui, wako wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wanachukulia yale wanayoyatoa kuwa ni njia ya makurubisho mbele ya Allaah, na kupata duaa za Rasuli. Tanabahi! Hakika hiyo ni njia ya kikurubisho kwao. Allaah Atawaingiza katika Rahmah Yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾

100. Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiruwn na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan[25], Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.

 

 

 

وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ ۖ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ﴿١٠١﴾

101. Na katika Mabedui wanaokuzungukeni wako wanafiki. Na katika watu wa Madiynah (pia) wapo waliobobea katika unafiki. Huwajui (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Sisi Tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili kisha watarudishwa katika adhabu kubwa mno.

 

 

 

وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّـهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٠٢﴾

102. Na wengineo wamekiri madhambi yao, wamechanganya amali njema na nyinginezo ovu, asaa Allaah Atapokea tawbah zao. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٠٣﴾

103. Chukua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mali zao swadaqa, uwatwaharishe na uwatakase kwazo, na waombee duaa (na maghfirah). Hakika duaa yako ni utulivu kwao. Allaah Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١٠٤﴾

104. Je, hawajui kwamba Allaah Ndiye Anayekubali tawbah ya Waja Wake, na Anapokea swadaqa, na kwamba Allaah Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿١٠٥﴾

105. Na sema: Fanyeni (mtakavyo). Allaah Ataona amali zenu na Rasuli Wake na Waumini (pia wataona). Na mtarudishwa kwa Mjuzi wa Ghaibu na dhahiri, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.

 

 

 

وَآخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّـهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٠٦﴾

106. Na wengineo wamengojeshewa Amri ya Allaah. Ama Atawaadhibu au Atawapokelea tawbah zao. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿١٠٧﴾

107. Na wale waliojenga Msikiti kwa ajili ya kuleta madhara,[26] na kufuru, na kufarikisha baina ya Waumini, na kuwa ngome kwa waliompiga vita Allaah na Rasuli Wake hapo kabla. Na bila shaka wanaapa: Hatukukusudia ila jambo zuri. Na Allaah Anashuhudia kwamba hakika wao ni waongo.

 

 

 

 

لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا ۚ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ﴿١٠٨﴾

108. Usisimame humo abadani! Bila shaka Msikiti ulioasisiwa juu ya taqwa[27] tokea siku ya kwanza unastahiki zaidi usimame humo. Humo mna watu wanaopenda kujitwaharisha. Na Allaah Anapenda wanaojitwaharisha.

 

 

 

أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٩﴾

109. Je, yule aliyeasisi jengo lake juu ya taqwa ya Allaah na Radhi (Zake), ni bora au yule aliyeasisi jengo lake juu ya ukingo wa bonde lenye ufa na lenye kuburugunyika na likaporomoka pamoja naye katika moto wa Jahannam?  Na Allaah Hawahidi watu madhalimu.

                                               

 

 

لَا يَزَالُ بُنْيَانُهُمُ الَّذِي بَنَوْا رِيبَةً فِي قُلُوبِهِمْ إِلَّا أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١١٠﴾

110. Halitoacha jengo lao hilo walilolijenga kuwa ni sababu ya kuwatia shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao zikatike katike. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١١١﴾

111. Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Jannah. Wanapigana katika Njia ya Allaah, wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi ya haki Aliyojiwekea katika Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Na nani atimizae zaidi ahadi yake kuliko Allaah?  Basi furahieni kwa biashara yenu mliyofungamana Naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa. 

 

 

 

التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١١٢﴾

112. (Waumini hao ni) wanaotubia, wanaodumisha ibaada (kwa ikhlaasw na utiifu), wanaomhimidi (Allaah), wenye kusafiri kwa ajili ya ibaada (au wenye kufunga Swawm[28], wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza munkari, na wanaohifadhi Mipaka ya Allaah. Na wabashirie Waumini.

 

 

 

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾

113. Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa motoni.[29]

 

 

 

وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾

114. Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu.

 

 

 

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١٥﴾

115. Na haiwi kwa Allaah Awapotoze watu baada ya kuwa Amewahidi mpaka Awabainishie ya kujikinga nayo. Hakika Allaah kwa kila kitu Ni Mjuzi.

 

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿١١٦﴾

116. Hakika Ni Wake Allaah ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na Anafisha. Nanyi hamna pasi na Allaah rafiki mlinzi wala mwenye kunusuru.

 

 

 

لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾

117. Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhaajiruwn na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao kukurubia kuelemea mbali na haki, kisha Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao Ni Mwenye huruma mno, Mwenye Kurehemu.[30]

 

 

 

وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾

118. Na (akapokea tawbah) ya wale watatu[31] waliobaki nyuma (wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa kuelekea Kwake, kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾

119. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli.

 

 

 

مَا كَانَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا عَن رَّسُولِ اللَّـهِ وَلَا يَرْغَبُوا بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴿١٢٠﴾

120. Haikuwapasa watu wa Madiynah na Mabedui walio pembezoni mwao kwamba wabakie nyuma wasitoke na Rasuli wa Allaah, wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hilo ni kwa kuwa hakiwasibu wao kiu wala machofu, wala njaa kali katika Njia ya Allaah, na wala hawakanyagi ardhi yoyote inayowaghadhibisha makafiri (wao kuikanyaga), na wala hawawasibu maadui msiba wowote ila wanaandikiwa kwayo amali njema. Hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.

 

 

 

وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢١﴾

121. Na wala hawatoi mchango wowote mdogo au mkubwa na wala hawavuki bonde lolote isipokuwa huandikiwa (ujira), ili Allaah Awalipe mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wanayatenda.

 

 

 

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ﴿١٢٢﴾

122.  Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja (kupigana Jihaad). Basi kwa nini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi (moja tu) wajifunze vyema Dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kujihadharisha.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿١٢٣﴾

123. Enyi walioamini! Piganeni Jihaad na wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.

 

 

 

وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ﴿١٢٤﴾

124. Na inapoteremshwa Suwrah, basi miongoni mwao wako wanaosema: Nani kati yenu imemzidishia (Suwrah) hii imaan? Ama wale walioamini huwazidishia imaan nao wanafurahia.[32] 

 

 

 

وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ﴿١٢٥﴾

125. Na ama wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, huwazidishia rijs (unafiki, shaka n.k.) juu ya rijs yao, na wakafa hali wao ni makafiri.

 

 

 

أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿١٢٦﴾

126. Je, hawaoni kwamba wao wanatahiniwa kila mwaka mara moja au mara mbili, kisha hawatubii na wala wao hawakumbuki?

 

 

 

وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ انصَرَفُوا ۚ صَرَفَ اللَّـهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿١٢٧﴾

127. Na inapoteremshwa Suwrah wanatazamana wenyewe kwa wenyewe (wakisema:) Je, kuna mmoja yeyote anayekuoneni? Kisha wanageuka kuondokea mbali. Allaah Amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.

