109-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 109: ‏وَدَّ كَثِيرٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُمْ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا

 

 

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Al-Baqarah Aayah  109: Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani kama wangelikurudisheni...

 

 

وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٩﴾

Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani kama wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri kwa husuda iliyomo katika nafsi zao; baada ya kuwabainikia kwao haki. Basi sameheni na puuzeni; mpaka Allaah Alete amri Yake. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

عن أُسَامَةَ بْنَ زَيْدٍ رضى الله عنهما ـ أَخْبَرَهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَكِبَ عَلَى حِمَارٍ عَلَى قَطِيفَةٍ فَدَكِيَّةٍ، وَأَرْدَفَ أُسَامَةَ بْنَ زَيْدٍ وَرَاءَهُ، يَعُودُ سَعْدَ بْنَ عُبَادَةَ فِي بَنِي الْحَارِثِ بْنِ الْخَزْرَجِ قَبْلَ وَقْعَةِ بَدْرٍ ـ قَالَ ـ حَتَّى مَرَّ بِمَجْلِسٍ فِيهِ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ، ابْنُ سَلُولَ، وَذَلِكَ قَبْلَ أَنْ يُسْلِمَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ فَإِذَا فِي الْمَجْلِسِ أَخْلاَطٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُشْرِكِينَ عَبَدَةِ الأَوْثَانِ وَالْيَهُودِ وَالْمُسْلِمِينَ، وَفِي الْمَجْلِسِ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ رَوَاحَةَ، فَلَمَّا غَشِيَتِ الْمَجْلِسَ عَجَاجَةُ الدَّابَّةِ خَمَّرَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ أَنْفَهُ بِرِدَائِهِ، ثُمَّ قَالَ لاَ تُغَبِّرُوا عَلَيْنَا‏.‏ فَسَلَّمَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَيْهِمْ ثُمَّ وَقَفَ فَنَزَلَ فَدَعَاهُمْ إِلَى اللَّهِ، وَقَرَأَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنَ، فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ أَيُّهَا الْمَرْءُ، إِنَّهُ لاَ أَحْسَنَ مِمَّا تَقُولُ، إِنْ كَانَ حَقًّا، فَلاَ تُؤْذِينَا بِهِ فِي مَجْلِسِنَا، ارْجِعْ إِلَى رَحْلِكَ، فَمَنْ جَاءَكَ فَاقْصُصْ عَلَيْهِ‏.‏ فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ رَوَاحَةَ بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَاغْشَنَا بِهِ فِي مَجَالِسِنَا، فَإِنَّا نُحِبُّ ذَلِكَ‏.‏ فَاسْتَبَّ الْمُسْلِمُونَ وَالْمُشْرِكُونَ وَالْيَهُودُ حَتَّى كَادُوا يَتَثَاوَرُونَ، فَلَمْ يَزَلِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يُخَفِّضُهُمْ حَتَّى سَكَنُوا، ثُمَّ رَكِبَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم دَابَّتَهُ فَسَارَ حَتَّى دَخَلَ عَلَى سَعْدِ بْنِ عُبَادَةَ، فَقَالَ لَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ يَا سَعْدُ أَلَمْ تَسْمَعْ مَا قَالَ أَبُو حُبَابٍ ‏"‏‏.‏ يُرِيدُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ أُبَىٍّ ‏"‏ قَالَ كَذَا وَكَذَا ‏"‏‏.‏ قَالَ سَعْدُ بْنُ عُبَادَةَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، اعْفُ عَنْهُ وَاصْفَحْ عَنْهُ، فَوَالَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ، لَقَدْ جَاءَ اللَّهُ بِالْحَقِّ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ، لَقَدِ اصْطَلَحَ أَهْلُ هَذِهِ الْبُحَيْرَةِ عَلَى أَنْ يُتَوِّجُوهُ فَيُعَصِّبُونَهُ بِالْعِصَابَةِ، فَلَمَّا أَبَى اللَّهُ ذَلِكَ بِالْحَقِّ الَّذِي أَعْطَاكَ اللَّهُ شَرِقَ بِذَلِكَ، فَذَلِكَ فَعَلَ بِهِ ما رَأَيْتَ‏.‏ فَعَفَا عَنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم وَأَصْحَابُهُ يَعْفُونَ عَنِ الْمُشْرِكِينَ وَأَهْلِ الْكِتَابِ كَمَا أَمَرَهُمُ اللَّهُ، وَيَصْبِرُونَ عَلَى الأَذَى قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏{‏وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا}‏ الآيَةَ، وَقَالَ اللَّهُ ‏{وَدَّ كَثِيرٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُمْ مِنْ بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِنْ عِنْدِ أَنْفُسِهِمْ}‏ إِلَى آخِرِ الآيَةِ، وَكَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَتَأَوَّلُ الْعَفْوَ مَا أَمَرَهُ اللَّهُ بِهِ، حَتَّى أَذِنَ اللَّهُ فِيهِمْ، فَلَمَّا غَزَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَدْرًا، فَقَتَلَ اللَّهُ بِهِ صَنَادِيدَ كُفَّارِ قُرَيْشٍ قَالَ ابْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ، وَمَنْ مَعَهُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ، وَعَبَدَةِ الأَوْثَانِ هَذَا أَمْرٌ قَدْ تَوَجَّهَ‏.‏ فَبَايَعُوا الرَّسُولَ صلى الله عليه وسلم عَلَى الإِسْلاَمِ فَأَسْلَمُوا‏.

