097-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 097: قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah Aayah: 97 - 101: Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika
قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾
97. Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini
مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾
98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rasuli Wake, na Jibriyl, na Miykaala, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri.
وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾
99. Na kwa yakini Tumeteremsha kwako Aayaat bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.
أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Je, ndio kila wanapochukua ahadi kundi miongoni mwao huivunja? Bali wengi wao hawaamini.
وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٠١﴾
101. Na alipowajia Rasuli kutoka kwa Allaah mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao kundi miongoni mwa wale waliopewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui (yaliyomo humo).
Sababun-Nuzuwl:
Aayah zimeteremka hali ya kuwa ni jawabu kwa Mayahudi miongoni mwa wana wa Israaiyl, pale walipodai kuwa Jibriyl ((عليه السلام ni adui yao. [Imaam Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)] kwamba:
حضرت عصابة من اليهود نبيّ الله صلى الله عليه وسلم
فقالوا:حدِّثنا عن خلال نسألك عنهن لا يعلمهن إلا نبي.
قال : سَلُونِي عَمَّا شِئْتُمْ ، وَلَكِنْ اجْعَلُوا لِي ذِمَّةَ اللَّهِ، وَمَا أَخَذَ يَعْقُوبُ عَلَى بَنِيهِ لَئِنْ أنا حَدَّثْتُكُمْ شَيْئًا فَعَرَفْتُمُوهُ لَتُتَابِعُنِّي عَلَى الإسْلامِ
قَالُوا:فَذَلِكَ لَكَ.
قَالَ : فَسَلُونِي عَمَّا شِئْتُمْ
قالوا:أَخْبرْنَا عن أربع خلال:أَخْبرْنَا أَيُّ الطعام حَرَّمَ إسرائيل على نفسه ؟ وكيف ماء المرأة وماء الرجل؟ كيف هذا النبي الأمّي في النوم؟ ومن وَليّه من الملائكة؟
فأخذ عليهم العهد لئن أخبرهم ليتابعنه
وقال : أَنْشُدُكُمْ بِالَّذِي أَنزلَ التَّوْرَاةَ عَلَى مُوسَى:هَلْ تَعْلَمُونَ أَنَّ إِسْرَائِيلَ مَرِضَ مَرَضًا شَدِيدًا وَطَالَ سُقْمُهُ ، فَنَذَرَ لِلَّهِ نَذْرًا لَئِنْ شَفَاهُ اللَّهُ مِنْ سُقْمِهِ لَيُحَرِّمَنَّ أَحَبَّ الشَّرَابِ إِلَيْهِ وَأَحَبَّ الطَّعَامِ إِلَيْهِ ، وَكَانَ أَحَبَّ الطَّعَامِ إِلَيْهِ لُحْمان الإبِلِ ، وَأَحَبَّ الشَّرَابِ إِلَيْهِ أَلْبَانُهَا
فقالوا:اللهم نعم.
قال: اللَّهُمَّ اشْهَدْ عَلَيْهِمْ
وقال : أَنْشُدُكُمْ بِاللَّهِ الَّذِي لا إِلَهَ إِلا هُوَ، الَّذِي أَنزلَ التَّوْرَاةَ عَلَى مُوسَى:هَلْ تَعْلَمُونَ أَنَّ مَاءَ الرَّجُلِ أَبْيَضُ غَلِيظٌ ، ومَاءَ الْمَرْأَةِ أَصْفَر رَقِيقٌ، فَأَيُّهُمَا عَلا كَانَ لَهُ الولد وَالشَّبَهُ بإذنِ اللَّهِ ، إِنْ عَلا مَاءُ الرَّجُلِ مَاءَ المرأة كَانَ ذَكَرًا بِإِذْنِ اللَّهِ وَإِنْ عَلا مَاءُ الْمَرْأَةِ مَاءَ الرَّجُلِ كَانَ أُنْثَى بِإِذْنِ اللَّهِ
قالوا:نعم.
قال: اللَّهُمَّ اشْهَدْ عَلَيْهِمْ
وقال: أَنْشُدُكُمْ بِالَّذِي أَنزلَ التَّوْرَاةَ عَلَى مُوسَى:هَلْ تَعْلَمُونَ أَنَّ هَذَا النَّبِيَّ الأمِّيَّ تَنَامُ عَيْنَاهُ وَلا يَنَامُ قَلْبُهُ
قالوا:اللهم نعمْ .