 

 

 

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾

128. Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rehma.[33]

 

 

 

فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ﴿١٢٩﴾

129. Na wakikengeuka, basi sema: Amenitosheleza Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Kwake nimetawakali. Naye Ni Rabb wa ‘Arsh Adhimu.[34]

 

 

 

 

 

 

[1] Suwrah Pekee Isiyoanza kwa بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم  (Kwa Jina la Allaah Mwingi wa Rahmah Mwenye Kurehemu):

 

Kauli Za ‘Ulamaa:

 

(i) Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله):

 

Suwrah At-Tawbah haikuanzwa na Basmalah kwa sababu hivyo ndivyo ilivyokuja, na kwamba lau Basmalah ingekuwa ina nafasi ndani yake, ingelihifadhiwa na ingekuwepo kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

“Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka Ndio Wenye Kuihifadhi.” [Al-Hijr (15:9)]

 

[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb Shariytw (103) - Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله)]

 

(iii) Shaykh Swaalih Bin Fawzaan (حفظه الله):

 

Kwanza: Suwrat Al-Anfaal inaendelezwa na Suwrat At-Tawbah, kwa hivyo haikuja mwanzoni mwake kwa

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

Pili: Suwrat At-Tawbah haikuanzwa na

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

 

kwa sababu ni Suwrah iliyotajwa ndani yake Jihaad na makafiri, na pia kuna maonyo, makemeo na vitisho vikali kwa wanafiki, na kufichua fedheha, kashfa na khiyana zao. Kwa hayo, haikupasa kuanziwa kwa

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

kwani humu mna Rehma ambayo haiwafikiani na hayo yaliyotajwa kuhusu wanafiki na makafiri na sifa zao. Kwa hivyo haikuanziwa kwa

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

 

 [Shaykh Swaalih Bin Fawzaan Al-Fawzaan]

 

(iii) Imaam Ibn Baaz (رحمه الله):

 

Sababu ya kutokuweko  

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

katika Suwrat At-Tawbah ni kwamba ‘Uthmaan (رضي الله عنه) aliulizwa kuhusu hili akasema: Suwrat Al-Anfaal na Suwrat Al-Baraa (At-Tawbah) zinakaribiana kimaana, kwa hivyo haikuteremshwa baina yake

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

Hivyo ‘Uthmaan na Swahaba (رضي الله عنهم) walidhania kwamba ni Suwrah moja kwa kuwa zimewekwa pamoja na hakuna Aayah baina yake ya

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

na pia hakuna dalili inayoonyesha kuwa ni Suwrah mbili. Swahaba walikuwa makini, na wakazifanya ziwe karibu pamoja kwa sababu hawakuhifadhi Uteremsho wa

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيْمِ

baina ya Suwrah hizi mbili. Na rai hii ndio iliyo mashuhuri kama ilivyopokelewa na ‘Ulamaa kutoka kwa ‘Uthmaan pale alipokusanya Mswahafu katika ukhalifa wake.  [Nuwr ‘Alad-Darb - Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz]

 

[2] Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah Hayakuumbwa:

 

Qur-aan ni Maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) kwa herufi zake na maana zake. Allaah (عزّ وجلّ) Ameizungumzia kwa namna Aliyoitaka. Hivyo, nasi tunamueleza Allaah kwa Sifa Yake ya Kuzungumza. Na Al-Kalaam (Maneno) ni kutoka kwenye Sifa za Allaah Ambazo ni Swifaat Fi’liyyah (Sifa za vitendo). Na hatuulizi kayfiyyah (namna) yake, au hatuleti Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake, au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, au kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah). 

 

‘Ulamaa wameelezea mengi kuhusu kauli hiyo ya Allaah (عزّ وجلّ). Miongoni mwao ni Imaam Al-Qurtwubiy (رحمه الله) ambaye amesema kuhusiana na Aayah hii: “Allaah (سبحانه وتعالى) Akadalilisha kwamba Maneno Yake yanasikilizwa pindi msomaji wa Qur-aan anapoyasoma.  Na jambo hili linawafikiana na Waislamu kuwa msomaji Qur-aan akisoma Suwratul-Faatihah au Suwrah yoyote, wanasema tumeyasikia Maneno ya Allaah.”

 

Pia, Imaam ‘Abdur-Rahmaan Naaswir As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: “Katika Aayah hii, kuna hoja ya wazi kuhusiana na mafundisho ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa'ah wanaosema kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah Ambayo hayakuumbwa, kwa sababu Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Anayeizungumza, na Akaihusisha Kwake Mwenyewe kuongezea sifa ya kielelezo chake. Na hii inabatilisha madhehebu ya Mu-‘utazilah na wengineo wanaosema kwamba Qur-aan imeumbwa. Ni dalili ngapi zipo zinazothibitisha ubatilifu wa msemo huu? (Bila shaka ni nyingi), lakini hapa si mahala pa kuzitaja au kuzielezea. [Tafsiyr As-Sa’adiy] 

 

Rejea pia Suwrat An-Nisaa (4:164), Aayah ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema kuwa Alimsemesha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kwa Maneno ya uhakika, na kuna maelezo katika tanbihi ya Aayah hiyo.

 

[4] Ghazwat Hunayn:

 

Hunayn ni bonde baina ya Twaaif na Makkah.

 

Vita vya Hunayn vilitokea mwezi wa Shawwaal mwaka wa 8 Hijriyyah.

 

Baada ya Fat-h Makkah, Uislamu ulisambaa na yakabakia makabila machache ambayo watu wake hawakuingia Uislamu. Miongoni mwa makabila hayo ni kabila la Thaqiyb na Hawaazin ambao waliendelea na ushirikina. Wakachukia wito wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakampinga. Basi wakapanga vita kupigana na Waislamu. Na ikawa mara ya mwanzo Waislamu kupigana vita kwa idadi kubwa zaidi kuliko idadi ya makafiri. Hakupata Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka na jeshi kubwa kuliko la siku hiyo, alitoka na watu elfu kumi na mbili, hata Waislamu wakawa wanasema: “Hatutoshindwa leo kwa tuko wengi.” Ndio Anataja haya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah hii tukufu kuwa Waislamu walijigamba kwa kuwa walijiamini na wakadhani kuwa hawatashindwa. Walijisahau hali yao ilivyokuwa katika Vita vya Badr ambavyo    Allaah Aliwapa ushindi juu ya uchache wao. Wakawa hawakujitayarisha kuingia vitani kwa silaha kwa kuamini wingi wao.

 

Wakatekwa na makafiri kwa mishale hapo basi wakaanza kumahanika. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukata tamaa na Rehma ya Allaah akawa anawatuliza Waislamu kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atawapa ushindi. Wakapata nguvu kwa kutiwa nguvu na maneno ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Allaah Akawateremshia Utulivu Wake. Wakapigana na makabila hayo ya Thaqiyf na Hawaazin mpaka wakashinda. Makafiri hao wakakimbia na wakaacha ngawira tele za farasi, mbuzi na mateka ya wanawake. 

 

Miongoni mwa Hadiyth zinzoaelezea tukio la Vita hivi vitukufu ni zifuatazo:

 

حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ، حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ،‏.‏ قَالَ رَجُلٌ لِلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ ـ رضى الله عنهما ـ أَفَرَرْتُمْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ حُنَيْنٍ قَالَ لَكِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لَمْ يَفِرَّ، إِنَّ هَوَازِنَ كَانُوا قَوْمًا رُمَاةً، وَإِنَّا لَمَّا لَقِينَاهُمْ حَمَلْنَا عَلَيْهِمْ فَانْهَزَمُوا، فَأَقْبَلَ الْمُسْلِمُونَ عَلَى الْغَنَائِمِ وَاسْتَقْبَلُونَا بِالسِّهَامِ، فَأَمَّا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَلَمْ يَفِرَّ، فَلَقَدْ رَأَيْتُهُ وَإِنَّهُ لَعَلَى بَغْلَتِهِ الْبَيْضَاءِ وَإِنَّ أَبَا سُفْيَانَ آخِذٌ بِلِجَامِهَا، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ "‏ أَنَا النَّبِيُّ لاَ كَذِبْ أَنَا ابْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبْ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abuu Is-haaq kuwa mtu mmoja alimuuliza Al-Baraa Bin ‘Aazib (رضي الله عنهما): Je, mlikimbia mkamuacha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Hunayn? Al-Baraa akajibu: Lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukimbia. Hakika Hawaazin walikuwa ni watu hodari sana kurusha mishale. Tulipopambana nao, tuliwashambulia, nao wakakimbia. Pindi Waislamu walipoanza kukusanya ngawira, wakapambana nasi kwa mishale, lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukimbia, kwani   nilimuona juu ya nyumbu wake mweupe, ilhali Abuu Sufyaan ameshika hatamu, huku Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Mimi ni Nabiy wa kweli, mimi ni mtoto wa ‘Abdul-Mutw-twalib.” [Al-Bukhaariy Kitaabu Cha Jihaad (56)]