 

Imehadithiwa na Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipanda punda aliyefunikwa kitambaa kizito cha fadakiyyah na Usaamah alikuwa amepanda naye nyuma yake. Alikuwa anaenda kumtembelea Sa’ad bin ‘Ubaadah Al-Haarith bin Al-Khazraj kabla ya vita vya Badr.  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawapitia watu katika majlisi ambako alikuweko ‘Abdullaah bin ‘Ubay  bin Saluwl na hapo kabla ya ‘Abdullaah bin Ubay kuingia Uislaam (juu ya kuwa alibakia kuwa mnafiki). Katika kikao hicho walikuweko mchanganyiko wa Waislaam na washirikina, wanaoabudu masanamu na Mayahudi. Na katika majlisi hiyo alikuweko pia ‘Abdullaah bin Rawaahaa. Wingu la vumbi alolivurumisha punda huyo lilipowafunika watu hao, ‘Abdullaah bin ‘Ubay alisema: “Usitufunike na vumbi!” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasalimia akasimama na kuteremka chini kisha akawalingania katika Uislaam na akawasomea Qur-aan. Hapo ‘Abdullaah bin Ubay bin Saluwl akasema: “Hakika hakuna unachosema isipokuwa ni mazuri. Ikiwa ni haki basi usituudhi kwayo katika majlisi yetu. Rudi katika kipando chako na atakapokujia mtu hapo msimulie (visa vyako).” Hapo ‘Abdullaah bin Rawaaha akasema: “Naam Ee Rasuli waAllaah, tuletee (uyesamayo) katika majlisi yetu, kwani hakika tunayapenda.” Hapo Waislaam, washirikina na Mayahudi wakaanza kutuhumiana mpaka wakakaribia kupigana. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anawanyamazisha mpaka wakabakia kimya, kisha hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akampanda mnyama wake akaendelea mpaka akafika kwa Sa’d bin ‘Ubaadah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Je hukumsikia alivyosema Abuu Hubaab.” Alikusudia ‘Abdullaah bin ‘Ubay. “Amesema kadhaa wa kadhaa.” Sa’ad bin ‘Ubaadah akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Msamehe na mpuuze kwani naapa kwa Ambaye Amekuteremshia Kitaab, hakika Allaah Ameleta haki ambayo Amekuteremshia kipindi ambacho watu wa mji huu (Madiynah) wameamua kwa shauri moja kumvisha taji na kumfunga kilemba kichwani mwake (kumchagua kuwa kiongozi). Lakini Allaah Alipokataa hayo kwa haki Aliyokupa basi yeye (‘Abdullaah bin ‘Ubay) amesikitika kwa wivu na ndio ikamfanya afanye uliyoyaona.”  Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsamehe kwani Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake walikuwa wakisamehe washirikina na Ahlul-Kitaab kama Allaah Alivyowaamrisha na walikuwa wakivumilia maudhi. Allaah  (عزّ وجلّ)  Akasema:   “na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale walioshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni mambo ya (thamani yapasayo) kuazimiwa (Aal-‘Imraan: 185) na Akasema Allaah: “Wengi katika Ahlil-Kitaab wametamani kama wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri kwa husuda iliyomo katika nafsi zao; (mpaka mwisho wa Aayah Al-Baqarah 2: 109). Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akishikilia kuwasemehe madamu Allaah Amemuamrisha mpaka Allaah Alipompa idhini ya kuwapiga vita.  Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipopigana vita vya Badr na Akawaua wakuu wa ki Quraysh kwa idhini ya Allaah, basi  ‘Abdullaah bin Ubay bin Saluwl na washirikina na waalioabudu masanamu wakasema: “Jambo hili (la Uislaam) limeelekea ushindi.” Hapo wakam baa’iy Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kiapo cha kuingia Uislaam wakawa Waislaam.” [Al-Bukhaariy katika Kitaab At-Tafsiyr]

 

 

Sababun-Nuzuwl: Kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete Amri Yake…” (2:109). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipanda punda akamwambia Sa’d: “Je hukusikia alivyosema Abuu Hubaab?” (akikusudia ‘Abdullaah bin Ubayy. “Amesema kadhaa wa kadhaa.” Sa’d bin ‘Ubaadah akasema: “Msamehe na puuza, basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsamehe. Na alikuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake wakiwasamehe Ahlul-Kitaab na Washirikina, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete Amri Yake…”   [Amehadithia ‘Urwah kutoka kwa Usaamah bin Zayd, amepokea Abuu Ash-Shaykh katika Al-Akhlaaq].

 

An-Naasikh Wal-Mansuwkh: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete amri Yake” kuwa imefutwa hukmu yake kwa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “Basi waueni washirikina popote muwakutapo” (9:5) na “Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho” (9:29).

 

 

Share