قَالَ: اللَّهُمَّ اشْهَدْ
قالوا:وأنت الآن فحدثنا منْ وليُّك من الملائكة؟ فعندها نجامعك أو نفارقك
قال: إِنَّ وَلِيِّيَ جِبْرِيلُ، وَلَمْ يَبْعَث اللَّهُ نَبِيًّا قَطُّ إِلا وَهُوَ وَلِيُّهُ
قالوا:فعندها نفارقك، ولو كان وليك غيره لتابعنَاك ، فعند ذلك قال الله تعالى: ((قُلْ مَنْ كَانَ عَدُوًّا لِجِبْرِيلَ ...))
Kundi miongoni mwa Mayahudi lilihudhuria kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema: Yaa Abaa Qaasim! Tuelezee kuhusu tunayokuuliza kwani hayajui isipokuwa Nabiy. Akasema: “Niulizeni mnayotaka lakini niwekeeni ahadi kwa Allaah (kama ahadi) aliyofungamana Ya’quwb kwa wanawe, kuwa nikikuhadithieni jambo mkalijua, mtanifuata katika Uislamu.” Wakasema: Umelipata hilo! (tumekubali). Akasema: “Niulizeni mtakacho.” Wakasema: Tuelezee mambo manne tutakayokuuliza; Tueleze ni chakula gani alichojiharamishia Ya’quwb kabla ya kuteremshwa Tawraat? Na tueleze vipi yanakuwa maji (manii) ya mwanamme na mwanamke, na vipi anakuwa (mtoto) wa kiume anayetokana na maji hayo? Na tueleze vipi anakuwa usingizini huyu Nabiy ambaye hajui kusoma? Na nani anakuwa kipenzi chake katika Malaika? Akasema: “Je mnanipa ahadi kwa Allaah kuwa nikikuelezeni mtanifuata?” Ibn ‘Abbaas akasema: Mayahudi wakampa ahadi. Akasema: “Nakuapieni kwa Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa (عليه السّلام). Hivi mnajua kuwa Ya’quwb aliugua maradhi makali, yakakaa muda mrefu maradhi yake? Akaweka nadhiri kwa Allaah kuwa, endapo atapona maradhi yake, atajiharamishia vinywaji avipendavyo sana na vyakula avipendavyo sana? Na kilikuwa chakula akipendacho zaidi nyama ya ngamia na kinywaji akipendacho zaidi ni maziwa yake?” Wakasema: Allaahumma na’am! Akasema: “Yaa Allaah Washuhudie! Na nakuapieni kwa Allaah Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa ((عليه السلام, hivi mnajua kuwa maji ya mwanamme ni meupe mazito, na maji ya mwanamke ni ya njano mepesi? Basi moja ya maji hayo yakiwa juu ya mengine, anakuwa jinsia yake huyo mtoto na kufanana naye kwa Idhini ya Allaah. Na endapo yakiwa maji ya mwanaume juu ya maji ya mwanamke, anakuwa (mtoto) wa kiume, na yakiwa maji ya mwanamke juu ya mwanamme, anakuwa wa kike kwa idhini ya (Allaah سبحانه وتعالى)?” Wakasema: Allaahumaa na’am! Akasema: “Yaa Allaah Washuhudie! Na nakuapieni kwa Allaah Ambaye Ameteremsha Tawraat kwa Muwsaa, hivi mnajua kuwa huyu Nabiy asiyejua kusoma (kuwa) yanalala macho yake wala haulali moyo wake?” Wakasema: Allaahumma na’am! Akasema: “Yaa Allaah Shuhudia!” Wakasema: Basi sasa wewe tuelezee ni nani kipenzi chako katika Malaika? Hapo ndio tutakuwa na wewe au tutafarikiana. Akasema: “Hakika kipenzi changu ni Jibriyl na wala Allaah Hakutuma Nabiy yeyote ila anakuwa kipenzi chake.” Wakasema: Hapo ndio tunafarikiana! Lau angekuwa kipenzi chako mwengine katika Malaika tungekufuata na tungekusadikisha. Akasema: “Kipi kinachokuzuieni kumsadikisha?” Wakasema: Hakika yeye ni adui yetu. Ibn ‘Abbaas akasema: Hapo ndipo Alipoteremsha Allaah Ta’aala: “Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako...” mpaka Kauli ya Allaah [Aayah (2:101)] “...Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui.” Na hapo wakastahiki ghadhabu juu ya ghadhabu (2:90) Suwrah Al-Baqarah) [Musnad Ahmad (2384). Ni Hadiyth Swahiyh kwa mkusanyiko wa njia zake na imenukuliwa Ijmaa’ juu ya usahihi wake]