 

 

عن أبي الفضل العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قال : شَهِدْتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَومَ حُنَيْن ، فَلَزِمْتُ أنا وأبو سُفْيَانَ بن الحارثِ بن عبد المطلب رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَلَمْ نُفَارِقْهُ ، وَرسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، عَلَى بَغْلَةٍ لَهُ بَيْضَاءَ ، فَلَمَّا التَقَى المُسْلِمُونَ وَالمُشْرِكُونَ ، وَلَّى المُسْلِمُونَ مُدْبِريِنَ ، فَطَفِقَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يَرْكُضُ بَغْلَتَهُ قِبلَ الكُفَّارِ ، وأنا آخِذٌ بِلِجَامِ بَغْلَةِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، أكُفُّهَا إرَادَةَ أنْ لاَ تُسْرِعَ ، وأبُو سُفْيَانَ آخِذٌ بِرِكَابِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فقالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أيْ عَبَّاسُ ، نَادِ أصْحَابَ السَّمُرَةِ )) . قالَ العَبَّاسُ - وَكَانَ رَجُلاً صَيِّتاً - فَقُلْتُ بِأَعْلَى صَوْتِي : أيْنَ أصْحَابُ السَّمُرَةِ ، فَوَاللهِ لَكَأنَّ عَطْفَتَهُمْ حِينَ سَمِعُوا صَوْتِي عَطْفَةُ البَقَرِ عَلَى أَوْلاَدِهَا ، فقالوا : يَا لَبَّيْكَ يَا لَبَّيْكَ ، فَاقْتَتَلُوا هُمْ وَالكُفَّارُ ، وَالدَّعْوَةُ في الأنْصَارِ يَقُولُونَ : يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ، يَا مَعْشَرَ الأنْصَارِ ، ثُمَّ قَصُرَتِ الدَّعْوَةُ عَلَى بَنِي الحَارِثِ بْنِ الخَزْرَجِ ، فَنَظَرَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ عَلَى بَغْلَتِهِ كَالمُتَطَاوِلِ عَلَيْهَا إلَى قِتَالِهِمْ ، فَقَالَ : (( هَذَا حِينَ حَمِيَ الوَطِيسُ )) ، ثُمَّ أَخَذَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، حَصَيَاتٍ فَرَمَى بِهِنَّ وُجُوهَ الكُفَّارِ ، ثُمَّ قَالَ : (( انْهَزَمُوا وَرَبِّ مُحَمَّدٍ )) ، فَذَهَبْتُ أنْظُرُ فَإذَا القِتَالُ عَلَى هَيْئَتِهِ فِيما أرَى ، فَواللهِ مَا هُوَ إلاَّ أنْ رَمَاهُمْ بِحَصَيَاتِهِ ، فَمَا زِلْتُ أرَى حَدَّهُمْ كَلِيلاً وَأَمْرَهُمْ مُدْبِراً . رواه مسلم .

Amesema Abul-Faadhwl Al-'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه): Nilishuhudia pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Vita vya Hunayn. Mimi na Abu Sufyaan bin Al-Haarith bin 'Abdil-Muttwalib tulijilazimisha kuwa karibu na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wala hatukuachana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyekuwa amempanda nyumbu mweupe. Walipokutana Waislamu na mushirikina katika Vita hivyo, Waislamu waligeuza migongo yao na kuanza kukimbia. Hata hivyo, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aalimtia chonjo nyumbu wake kuwakabili makafiri, nami nilikuwa nimeshika hatamu ya nyumbu wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili kumzuia asiende kwa kasi mno. Na Abu Sufyaan alikuwa amezishikilia *zikuku* (za kupandia) za mnyama huyo wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee 'Abbaas! Waite Swahaba wa Samurah (wale waliokuwepo katika Bay’atur-Ridhwaan (Ahadi ya utiifu ya Radhi).” Anasema 'Abbaas (رضي الله عنهما): Mimi nilikuwa na sauti kubwa. Nikawaita kwa sauti yangu ya juu kabisa: Wako wapi Swahaba wa Samurah? Naapa kwa Allaah! Walipoisikia sauti walikimbia haraka haraka kuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama ng'ombe kuwakimbilia ndama wake. wakasema: Tuko hapa, tuko hapa! Hapo hapo wakaanza kupigana na makafiri. Kwa wakati huo viongozi wa Answaar wakaanza kuita: Enyi kongamano la Answaar! Kisha wakaita Bani Al-Haarith ibn Al-Khazraj. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinyanyua kichwa chake kuangalia vita vinavyoendelea akiwa juu ya nyumbu wake. Akasema: "Hii ni pindi vita vinapopamba moto na kufikia kilele." Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alichukua changarawe na kuvirusha kwenye nyuso za makafiri, kisha akasema: "Kwa Rabb wa Muhammad, wameshindwa!" Baada ya muda nilikwenda kutizama hali ya vita ambavyo vilikuwa kama awali, lakini naapa kwa Allaah pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliporusha zile changarawe nikaona ile harara na nguvu za makafiri zimepungua, hivyo kuanza kukimbia." [Muslim]

 

Na ugawaji wa ngawira uliwatia mtihani Answaar wa Madiynah kama zinavyoelezea Hadiyth zifuatazo: 

 

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَزْهَرُ، عَنِ ابْنِ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ زَيْدِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمَ حُنَيْنٍ الْتَقَى هَوَازِنُ وَمَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم عَشَرَةُ آلاَفٍ وَالطُّلَقَاءُ فَأَدْبَرُوا قَالَ ‏"‏ يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ‏"‏‏.‏ قَالُوا لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَسَعْدَيْكَ، لَبَّيْكَ نَحْنُ بَيْنَ يَدَيْكَ، فَنَزَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ ‏"‏ أَنَا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ ‏"‏‏.‏ فَانْهَزَمَ الْمُشْرِكُونَ، فَأَعْطَى الطُّلَقَاءَ وَالْمُهَاجِرِينَ وَلَمْ يُعْطِ الأَنْصَارَ شَيْئًا فَقَالُوا، فَدَعَاهُمْ فَأَدْخَلَهُمْ فِي قُبَّةٍ فَقَالَ ‏"‏ أَمَا تَرْضَوْنَ أَنْ يَذْهَبَ النَّاسُ بِالشَّاةِ وَالْبَعِيرِ، وَتَذْهَبُونَ بِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏لَوْ سَلَكَ النَّاسُ وَادِيًا وَسَلَكَتِ الأَنْصَارُ شِعْبًا لاَخْتَرْتُ شِعْبَ الأَنْصَارِ ‏"‏

 

Amesimulia Anas Bin Maalik (رضي الله عنه): Katika siku ya (vita vya) Hunayn, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwakabili kabila la Hawaazin ilhali kulikuwa na watu elfu kumi na Atw-Twulaqaa (waliosilimu katika Siku ya Fat-h [ukombozi] wa Makkah) pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). (Waislamu) walipokimbia, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaambia, “Enyi kundi la Answaar!” Wakajibu:  "Labbayka, Ee Rasuli wa Allaah wa Sa’dayka! Tuko chini ya amri yako.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremka chini (kutoka juu ya nyumbu wake) na kusema: "Mimi ni Mja wa Allaah na Rasuli Wake.” Washirikina wakashindwa vita. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawagawia ghanima (mateka) ya vita Atw-Twulaqaa na Muhaajiruwn na hakuwapa chochote Answaar. Answaar wakasema (maneno ya kutoridhika) basi akawaita na kuwakaribisha chini ya hema la ngozi na kuwaambia: "Je, hamtoridhia kuwa wao wamechukua kondoo na ngamia na nyinyi mtaondoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaongeza: “Kama watu wangepita njia ya bondeni na Answaar wakapita njia ya milimani, basi ningepita njia ya milimani ya Answaar." [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Maghaazi]

