102 - At-Takaathur
التَّكَاثُر
102-At-Takaathur
102-At-Takaathur: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ﴿١﴾
1. Kumekughafilisheni kushindana kukithirisha (mali na watoto kwa).
حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ ﴿٢﴾
2. Mpaka muingie makaburini.
كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣﴾
3. Laa hasha! Mtakuja kujua.
ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾
4. Kisha laa hasha! Mtakuja kujua.
كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ ﴿٥﴾
5. Laa hasha! Lau mngelijua ujuzi wa yakini.
لَتَرَوُنَّ الْجَحِيمَ ﴿٦﴾
6. Bila shaka mtauona moto uwakao vikali mno.
ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ الْيَقِينِ ﴿٧﴾
7. Kisha kwa hakika mtauona kwa jicho la yakini.
ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
8. Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu neema.