Ni Nani Ahlul-Hadiyth?

 

Ni Nani Ahlul-Hadiyth?[1]

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Ahlul-Hadiyth:

 

Shaykh ul-Islaam amesema: 'Hatuna maana ya kuweka kikomo Ahlul-Hadiyth (watu wa Hadiyth) kwa wale tu wanaofikisha hadiyth, wanaoziandika au kuzihadithia; bali (tusemapo hivyo) twamaanisha: Kila mtu wa haki ambaye kahifadhi hadiyth, kazijua na kuzifahamu maana yake ya dhahiri na ya siri na kuzifuata katika yale ya dhahiri na ya siri, na pia (ni) watu wa Qur-aan.'

 

Anaendelea (kusema Shaykh):

 

'Sifa zao ni, mapenzi kwa Qur-aan na Hadiyth, kuzifanyia utafiti,
kutafuta maana zao na kuzifanyia kazi kwa yale wanayojua yanaambatana kwazo. Fuqahaa (wanachuoni) wa Hadiyth ni bora zaidi kumhusu Nabiy (Swalla Allaahu `alayhi wa aalihi wa sallam) kuliko Fuqahaa wengine zaidi yao.'[2]

 

Anataja:

'Ahlul-Hadiyth ni wale ambao Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu `alayhi wa aalihi wa sallam) kawazungumzia kwa kusema: 'Ni wale watakaokuwa (wanafuata) niliyomo mimi na Swahaba wangu.' Na katika riwaya nyingine: 'Ni Jamaa`ah, Mkono wa Allaah Uko juu ya Jamaa`ah.'[3]

 

Ahlul-Hadiyth ni watu bora Duniani, kama Hafsw bin Ghayaath alivyosema.[4]

 

Ash-Shafi'iy kasema: Ninapoona mtu wa Hadiyth basi ni kama kwamba nimeona mtu katika Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu `alayhi wa aalihi wa sallam) ni katika hadhi hiyo.'

 

Pia akasema:

'Allaah Awalipe mema kwa niaba yetu, walihifadhi msingi kwa ajili yetu, kwa hiyo ni bora juu yetu.'[5]

 

'Aliy bin al-Madiyni amesema: 'Hakuna watu bora kuliko watu wa
Hadiyth. Watu wengine walikuwa wako katika kutafuta Dunia, wakati wao walikuwa wako katika kusimamisha Dini[6] sawa; yaani Sunnah'

 

Haafidhw Ibn Rajab kasema:

'Ahlul-Hadiyth ni mamlaka ya kujua Hadiyth na kujua Hadiyth sahihi kutoka dhaifu.'[7]

 

Nabiy (Swalla Allaahu `alayhi wa aalihi wa sallam) kamuombea du`aa ya nuru kwa yule mtu ambaye anajishughulisha mwenyewe na elimu ya Hadiyth, kuzihifadhi, kuzitangaza na kuzifahamu. 

 

Yeye Nabiy (Swalla Allaahu `alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Allaah Anampenda mtu aliyesikia kitu kutoka kwetu na akakifikisha kama vile alivyokisikia, huenda mfikishiwaji akafahamu vizuri zaidi kuliko aliyesikia” na katika mapokezi mengine “Huenda mbebaji Fiqh akaipeleka Fiqh kwa aliye mweledi zaidi  yake, na wakati mwingine mbebaji wa Fiqh akawa si mweledi.”[8]

 

Haafidhw Abu Bakr Ahmad bin 'Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy mwandishi hasa wa kitabu ambacho kinaitwa 'Sharaf Aswhaabil-Hadiyth' (heshima ya watu wa Hadiyth). Ndani yake kataja Ahaadiyth na Aathaar kutoka kwa Swahaba, Taabi´iyn, wafalme, mawaziri na wengine kutoka kwa wale wanaowafuata juu ya ubora wa elimu ya Hadiyth, kujishughulisha nayo na heshima ya watu wake juu ya Ahlul-Bid´ah na wale watu wapotofu miongoni mwa Zanaadiqah (wanafiki) ambao wanajishughulisha sana na elimu ya balagha na falsafa. Kitabu hiki (cha al-Khatwiyb al-Baghdaadiy) ni muhimu sana katika somo hili.'

 

 
 

 

 

 

[1] Imechukuliwa kutoka 'Mustwalah Mu'jam al-Hadiyth wa Latwaaif al-Asaaniyd' uk. 61-63.

 

[2]  Majmuw' al-Fataawa a(4/95).

 

[3] Majmuw' al-Fataawa (3/345-347).

 

[4] Al-Ilma' uk. 27.

 

[5] Mas-alat al-'Uluw wal Nuzuwl, uk. 45.

 

[6] Mas-alat al-'Uluw wan-Nuzuwl, uk. 45.

 

[7] Jamu'l-’Uluwm wal-Hikam (2/105).

 

[8] Imesimuliwa na Abu Daawuwd (4/69), At-Tirmidhiy (5/33) kwa njia ya `Umar bin Sulaymaan kuanzia mtoto wa `Umar bin Al-Khattwaab, juu ya mamlaka ya `Abdur-Rahmaan bin Abaan, juu ya mamlaka ya baba yake, kwa mamlaka ya Zayd bin Thaabit (Radhwiya Allaahu ’anhu) Marfuu'. Pia imesimuliwa na Ibn Maajah (1/84) njia mbalimbali kutoka kwa Zayd bin Thaabit. At-Tirmidhiy kasema ni Hasan na pia kasema: 'katika mlango huu imesimuliwa kutoka kwa ’Abdullaah bin Mas'uwd, Mu`aadh bin Jabal, Jubayr bin Mutw'im, Abu Dardaa na Anas – (Radhwiya Allaahu 'anhum).

 

Share