 

عن عبد الله ابن مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا كَانَ يَومُ حُنَينٍ آثَرَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم نَاسًا في القسْمَةِ، فَأعْطَى الأقْرَعَ بْنَ حَابسٍ مائَةً مِنَ الإِبِلِ، وَأَعْطَى عُيَيْنَة بْنَ حصن مِثْلَ ذلِكَ، وَأَعطَى نَاسًا مِنْ أشْرافِ العَرَبِ وآثَرَهُمْ يَوْمَئِذٍ في القسْمَةِ. فَقَالَ رَجُلٌ: واللهِ إنَّ هذِهِ قِسْمَةٌ مَا عُدِلَ فِيهَا، وَمَا أُريدَ فيهَا وَجْهُ اللهِ، فَقُلْتُ: وَاللهِ لأُخْبِرَنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، فَأَتَيْتُهُ فَأخْبَرتُهُ بمَا قَالَ، فَتَغَيَّرَ وَجْهُهُ حَتَّى كَانَ كالصِّرْفِ. ثُمَّ قَالَ: ((فَمَنْ يَعْدِلُ إِذَا لم يَعْدِلِ اللهُ وَرسولُهُ؟)) ثُمَّ قَالَ: ((يَرْحَمُ اللهُ مُوسَى قَدْ أُوذِيَ بأكْثَرَ مِنْ هَذَا فَصَبر)). فَقُلْتُ: لا جَرَمَ لا أرْفَعُ إِلَيْه بَعدَهَا حَدِيثًا. مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: “Siku ya vita vya Hunayn, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwafadhilisha baadhi ya watu katika mgao. Akampa Al-Aqra’ bin Haabis ngamia mia moja, akampa Uyaynah bin Hiswn mfano wake, na akawapa watu watukufu wa Kiarabu na akawafadhilisha katika mgao siku hiyo. Mtu mmoja akasema: Wa-Allaahi huu ni mgao usio na uadilifu! Wala haujakusudiwa Radhi ya Allaah! Nikasema: Wa-Allaahi nitamueleza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Nikaenda na kumueleza aliyoyasema mtu huyo. Uso wake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ukabadilika hata ukawa mwekundu. Kisha akasema: “Ni nani atakaefanya uadilifu ikiwa Allaah na Rasuli wake Hawakufanya uadilifu?” Halafu akasema: “Allaah Amrehemu Muwsaa, hakika aliudhiwa zaidi ya hivi na akasubiri!” Nikasema: Kwa hakika sitomueleza tena (mazungumzo kama haya ya kumuudhi). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[5] Uzayr Hakuwa Nabiy Wala Haiwezekani Allaah (سبحانه وتعالى) Ajifanyie Mwana:

 

‘Uzayr alikuwa ni mja mwema miongoni mwa Wana wa Israaiyl. Na haijathibitika kuwa yeye ni Nabii, lakini Mayahudi wanasema kuwa ‘Uzayr ni Nabii miongoni mwa Manabii wa Bani Israaiyl. [Ibn Kathiyr, Al-Bidaaya Wan-Nihaayah (2/389)] 

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sijui kama Tubba’ (Mfalme wa Yemen alikuwa mshirikina kisha akasilimu) alilaaniwa au laa! Na sijui kama ‘Uzayr ni Nabii au laa.” [Sunan Abiy Daawuwd, ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy]

 

Rejea Al-Baqarah (2:259) kuhusu ‘Uzayr.

 

Kuhusu Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) rejea Aayah inayofuatia (9:31) na tanbihi yake.

 

Na pia:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ أُنَاسًا فِي زَمَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلْ نَرَى رَبَّنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ نَعَمْ، هَلْ تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ الشَّمْسِ بِالظَّهِيرَةِ، ضَوْءٌ لَيْسَ فِيهَا سَحَابٌ ‏"‏‏.‏ قَالُوا لاَ‏.‏ قَالَ ‏"‏ وَهَلْ تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ، ضَوْءٌ لَيْسَ فِيهَا سَحَابٌ ‏"‏‏.‏ قَالُوا لاَ‏.‏ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ مَا تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، إِلاَّ كَمَا تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ أَحَدِهِمَا، إِذَا كَانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ تَتْبَعُ كُلُّ أُمَّةٍ مَا كَانَتْ تَعْبُدُ‏.‏ فَلاَ يَبْقَى مَنْ كَانَ يَعْبُدُ غَيْرَ اللَّهِ مِنَ الأَصْنَامِ وَالأَنْصَابِ إِلاَّ يَتَسَاقَطُونَ فِي النَّارِ، حَتَّى إِذَا لَمْ يَبْقَ إِلاَّ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ اللَّهَ، بَرٌّ أَوْ فَاجِرٌ وَغُبَّرَاتُ أَهْلِ الْكِتَابِ، فَيُدْعَى الْيَهُودُ فَيُقَالُ لَهُمْ مَنْ كُنْتُمْ تَعْبُدُونَ قَالُوا كُنَّا نَعْبُدُ عُزَيْرَ ابْنَ اللَّهِ‏.‏ فَيُقَالُ لَهُمْ كَذَبْتُمْ، مَا اتَّخَذَ اللَّهُ مِنْ صَاحِبَةٍ وَلاَ وَلَدٍ، فَمَاذَا تَبْغُونَ فَقَالُوا عَطِشْنَا رَبَّنَا فَاسْقِنَا‏.‏ فَيُشَارُ أَلاَ تَرِدُونَ، فَيُحْشَرُونَ إِلَى النَّارِ كَأَنَّهَا سَرَابٌ، يَحْطِمُ بَعْضُهَا بَعْضًا فَيَتَسَاقَطُونَ فِي النَّارِ، ثُمَّ يُدْعَى النَّصَارَى، فَيُقَالُ لَهُمْ مَنْ كُنْتُمْ تَعْبُدُونَ قَالُوا كُنَّا نَعْبُدُ الْمَسِيحَ ابْنَ اللَّهِ‏.‏ فَيُقَالُ لَهُمْ كَذَبْتُمْ، مَا اتَّخَذَ اللَّهُ مِنْ صَاحِبَةٍ وَلاَ وَلَدٍ‏.‏ فَيُقَالُ لَهُمْ مَاذَا تَبْغُونَ فَكَذَلِكَ مِثْلَ الأَوَّلِ، حَتَّى إِذَا لَمْ يَبْقَ إِلاَّ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ اللَّهَ مِنْ بَرٍّ أَوْ فَاجِرٍ، أَتَاهُمْ رَبُّ الْعَالَمِينَ فِي أَدْنَى صُورَةٍ مِنَ الَّتِي رَأَوْهُ فِيهَا، فَيُقَالُ مَاذَا تَنْتَظِرُونَ تَتْبَعُ كُلُّ أُمَّةٍ مَا كَانَتْ تَعْبُدُ‏.‏ قَالُوا فَارَقْنَا النَّاسَ فِي الدُّنْيَا عَلَى أَفْقَرِ مَا كُنَّا إِلَيْهِمْ، وَلَمْ نُصَاحِبْهُمْ، وَنَحْنُ نَنْتَظِرُ رَبَّنَا الَّذِي كُنَّا نَعْبُدُ‏.‏ فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ، فَيَقُولُونَ لاَ نُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا‏.‏ مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا ‏"‏‏.‏

