Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hukmu Ya Kujenga Jengo La Sinema (Thieta) Au Kuendesha Kazi Zake

 Hukmu Ya Kujenga Jengo La Sinema (Thieta ) Au Kuendesha Kazi Zake

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah 

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Muislamu anaruhusiwa kujenga jengo la sinema au kuendesha kazi zake humo?

 

JIBU:

 

Muislamu haruhusiwi kujenga jengo la sinema (thieta) au kuendesha kazi zake kwa ajili ya nafsi yake wala kwa ajili ya mtu mwengine kwa sababu ya burudani zilizo haramishwa humo.  Kama inavyojulikana siku hizi duniani, zinaonyeshwa filamu chafu na picha za wasichana ambazo zinachochea uchu na zinashajiisha  uasharati na uharibifu wa akhlaaq. Juu kuna michanganyiko ya wanawake na wanaume ambao si mahaarim zao. (walioharamishwa kuwaoa)

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa, mj. 26, uk. 277, (3501)]

 

 

Share