Shairi La اللامية (Al-Laamiyyah) La Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله)

 

Shairi La  اللامية  (Al-Laamiyyah) Linalonasibishwa Na

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله)

 

القصيدة اللامية المنسوبة لشيخ الإسلام ابن تيمية

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Shairi hili zuri la ‘Aqiydah linanasibishwa na 'Aalim mkubwa wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah, Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

 

Wametofautiana 'Ulamaa kuhusiana na unasibisho wa utenzi huu kwa Shaykh Al-Islaam. Wako baadhi wachache wanaoona hakuna uthibitisho kuwa ni shairi la Shaykh Al-Islaam, miongoni mwao ni Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah), hata hivyo, 'Ulamaa wengi wameunasibisha naye na kuthibitisha kuwa ni shairi la Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah, miongoni mwao ni 'Aalim mkubwa aliye hai Shaykh Al-‘Allaamah Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah).

 

 

منظومة لشيخ الإسلام ابن تيمية - رحمه الله - بين فيها عقيدته باختصار

 

 

 

يا سَائِلي عَنْ مَذْهَبِي وعَقيدَتِي *** رُزِقَ الهُدى مَنْ لِلْهِدايةِ يَسْأل

Ee mwenye kuniuliza mimi kuhusu madhehebu yangu na ’Aqiydah yangu, ameruzukiwa uongofu mwenye kuuliza kwa ajili ya kuongoka.

 

 

 

اسمَعْ كَلامَ مُحَقِّقٍ في قَـولـِه *** لا يَنْـثَني عَنـهُ ولا يَتَبَدَّل

Sikiliza maneno ya mwenye kuhakiki katika kauli yake, harejei kuachana nayo na wala habadiliki.

 

 

 

حُبُّ الصَّحابَةِ كُلّهمْ لي مَذْهَبٌ *** وَمَوَدَّةُ القُرْبى بِها أَتَوَسّل

Kuwapenda Swahaba wote kwangu mimi ndio madhehebu yangu, na kuwapenda jamaa (Ahlul-Bayt) kwa mapenzi hayo natawasali.

 

 

وَلِكُلِّهِمْ قَـدْرٌ وَفَضْلٌ سـاطِعٌ *** لكِنَّما الصِّديقُ مِنْهُمْ أَفْضَل

Na anacho kila mmoja wao cheo na fadhila za juu, lakini si vinginevyo Asw-Swiddiyq katika wao ni mbora zaidi.

 

 

 

وأقول في القرآن ما جاءت به *** آيـاتـه فـهـو الكريـم المنـزل

Na ninasema katika Qur-aan kile ambacho imekuja nacho, ni Aayah zake Allaah nayo hiyo Qur-aan ni tukufu yenye kuteremshwa.

 

 

 

وأقــول قــال الله جــل جــلالــه *** والمصطفى الهادي ولا أتأول

Na ninasema amesema Allaah umetukuka utukufu wake, na Mustwafaa (Nabiy) mwenye kuongoza wala sifanyi taawili.

 

 

 

وجميعُ آياتِ الصِّفاتِ أُمِرُّهـا *** حَقـاً كما نَقَـلَ الطِّرازُ الأَوَّلُ

Na Aayah zote za sifa nazipitisha, kwa uhakika kabisa kama walivyonukuu kundi la mwanzo.

 

 

 

وأَرُدُّ عُقْبَتَـهـا إلى نُقَّالِهـا *** وأصونُها عـن كُلِّ ما يُتَخَـيَّلُ

Mapokezi mengine...

وأرد عـهـدتــهـا إلـى نـقّـالهـا *** وأصونها عن كل ما يُتخـيـل

Na ninarudisha dhamana yake kwa wanukuzi wake, na ninazilinda kutokana na kila chenye kudhaniwa kibaya.

 

 

 

قُبْحاً لِمَنْ نَبَذَ الكِّتابَ وراءَهُ *** وإذا اسْتَدَلَّ يقولُ قالَ الأخطَلُ

Mapokezi mengine...

قبحاً لمن نبـذ القـرآن وراءه ***  وإذا استدل يقول قال الأخطل

Ni ubaya ulioje kwa mwenye kuitupa Qur-aan nyuma yake, na anapotoa dalili anasema amesema Al-Akhtwalu (Mshairi wa Kikristo).

 

 

 

والمؤمنون يَـرَوْنَ حقـاً ربَّهُمْ *** وإلى السَّمـاءِ بِغَيْرِ كَيْفٍ يَنْزِلُ

Na waumini watamuona kwa uhakika kabisa Rabb wao, na kuielekea mbingu ya dunia (Allaah) Anashuka bila namna (mfano).

 

 

 

وأُقِرُ بالميـزانِ والحَوضِ الذي *** أَرجو بأنِّي مِنْـهُ رَيّاً أَنْهَلُ

Na ninakiri mizani na hodhi ambalo, natarajia kuwa mimi kutokana na hodhi hilo kiu nitakata.

 

 

 

وكذا الصِّراطُ يُمَدُّ فوقَ جَهَنَّمٍ *** فَمُوَحِّدٌ نَاجٍ وآخَـرَ مُهْمِلُ

Na hivyo hivyo Swiraatw (njia) itakunjuliwa juu ya Jahannam, basi mwenye kumpwekesha Allaah ni mwenye kuokoka na mwengine (asiyempwekesha Allaah) ni mwenye kupuuzwa (ataporomokea Jahannam).

 

 

 

والنَّارُ يَصْلاها الشَّقيُّ بِحِكْمَةٍ *** وكذا التَّقِيُّ إلى الجِنَانِ سَيَدْخُلُ

Na Moto atauingia muovu kwa hekima yake Allaah, na hivyo hivyo mwenye kumcha Allaah katika mabustani ataingia.

 

 

 

ولِكُلِّ حَيٍّ عاقـلٍ في قَبـرِهِ *** عَمَلٌ يُقارِنُـهُ هناك وَيُسْأَلُ

Na analo kila aliye hai mwenye akili katika kaburi lake, tendo ambalo litasuhubiana naye huko na ataulizwa.

 

 

 

هذا اعتقـادُ الشافِعيِّ ومالكٍ *** وأبي حنيفـةَ ثم أحمدَ يَنْقِـلُ

Hii ni itikadi ya Ash-Shaafi’iy na Maalik,na Abuu Haniyfah kisha Ahmad hunukuliwa.

 

 

 

فإِنِ اتَّبَعْتَ سبيلَهُمْ فَمُوَحِّـدٌ *** وإنِ ابْتَدَعْتَ فَما عَلَيْكَ مُعَوَّلً

Ikiwa utafuata mwenendo wao basi utakuwa ni mwenye kuafikishwa, na ikiwa utazusha basi huna wewe mahali pa kuegemea.

 

 

 

 

Share