Amesimulia Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه):  Hakika watu katika zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walisema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, tutamuona Rabb wetu Siku ya Qiyaamah?  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naam! Je, kwani mna shida yoyote ya kuliona jua adhuhuri yenye mwangaza na hakuna mawingu (mbinguni)?” Wakajibu: Hapana. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je, mna tatizo lolote la kuuona mwezi usiku unapokuwa umekamilika ukiwa umeng’ara na hakuna mawingu mbinguni?” Wakajibu: Hapana. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “(Hivyo hivyo) hamtakuwa na shida kumuona Allaah (عزَّ وجلَّ) Siku ya Qiyaamah kama ambavyo kwamba hamna tatizo kuviona hivyo viwili (jua na mwezi). Siku ya Qiyaamah, atanadi mwenye kunadi: Kila ummah ufuate kile ambacho walikuwa wakiabudu. Hawatobakia wale wote waliokuwa wakiabudu asiyekuwa Allaah, miongoni mwa masanamu na miungu mingine isipokuwa wataanguka motoni mpaka hakutabakia isipokuwa waliokuwa wakimuabudu Allaah tu katika wema au waovu, na waliobakia katika katika kundi la waliopewa Kitabu. Kisha Mayahudi wataitwa na wataulizwa: Mlikuwa mkimuabudu nani? Watasema: Tulikuwa tukimuabudu ‘Uzayr mwana wa Allaah. Wataambiwa: Nyinyi ni waongo, kwani Allaah Hakumfanya yeyote kuwa mke au mwana. Je, mnataka nini sasa? Watasema: Ee Rabb wetu! Tuna kiu, hivyo Tunyweshe kinywaji. Wataelekezwa na wataambiwa: Je, mtakunywa? Hapo watakusanywa motoni, moto ambao utaonekana kama sarabi ambayo pande zake tofauti zitajivunjavunja. Kisha wataanguka motoni. Baada ya hapo wataitwa Manaswara wataulizwa: Je, mlikuwa mkimuabudu nani? Watasema: Tulikuwa tukimuabudu Masiyh mwana wa Allaah. Wataambiwa:  Mumesema uwongo, kwani Allaah Hakumfanya yeyote kuwa mkewe au mwana. Kisha wataambiwa: Je, mnataka nini? Watasema kama walivyosema wale waliotangulia (yaani Mayahudi). Hatimaye, watabakia (katika mkusanyiko) wale tu waliokuwa wakimuabudu Allaah Pekee, katika wema na waovu. Kisha (Allaah) Rabb wa walimwengu Atakuja kwao katika sura iliyo karibu waliyofikiria akilini mwao kumhusu Yeye. Kutasemwa: Je, mnasubiri nini? Kila ummah umefuata walichokuwa wakiabudu. Watajibu: Tuliwaacha watu duniani tulipokuwa na haja kubwa nao, nasi hatukuwafanya wao kuwa rafiki zetu. Sasa tunamsubiri Rabb wetu tuliyekuwa tukimuabudu. Allaah Atasema: Mimi Ndiye Rabb wenu. Watasema mara mbili au tatu: Sisi hatumshirikishi yeyote na Allaah.” [Al-Bukhaariy, Kitaab At-Tafsiyr]

 

[6] Ahbaar: Ni Mafuqahaa weledi wa Kiyahudi:

 

[7] Ruhbaan: Ni Monaki wa Kinaswara: Rejea Al-Maaidah (5:82).

 

[8] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Amekanusha Kuabudiwa:

 

Rejea An-Nisaa (4:171), Al-Maaidah (5:17), (5:72-76), (5:116-118), na Maryam (19:30-36). Ni Aayah ambazo Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  mwenyewe amekanusha kuwa yeye hapasi kuabudiwa, bali yeye ni mja na Rasuli wa Allaah, na kwamba anayepasa kuabudiwa ni Allaah Pekee.

 

[9] Dini Ya Kiislamu Ndio Dini Itakayoshinda Dini Nyenginezo:

 

Rejea Al-Fat-h (48:28) na Asw-Swaff (6:9) kwenye maelezo bayana.

 

[11] Miezi Minne Mitukufu:

 

عن أبي بَكْرَةَ رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أنه قَالَ:  ((إن الزَّمَانَ قَدْ اسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ثَلاثٌ مُتَوَالِيَاتٌ ذُو الْقَعْدَةِ وَذُو الْحِجَّةِ وَالْمُحَرَّمُ وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشَعْبَانَ))

Amesimulia Abu Bakr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika mgawano wa zama umerudi katika hali yake ya asili siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili; minne miongoni mwa hiyo ni Mitukufu, mitatu inafuatana pamoja, nayo ni Dhul-Qa'dah, Dhul-Hijjah na Al-Muharram, na mwengine ni Rajab wa (kabila la) Mudhwarr ambao uko baina ya Jumaadaa na Sha'baan.”  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Imeharamishwa kufanya aina yoyote ile ya maasi ndani ya miezi mitukufu ikiwemo amri ya kutokupigana vita. Rejea pia Al-Baqarah (2:217).

 

Na imeamrishwa pia kutenda mema kwa wingi ndani ya Miezi hii kwa kuwa malipo yake yanakuwa maradufu. Na kutenda maasi pia jazaa yake ni maradufu. Imaam Atw-Twabariy (رحمه الله)  amesema: “Katika miezi yote kumi na mbili, Allaah (سبحانه وتعالى)    Ameichagua hii minne, na Ameifanya kuwa ni mitukufu, na Amesisitiza itakaswe, na kwamba dhambi zitakazofanyika humo malipo yake ni maradufu, na hali kadhalika thawabu za amali njema zinakuwa maradufu na zaidi. [Atw-Twabariy (14:238)].

Na Qataadah amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):  

فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ

“Basi msijidhulumu humo nafsi zenu humo.”

 

"Dhulma itakayotendeka katika Miezi Mitukufu ni mbaya na kubwa (au hatari) kuliko dhulma itakayotendeka katika miezi mingine. Hakika dhulma daima ni dhambi, lakini Allaah Hufanya baadhi ya vitu kuwa ni vizito kuliko vingine vile Apendavyo Mwenyewe. Akachagua baadhi ya Viumbe Vyake na baadhi ya vitu kuwa bora zaidi kuliko vingine. Amechagua Wajumbe kutoka Malaika na kutoka wanaadamu. Vile vile Amechagua baadhi ya kauli Zake kuwa ni bora kuliko nyingine, Misikiti kuwa bora kuliko sehemu nyingine za ardhi, Ramadhwaan na Miezi Mitukufu kuwa bora kuliko miezi mingine, siku ya Ijumaa kuwa ni bora kuliko siku nyingine, na usiku wa Laylatul-Qadr kuwa ni bora kuliko masiku mengine. Kwa hiyo basi, vitakase vile Alivyovitakasa Allaah, kwani kufanya hivyo ni vitendo vya watu wenye akili na wenye kufahamu." [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[12] Ghazwat-Tabuwk:

 

Tambua kwamba, sehemu kubwa ya Suwrah hii imeteremshwa wakati wa Vita vya Tabuwk [Imaam As-Sa’diy]. Na Vita vitukufu vya Tabuwk vimetajwa katika Aayah zifuatazo za Suwrah hii At-Tawbah: (38-39), (46), (48), (64-66), (74), (107-110), (117-118).

