Shaykh Fawzaan - Bid’ah (Uzushi) Inayotendeka Katika Ziara Ya Kaburi La Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

Bid’ah (Uzushi) Inayotendeka Katika Ziara Ya Kaburi La

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com 

 

 

SWALI:

 

Je, bid’ah gani zinazotendeka na baadhi ya watu katika Kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?

 

 

JIBU:

 

Bid’ah mbali mbali zinatendeka mara kwa mara katika kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mfano; kuingia msikitini akitoa salaam kwake na kukaa karibu na kaburi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((لا تجعلوا قبري عيدًا))

((Msifanye kaburi langu ni sehemu ya kurudiwa rudiwa [kuendewa kila mara])) [Musnad Ahmad, Muswannaf 'Abdir-Razzaaq]

 

Bid’ah nyingine ni kuamini kwamba du'aa hapo hukubaliwa na watu huomba kwa sauti na kumuomba yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuamini kuwa du'aa yake itakubaliwa. Hii ni shirk kubwa kabisa.

 

Inapasa kuzingatia yaliyo katika shariy'ah kama kumtolea salaam Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Akiwa anataka mtu kuomba Du'aa aombe sehemu yoyote katika Msikiti. Na kuomba baada ya Swalah ni bora zaidi

 

 

[Shaykh Ibn Fawzaan, Al-Bid’ah wal- Muhdathaat wa maa laa aswla lahu – uk. 240 Majallah ad-Da’wah, uk. 1612 uk 37]

 

Share