Imaam Al-Albaaniy: Kupongezana Kwa Kusema "Kullu 'Aamin Wa Antum Bikhayr"

 

Kupongezana Kwa Kuambiana “Kullu ‘Aamin Wa Antum Bikhayr

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Kauli ya ‘Kullu ‘aam wa antum bikhayr’ (kila mwaka na nyinyi katika hali njema) [Hii pia inafanana na kusema “pongezi ya mwaka mpya”, na wengine husema: ‘Kullu sanatin wa anta twayyib’ ikiwa na maana kama hiyo juu.]

 

Haina asli, na tosheka na “Taqabbala Allaahu twaa’atakum” (Allaah Awataqabalie utiifu (‘amali) wenu). (Pia imethibiti kuambiana "Taqabbala Allaahu minnaa wa minkum" Allaah Atutaqabalie ‘amali zetu na zenu).

 

Ama (kusema) “Kullu ‘aamin wa antum bikhayr” ni salamu ya Makafiri iliyoingia kwetu sisi Waislamu kutokana na kughafilika kwetu.

Na kumbusha, kwani hakika ukumbusho unawafaa Waumini.

 

[Silsilatu Al-Hudaa Wan-Nuwr, kanda namba 323]

 

 

Share