 

[13] Ghaar (Pango) Thawr Na Swahibu Yake Ni Abu Bakr  (رضي الله عنه):

 

Swahibu yake katika pango  hilo  ni Abu Bakr (رضي الله عنه)  pale walipohajiri kutoka Makkah kuelekea Madiynah huku makafiri wa ki-Quraysh wakiwa wanawasaka ili wawaue, ndipo wakajificha katika pango hilo kwa siku tatu. Na humo Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwahifadhi kwa Uwezo na Miujiza Yake. Pango hilo lilikuwa linaitwa Jabal Thawr ambalo ni refu na njia yake ni hatari mno, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahibu yake Abu Bakr (رضي الله عنه)   walifanikiwa kulipanda na kulifikia pango hilo lililoko juu ya jabali hilo. Ndipo likajulikana baadaye kwa jina la Ghaar Thawr (Pango la Thawr), wakajificha humo.

 

 

عَنْ أَنَسٍ، عَنْ أَبِي بَكْرٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي الْغَارِ فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِأَقْدَامِ الْقَوْمِ، فَقُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ، لَوْ أَنَّ بَعْضَهُمْ طَأْطَأَ بَصَرَهُ رَآنَا‏.‏ قَالَ ‏ "‏ اسْكُتْ يَا أَبَا بَكْرٍ، اثْنَانِ اللَّهُ ثَالِثُهُمَا ‏

Amesimulia Anas (رضي الله عنه)  kwamba amemsikia Abu Bakr (رضي الله عنه)  akisema: Nilikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pangoni, nikanyanyua kichwa changu (kutazama), nikaiona miguu ya watu (ikitusogelea). Nikasema: Ee Nabiy wa Allaah!  Mmoja wao akitazama chini (kidogo tu) atatuona! Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: "Nyamaza ee Abu Bakr, (sisi) wawili, wa tatu wetu ni Allaah." [Al-Bukhaariy]

 

Na katika Riwaaya nyingine: "Unaonaje juu ya wawili, Allaah wa tatu wao?"

 

[14] Mawlaa "مَوْلَى":  Ni Rafiki Mwandani Wa Karibu Na Mlinzi, Msaidizi, Bwana.

 

Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Sifa Zake.

 

[15] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

058-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah Aayah 058: وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ

 

 

[16] Aina Ya Watu Wanane Wanaostahiki Zakaah Ya Mali:

 

(i) Mafakiri (ii) Masikini (iii) Wanaozitumikia kazi za ugawaji wa Zakaah (iv) Wanaotiwa nguvu nyoyo zao katika Uislamu (v) Kuwakomboa mateka (vi) Wenye Deni (vii) Katika Njia ya Allaah (viii) Msafiri Aliyeharibikiwa.

 

Na Tafsiyr ni kama ifuatavyo:

 

Zakaah za lazima (faradhi) zinapewa: (i) Wahitaji wasiomiliki kitu. (ii) Masikini wasiomiliki kiwango kinachowatosha kwa mahitaji yao. (iii) Wenye kuzishughulikia kwa kuzikusanya. (iv) Wale ambao mwazizoeza nyoyo zao miongoni mwa wale mnaotarajia wasilimu au ipate nguvu imaan yao au wawe na manufaa kwa Waislamu au mzuie kwazo madhara ya mtu yoyote yasiwafikie Waislamu. (v) Pia zinatolewa katika kuacha huru watumwa na wale wenye mikataba ya uhuru. (vi) Na zinatolewa kupewa wenye kuingia kwenye madeni kwa sababu ya kuleta maelewano baina ya watu na wenye kulemewa na madeni waliyokopa kwa lengo lisiliokuwa la uharibifu au utumiaji wa kupita kiasi kisha wakashindwa kulipa. (vii) Na zinapewa wapiganaji katika Njia ya Allaah. (viii) Na zinapewa msafiri aliyeishiwa na matumizi.

 

Ugawaji huu ni lazima Aliyoifaradhia Allaah na Akaikadiria. Na Allaah ni Mjuzi mno wa mambo yanayowafaa waja Wake, ni Mwingi wa Hikma katika Uendeshaji wa Mambo Yake na Sharia Zake. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[17] Maana Waliyokusudia Wanafiki Ya Mtegaji Sikio: 

 

Wanafiki wamekusudia kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposikia lolote hulikubali, na kwamba hapambanuwi baina ya kweli na uongo, wala kati ya baya na zuri. Na akiambiwa jambo lolote anaamini tu, na wakimwendea kumwapia anaamini, na wakimwendea kutoa nyudhuru na kuomba msamaha anawakubalia tu.

 

[18] Kufanya Istihzai Katika Mambo Ya Dini Ni Kukufuru:

 

Kuanzia Aayah namba (64-66), ni haramisho la kufanya istihzai, bali Aayah hii ‘Ulamaa wamesema kuwa ni dalili kuwa anayefanya istihzai katika mambo ya Dini, basi huyo amekufuru!  Rejea An-Nisaa (4:140).

 

[19] Al-Walaa Wal-Baraa (Kupenda Na Kuandamana, Kuchukia Na Kutengana Kwa Ajili Ya Allaah):

 

Rejea Al-Mujaadalah (58:22) kwenye faida ya maudhui hii.

 

 

[20] Mahimizo Ya Kuamrishana Mema Na Kukatazana Munkari (Maovu):

 

Rejea pia Adh-Dhaariyaat (51:55) kwenye faida nyenginezo na rejea zake.

 

[21]  Kisa Kinachonasibishwa Na Tha’labah Bin Haatwib (رضي الله عنه) Si Cha Kweli:

 

Baadhi ya makhatibu hutafsiri Aayah kuanza hii (75) hadi namba (77) kwamba zinamhusu Swahaba Mtukufu Tha’labah Bin Haatwib (رضي الله عنه). Lakini ‘Ulamaa wamepinga hili kwa maelezo kadhaa miongoni mwa ‘Ulamaa hao na kauli zao ni:  

 

(i)-Imaam Al-Qurtwuby amesema katika Jaami’ al-Ahkaam:

 

“Tha’labah alipigana vita vya Badr, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alishuhudia kuwa ni Muislamu wa kweli, kwa hivyo kisa hiki anachonasibishwa nacho si cha kweli.”

 

(ii)-Al-Haafidh Al-‘Iraaqiy amesema katika tahakiki ya Hadiyth za kitabu cha Al-Ihyaa ‘Uluwm ad-Diyn cha Ghazaaliy:

 

“Hadiyth hii imetolewa na Atw-Twabaraaniy na Isnaad yake ni dhaifu.”

 

(iii)-Ibn Hajar amesema katika Al-Iswaabah Fiy Tamyiyz Asw-Swahaabah:

 

“Kisa hiki sidhani kama ni sahihi kwa sababu Tha’labah huyu amepigana vita vya Badr, na Hadiyth Swahiyh ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) inasema: “Waliopigana vita vya Badr hawaingii motoni, na kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaambia; “Fanyeni mtakacho, mumekwisha ghufuriwa madhambi yenu.”

 

Kwa hiyo iweje Tha’labah awe mnafiki?”

 

Hali kadhaalika Fataawaa za ‘Ulamaa Wa Al-Lajnah al-Lajnah ad-Daaimah Lil-Buhuwth al-‘Ilmiyyah wal Iftaa’ (49/26) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn [Sharh Uswuwl fiy Tafsiyr - Ibn ‘Uthaymiyn]

 

[25] Waliotangulia Awali (Salaf):

 

Hao ndio Salaf Swaalih, nao ndio waliokuweko katika karne tatu za mwanzo; Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Taabi’iyn ni wanafunzi wao, pamoja na Atbaa’ Taabi’iyn (waliowafuata Taabi’iyn) ambao Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewashuhudia kwa kheri aliposema:

 

خَيْرُ النَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ

Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia.” [Al-Bukhaari]

 

Kisha wengineo waliowafuata hao kwa ihsaan katika Manhaj yao ya mafundisho ya Kitabu na Sunnah, na kuifanyia daawah (kuilingania), na kuifanyia kazi. Na wakawa kwa hayo ni Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah. Rejea Al-Hashr (59:10).

 

[26] Masjid Dhwiraar (Msikiti wa madhara):

 

Aayah hizi At-Tawbah (9:107-110), zinazungumzia msikiti wa madhara. Ni msikiti waliojenga wanafiki kwa sababu hawakutaka kuswali jamaa pamoja na Waislamu katika Masjid Qubaa ambao ulikuwa karibu na sehemu hiyo. Walioujenga msikiti huo wa madhara ni wanafiki kumi na mbili. Wakadai kuwa wameujenga kwa niya ya kusaidia walio dhaifu na wagonjwa kutokana na nyusiku za mvua na za baridi, na kwamba hawakukusudia isipokuwa wema. Wakamuomba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aswali humo ili awatilie barakah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anajiandaa wakati huo kuelekea katika vita vya Jihaad vya Tabuwk, hivyo akawaitikia kuwa pindi watakaporudi atakuja kuswali. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Aliteremsha Aayah hizo tukufu kufichua ubaya wao, na Akamkataza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuswali humo.

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn  (رحمه الله) amesema: “Masjid Dhwiraar (msikiti wa madhara) ulijengwa kwa niya ya ufisadi kutokana na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى)  ya Aayah hii ya At-Tawbah (9:107). Walioujenga ni wanafiki, na makusudio yao (kama ilivyotajwa katika Aayah) ni:

 

(i) Kuleta madhara kwa Masjid Qubaa, ndio maana ukaitwa msikiti wa madhara.

 

(ii) Kumkufuru Allaah, kwa kuwa ukafiri unapangwa humo na kupitishwa humo - tunaomba kinga kwa Allaah - na walioujenga pia ni wanafiki.

 

(iii) Kuwafarikisha Waumini, kwani badala ya kuswali katika Masjid Qubaa safu moja au safu mbili, iswaliwe nusu safu, na wengineo waswali  msikiti mwengine. Na kuna sharia (hukumu) kuhusu mijumuiko ya Waumini.

 

(iv) Kuwa ngome kwa waliompiga vita Allaah na Rasuli Wake. Mtu mmoja aitwaye Abu ‘Aamir Al-Faasiq alikwenda Sham. Kulikuweko mawasiliano baina yake na wanafiki walioujenga msikiti huo kwa maelekezo yake, wakawa wanajumuika humo kupanga waliyoyakusudia ya njama na hadaa za kumfanyia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na Swahaba zake. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ

“Na “Bila shaka wanaapa: Hatujakusudia ila jambo zuri.”

 

Basi hii ndio kawaida ya wanafiki; viapo vya uongo! [Majmuw’u Fataawaa wa Rasaail Ibn ‘Uthaymiyn (9:226-227)]

 

[27]  Msikiti Ulioasisiwa Juu Ya Taqwa:

 

Kuna kauli mbili kuhusu Msikiti huo uliokusudiwa. (i) Masjid Qubaa (ii) Masjid Nabawiy (Msikiti wa Nabiy  صلى الله عليه وآله وسلم)    Lakini ‘Ulamaa wanaona kuwa kauli hazipingani, kwani Misikiti yote hiyo miwili iliasisiwa, au ilikuwa Misikiti ya mwanzo kujengwa kwa ajili ya Waislamu.

 

(i) Masjid Qubaa: Ni Msikiti wa kwanza kabisa kujengwa na Waislamu walipofika Madiynah baada ya kuhajiri kutoka Makkah. Ngamia wake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alipiga magoti sehemu hiyo. Akapendelea hapo kujengwe Msikiti huo. Na hapo kulikuwa na kisima cha Swahaba Mtukufu Abu Ayyuwb Al-Answaariy. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akabashiria fadhila za kuswali rakaa mbili katika Masjid Qubaa kuwa ni sawa na thawabu za kutekeleza ‘Umrah kutokana na kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم): “Mwenye kutawadha nyumbani kwake, kisha akauendea Masjid Qubaa, akaswali ndani yake Swalaah moja, basi anapata thawabu za mfano wa ‘Umrah.”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Maajah (1412)] 

 

(ii) Masjid Nabawiy: Ni Msikiti wa kwanza kujengwa na Waislamu walipofika Madiynah, na ndio Masjid Nabawiy (Msikiti wa Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) na ndipo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   alipofanya kuwa ni maskani yake pamoja na wakeze. Na aghlabu ya Swahaba pia walifanya masikani zao pembezoni mwake.  Baina yake na Masjid Qubaa ni umbali wa kilo mita tano.

 

[28] As-Saaihuwn: 

 

‘Ulamaa wametaja maana mbili za As-Saaihuwn:

 

(i)   Wenye kufunga Swiyaam kama vile walivyokusudiwa wakeze Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Suwrat At-Tahriym (66:5).

 

(ii)   Wenye kusafiri kwa ajili ya ibaada kama vile Hajj, ‘Umrah, Jihaad katika Njia ya Allaah, kutafuta ilimu, Muhaajiruwn (wahamao kwa ajili ya Dini), kudumisha kuunga undugu wa damu na jamaa wa karibu, na mengineyo yote yaliyomo ndani ya juhudi za kwenda huku na kule kwa ajili ya ibaada na kufanya khayraat (mambo ya kheri).

 

[29] Haramisho La Kuwaombea Makafiri Maghfirah:

 

Aayah hii (113) imeteremshwa kumhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotaka kumuombea maghfirah ammi yake Abu Twaalib pindi alipofariki. Allaah (سبحانه وتعالى) Akamkataza kufanya hivyo. Bonyeza viungo vifuatavyo vya Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

028-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Qaswasw: Aayah (56): إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ

  

113-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah Aayah 113-114: مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ

 

Kwa hiyo haramisho hili linahusu yeyote yule aliyekafiri hata kama ni mzazi kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah inayofuatia namba (114), kuhusu Nabiy Ibraahiiym (عليه السّلام) ambaye naye aliacha kumuombea maghfirah baba yake baada ya kutambua ni adui wa Allaah. Rejea pia Al-Mumtahinah (60:4).  

 

Rejea pia Al-Qaswasw (28:56).

 

[30] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

117-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah Aayah 117: لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ

 

Rehma Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwaghufuria Swahaba:

 

Tafsiyr:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Amemuelekeza Nabiy Wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kurudi Kwake na kumtii, na Aakawakubalia tawbah Muhaajiruwn waliohama nyumba zao na jamaa zao wakaenda kwenye makazi ya amani (Madiynah), na pia Aliwakubalia tawbah Anaswaar waliomuhami Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), waliotoka pamoja na yeye kupambana na maadui katika vita vya Tabuwk, katika kipindi cha joto kali na shida ya chakula na vipando. Allaah (سبحانه وتعالى) Amwakubalia tawbah yao baada ya hali kufikia kiwango kwamba nyoyo za baadhi yao zilikaribia kuiyepuka haki na kupendelea ulegevu na utulivu. Lakini Allaah (عزّ وجلّ) Aliwathibitisha na Akawapa nguvu na Akawakubalia tawbah. Hakika Yeye kwao ni Mwingi wa Upole ni Mwenye Huruma. Na miongoni mwa Huruma Yake kwao ni kwamba Aliwapa neema ya kutubia, Akaikubali tawbah yao na Akawathibitisha juu yake. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[31] Watatu Hao Ni: Ka’ab Bin Maalik, Hilaal Bin Umayyah, Muraarah Bin Ar-Rabiy’ (رضي الله عنهم):

 

Swahaba watatu hao wamekusudiwa kuanzia Aayah (117-119), na ndio sababu ya kuteremshwa Aayah hizi. Kisa chao amekisimulia mwenyewe Ka’ab (رضي الله عنه) , na kimeanzia pale walipotangaziwa kwenda Jihaad ya vita vya Tabuwk ambavyo vilikuwa ni vita vya hali ngumu kabisa na mashaka makubwa kutokana na jua kali, ukosefu wa vifaa, zana, na vipando, mbali na wingi wa maadui. Na hii ndio sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Amevitaja Vita hivi katika Aayah (117) kuwa ni “Saa ya dhiki.”

Swahaba hawa watatu walikhalifu amri ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ya kutoka kwenda vitani wakabakia nyuma, lakini walikuja kujuta mno, wakaomba tawbah, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwangojelesha muda mrefu kupokea tawbah yao hadi wakafikwa na dhiki kubwa, lakini nao hawakukata tamaa na Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى). Hatimaye Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaghufuria.

 

Kisa hiki kina mafundisho kadhaa kwa Waumini: (i) Kutokuasi Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) (ii) Kuvumilia kwa subira ya juu katika hali ya dhiki (ii) Kutokukata tamaa katika kumuomba Allaah (سبحانه وتعالى) maghfirah (iv) Shaytwaan anaweza kuwaghilibu hata Waumini wa kweli kama Swahaba hao watukufu ambao waliteleza katika kutii amri.

 

Pia kuna mafundisho mengineyo mengi yaliyotokana na vita vyenyewe. Ni kisa kirefu ambacho kimepokelewa na Imaam [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ahmad]

 

Bonyeza kiungo kifuatacho katika Hadiyth namba (9) ambayo Ka’b Bin Maalik (رضي الله عنه) anaelezea mwenyewe kisa chao hicho:

 

002-Riyaadhw Asw-Swalihiyn: Mlango Wa Tawbah

 

[32] Qur-aan Inaposomwa, Inawazidisha Waumini Imaan. Ama Kafiri Na Wenye Maradhi Katika Nyoyo Zao, Haiwazidishii Ila Rijs (Unafiki, Shaka Kufru n.k).

 

Aayah hii namba (124) na inayofuatia (125), inataja kuwa Qur-aan inawazidisha imaan Waumini. Ama wenye maradhi ya moyo, inawazidishia rijs (unafiki, shaka, kufru n.k). Rejea Al-Israa (17:82) kwenye maelezo kuhusu Qur-aan kwamba ni shifaa na rehma kwa Waumini. Ama kwa makafiri, haiwazidishii isipokuwa khasara.

 

Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.

 

Rejea pia Fusw-Swilat (41:44) kwenye uchambuzi kuhusu Qur-aan kuwa ni shifaa (poza na tiba), mawaidha na rehma kwa Waumini.

 

Rejea pia Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.

 

Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.

 

[33] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuwa Na Upole, Huruma, Na Kuwajali Mno Waumini.

 

Utakuta katika Siyrah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) jinsi alivyokuwa na sifa hizo zote kwa Waumini, bali hata aliwajali Waumini asiokutana nao, yaani katika ummah wake wa zama zote. Rejea Al-Maaidah (5:118).

 

Hadiyth nyingi zimetaja sifa hizo zake. Kati yake ni hii ifuatayo ambayo amejali na kukhofia Waumini wakingwe na moto:

 

Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wangu na mfano wenu ni kama mtu anayewasha moto, kisha wadudu na nondo wala nguo wakawa wanaangukia humo, kisha yeye (huyo mtu) anajaribu kuwatoa humo nami huku nawazuia migongo yenu isiangukie katika moto, lakini mnateleza mikononi mwangu.” [Muslim]

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwajali hata Swahaba walio duni kabisa:

 

عَنْ أَبِي بَرْزَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ فِي مَغْزًى لَهُ فَأَفَاءَ اللَّهُ عَلَيْهِ فَقَالَ لأَصْحَابِهِ ‏"‏ هَلْ تَفْقِدُونَ مِنْ أَحَدٍ ‏"‏ ‏.‏ قَالُوا نَعَمْ فُلاَنًا وَفُلاَنًا وَفُلاَنًا ‏.‏ ثُمَّ قَالَ ‏"‏ هَلْ تَفْقِدُونَ مِنْ أَحَدٍ ‏"‏ ‏.‏ قَالُوا نَعَمْ فُلاَنًا وَفُلاَنًا وَفُلاَنًا ‏.‏ ثُمَّ قَالَ ‏"‏ هَلْ تَفْقِدُونَ مِنْ أَحَدٍ ‏"‏ ‏.‏ قَالُوا لاَ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ لَكِنِّي أَفْقِدُ جُلَيْبِيبًا فَاطْلُبُوهُ ‏"‏ ‏.‏ فَطُلِبَ فِي الْقَتْلَى فَوَجَدُوهُ إِلَى جَنْبِ سَبْعَةٍ قَدْ قَتَلَهُمْ ثُمَّ قَتَلُوهُ فَأَتَى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَوَقَفَ عَلَيْهِ فَقَالَ ‏"‏ قَتَلَ سَبْعَةً ثُمَّ قَتَلُوهُ هَذَا مِنِّي وَأَنَا مِنْهُ هَذَا مِنِّي وَأَنَا مِنْهُ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ فَوَضَعَهُ عَلَى سَاعِدَيْهِ لَيْسَ لَهُ إِلاَّ سَاعِدَا النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ فَحُفِرَ لَهُ وَوُضِعَ فِي قَبْرِهِ ‏.‏ وَلَمْ يَذْكُرْ غَسْلاً ‏.‏

Amesimlia Abuu Barzah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuweko katika uwanja wa vita ambao Allaah Alijaalia (ushindi) na kupata ngawira za vita. Akawaambia Swahaba zake: “Je! Kuna yeyote amekosekana kati yenu?” Wakasema: Naam, fulani na fulani.  Akasema tena: “Je! Kuna yeyote kati yenu aliyekosekana?” Wakasema: Naam, fulani na fulani. Kisha akasema tena: “Je! Kuna yeyote kati yenu aliyekosekana?” Wakasema: Hapana. Hapo (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Lakini nimemkosa (simuoni) Julaybiyb, hebu mtafuteni.”  (Swahaba) wakamtafuta (Julaybiyb) kati ya wale waliouawa, wakamkuta kando ya (maiti) saba ambao yeye aliwaua na yeye akauliwa (na adui). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaenda pale akasimama (kando yake) na akasema: “Amewaua watu saba. Ndipo (adui zake) wakamuua. Yeye ni wangu na mimi ni wake.” Kisha akamweka mikononi mwake na hakukuwa na mwingine yeyote wa kumuinua isipokuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha kaburi lilichimbwa kwa ajili yake, akawekwa kaburini na haikutajwa kuhusu kuoshwa kwake”. [Muslim]

 

Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amefafanua Aayah hii kwa sifa kama hizo na nyenginezo za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha mwishowe akasema:

 

“Basi kwa hayo, ndio maana haki yake inatangulizwa kuliko haki nyingine zote za viumbe wengineo, na ni wajibu kwa ummah kumwamini, kumuadhimisha, na kumheshimu kwa utukuzo.”

 

Bonyeza kiungo kifuatacho kupata faida tele kuhusu Sifa na Akhlaaq za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Sifa-Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

[34] Miongoni Mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni Ni Kusema Mara Saba: 

 

حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ

“Amenitosha Allaah Ambaye hakuna mwabudiwa wa haki ila Yeye tu, nimetawakkal Kwake, Naye Ndiye Rabbi wa ‘Arshi Adhimu.”

 

 

Share